Tukumbuke majina ya utani kwa walimu shule tulikotoka

Tukumbuke majina ya utani kwa walimu shule tulikotoka

Kentow_mwalim wangu mkuu shule y secondary alikuw mkali knyamaaaaa an na alikuw ananyoa kipara
 
Mabesi: huyu alikuwa mwalimu wetu wa kemia na biology alikuwa ana sauti kama simba mzee
 
Kamtambo; mwalimu wangu wa shule ya msingi, alikuwa anachapa huyo kama machine.. Tukamuita kamtambo

Chief; ni mwalimu wangu tena wa shule ya msingi, yeye alikuwa anataka ela ya quiz wakati quiz ni bure.. Tukamuita chief

Mkuna K... Alikuwa anapenda sana wanawake.. Na jina lake anaitwa mkunala ... Tukamuita mkuna K
 
Ng'ombe alikuwa anachapa utadhani anaua nyoka.
 
Nakumbuka baadhi ya majina ya walimu waliyopewa na wanafunzi kama ifuatavyo:

1. Solar system - mwalimu wa geograph form 1 au 2 alifundisha solar system akapatiwa jina hapohapo

2. Bambabay - mwalimu wa commerce form 3 alikua akielezea transport system,akaitaja bambabay ndio ikawa jina lake.

3.Magazijuto - mwalimu wa hisabati darasa la saba alifundisha magazijuto na yeye ndio ikawa jina lake la utani au aka

4. Chonya of chilimwa - mwalimu wa kiswahili secondary alisoma habari za chonya of chilomwa akawa ndio jina lake

tupeni majina zaidi
# we masharabu weweeeeee
 
Doppler effect ! Uyu Ticher alichukua terms Nzima kutufundisha topic ya WAVE function form 6!!
 
Doppler effect ! Uyu Ticher alichukua terms Nzima kutufundisha topic ya WAVE function form 6!!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] huyo ni kibokoooh khaaaah, chezea phys weyeeeeh
 
Mwalimu dudu ,alikua mwalimu wa history alikua anatembeza stiki,afu alikua aoni aibu kujamba class😀😀😀
 
"Ni Kwamba"--huyu alikuwa mwalimu wetu wa Siasa enzi hizo. Alikuwa kila baada ya sentesi 2 anatumbukiza "ni kwamba",siku moja tukaamua kumuhesabia hizo ni kwamba zinakuwa ngapi ktk kipindi cha dk 45;jamaa yetu akahesabu zikafika 78,basi ndo likawa jina lake hilo.
😁😁
 
BABU= Mwl wangu wa Hisabati primary,umri ulikuwa umeenda
CHAI=mwl. wa nidhamu primary viboko alikuwa akiita chai
KJ= Mwl wa Motor vehicle mechanics alikuwa mdoko balaa wanafunzi wakambatizaj ina la Kubwa Jinga so wakalifupisha kuwa KJ,ticha akadhani wanamsifia basi siku moja akasimama parade na kuanza kujitapa "mimi ndiye Kamanda wa Jeshi au KJ wanafunzi hoi ila kuna baadhi ya maticha walijua mchezo wakamtonya mbona ilikuwa shida.
COMANDO= 2nd Master Secondary alikuwa mnoko balaa afu alikuwa kajazia kifua.
CALLIPER= mwl wa Engineering Science
MABALA=mwl wa English
NGOSWE/FASIHI= mwl wa kiswahili.

Arusha Tech Mkuu chuo alikuwa akiitwa Mbosoli wakati wa uongozi wake pale chuoni kulikuwa na mikate fulani midogo inaokwa kwaajili ya wanachuo tukaibatiza jina la "vimbosoli"
Mungu anawaona
 
lufufu, dah huyu mwalimu bana alikua anakuja darasani anatutafsiria physical geography.
yani yeye anasoma tu kile kitabu anamaliza kufundisha.
 
Udaba alikuwa head master
Kirinyaga mwalimu wa kiswahili
Kichwa mwalimu wa History
 
Back
Top Bottom