Tukumbuke majina ya utani kwa walimu shule tulikotoka

Tukumbuke majina ya utani kwa walimu shule tulikotoka

Nakumbuka baadhi ya majina ya walimu waliyopewa na wanafunzi kama ifuatavyo:

1. Solar system - mwalimu wa geograph form 1 au 2 alifundisha solar system akapatiwa jina hapohapo

2. Bambabay - mwalimu wa commerce form 3 alikua akielezea transport system,akaitaja bambabay ndio ikawa jina lake.

3.Magazijuto - mwalimu wa hisabati darasa la saba alifundisha magazijuto na yeye ndio ikawa jina lake la utani au aka

4. Chonya of chilimwa - mwalimu wa kiswahili secondary alisoma habari za chonya of chilomwa akawa ndio jina lake

tupeni majina zaidi
Paree: Alikuwa mwalimu wa somo la biology jina lake lilitokana na parenchyma 😂😂😂😂😂😂
 
Hii wapi? Mkoa gani?

ISNT IT, mwl wa kemia f2 alikuwa kila baada ya sentens anasema isnt it ndo likawa jina lake.
NTAKULIMA, Alikuwa akikukuta na kosa anakuambia ntakulima bakora.
KISIKIO. Sikio lake moja lilikuwa kama limekatwa
 
Mwl. Kalaghabao popote ulipo nakusabahi sana
 
Diski mweku. ,, Mwalimu wa kiswahili alietueleza kwamba komputer kwa kiswahili ni diskimweku.. basi kuanzia huyo siku msela ni diski mweku hata leo
 
Liteacher letu la BIOLOGY A-level lilikuwa linafunga nywele badala ya kufuga kuku, tukalipa jina teacher k.mwaunywele
 
Anyone anamkumbuka mwalimu SIHUSIKI from kwakilosa secondary school
 
Makondoo..alikua ticha wa agriculture, alikua anapend kuita wanafunzi kondoo jina likamgeukia yeye siku alipojua wanamwita hivy shule nzma tukapig kura km ulishawah kusikia mwanafunz anaita unampigia kura af zinaenda kusomwa staff ilikua kam zoez l siku 3 iv
 
Kwa wanangu wa balangdalalu
Express - teacher wa English anapenda sana kuwaambia mwanafunz what's your problem express your problem.
Sharo - jamaa moja alikujaga katika chuo anatembea anadunda kinomah
Kuna siku tumedoji akatukimbiza tukakimbilia kwa shamba
Nilikuwa na mtaro wa maji machafu ulikuwa umeota majani ,tuka mtegea akadumbukia
Alisikika akisema ebhana dah kukimbizana nao ni noma

Kikotii/Survey - alikuja form 3 ,during survey na lafudhi yake ya kihaya akawa kituko ,suruali imeungwa kiunoni huyo Sam

Iyunga tech
Kiege- ticha wa ufundi
Mtanzania- anapenda kuita wanafunzi wa Tanzania
Zombie 1& zombie 2- mijamaa inatembea haileweki
 
Lomolomo - Mwl. Kiswahili
Waluwalu - Mwl. Maths
Bambucha - Mwl. English
Bajada - Mwl. Geography
 
Fuvu:
huyu alikuwa discipline master. noma. mwembambaaaa kama snoop dogg.

Kisu:
Bonge la headmaster niliyewahi kumuona. Aligeuza shule iliyokuwa ya wahuni kuwa shule yenye heshima inayofaulisha kwa kiwango cha juu bila mitihani kuvuja. Huyu jina yake kamili ni Kisusange. Kuna wakati alihamaki, akauliza wanafunzi: "naskia kuna wanafunzi wananiita Kisu, hivi wewe baba yako unaweza kumuita ba?"
Huyu fuvu alimrithi mapafu.alikuwa mkatili mno.

Kisu Ana bahati Sana tulimkosakosa yeye na nyumba yake kuchoma moto.alisababisha mgomo mbaya kabisa ambao ulileta uharibifu mkubwa mno.aliletwa shuleni kwetu baada ya kupata demotion huko wizarani,Basi hasira zake akaja nazo shuleni akaishia kusabibisha mgomo na vutugu.nakumbuka tulifukuzwa wanafunzi 45 hivi.
Lakini tunashukuru baada mgomo Hali ilibadilika na Mambo yakaboreshwa.umenikumbusha mbali bila kufukuzwa hapo ningekuwa mtu wa hivyo mno.
 
Back
Top Bottom