Baba wa taifa mwaka 1995 wakati wa kampeni za kumnadi Mkapa alisema hawezi kuiacha nchi yake iongozwe na mbwa,wengi hawakumuelewa kipindi kile kwa kudhani alimaanisha wapinzani hasa Mrema ambaye alikuwa juu kipindi kile,tujaribu kukumbuka ni watu gani Mwal Nyerere alikuwa akiwapinga kupewa madaraka makubwa ndani ya chama,na vile vile kupinga wasichaguliwe kuwania uraisi wakati ule,kwa sasa tunaona kile alichokimaanisha Mwalimu wakati ule kwani wale aliowapinga,wanatuonyesha fika ni kwanini Mwalimu aliwaita MBWA,kwani mbwa ni mroho wa mifupa siku zote na yuko tayari kufanya chochote ili abaki na mfupa wake na wengine wasipate hata kama ni kuua yuko tayari,TUKUMBUKE MANENO YALE NA NI YUPI ALIYEKATALIWA NA MWALIMU KIPINDI KILE????.
.
LAKINI BASI tumjadili huyu Kiongozi mwenye Tabia za Mbwa tuone. Yukoje Na tuiconclude statement ya Mzee wetu huyu.
.
1:-By the way Mbwa humlinda binadam so mbwa ana umuhimu Wa kipekee sana. Tofauti Na sasa ambapo binadamu hatulindwi ndio kwanza tunanyukwa mabom Na kulipuliwa Na serikali yetu.
2:- Mbwa hajui rushwa, ufisadi, hajikusanyii mali, si mlevi
Yeye anabite tu Penye makosa. So mbwa ni Muhimu sana Kwa Tanzania ya Leo. Kiongozi wetu Ws leo Hana memo, wazi, wala rushwa waziwazi wanapeta tu.
3:-mbwa yuko alert 24 hours, halali fofofo so ni Muhimu sana Kwa kulinda Uchumi na Rasilimali Za Nchi yetu visikwibwe na Mijitu ya ufisadi wa kukufuru. Kiongozi wetu wa Leo wako Na usingizi mzito sana kiasi ulinzi wa Mali Na Rasilimali zetu uko NJE NJE. Imagine Wachina, wamarekani wanakuja kujichotea tu Mali hizo hizo ambazo babu alisema waachiwe watanzania wakikua watachimba wenyewe.
3:-Mbwa kila siku yuko home akiilinda Nyumba but kiongozi wetu yuko bize masafa huyooo, kila siku anajibataaaz majuu si mbaya sana lakini..
4:- mbwa wana Uwezo wa kunusa hatari, lakini Kiongozi wetu Wa Leo Hapana hatari inayonuswa, inteligencia yetu pua zake zishaziba siku mingi sana kiasi mpaka mabomu yanawalipukia wananchi hawajanusa kabisaa harufu ya Hatari.
5:- mbwa hupandiana tu Kwa vipindi vya jotoridi lao Kwa ajili ya uzazi tu Na the rest of the time wanachapa Kazi, lakini VIONGOZI wetu wa Leo wanapandiana pandiana tu all the time Na kuwa Na utitiri wa nyumbakubwaz Na ndogoz Na matotoz plus kudisturb future ya mabint zetu..
Inatosha bana wasije ning'oa kucha bure