Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha

...ndio maana Shk Abeid Amaan Karume aliamrisha wananchi wote Unguja na pemba wakti huo kujitolea kujenga majumba ya maendeleo ya Michenzani, Kilimani mpaka Makunduchi, na serikali yake ilihakikisha kila mwenye flat anapatiwa 'Televisheni' kuona maendeleo, na Jiko la umeme, kuepusha kupikia kuni ndani ya flat.

...Wakti huo pia kulijengwa nyumba za wazee Kiembesamaki, kwa wale wasojiweza, leo hii nyumba za wazee Kiembesamaki ni wenye uwezo walozinunua, 🙁 , ...alipouwawa na kasi ya ujenzi wa haya majumba ikaishia hapo

 
Mchongoma sijaelewa hayo masaa

....Oh, pole mkuu,

Experience ya urubani inategemeana na masaa mangapi 'ume clock' ukiwa unarusha ndege (angani). Ile ndege muda mwingi ilikuwa angani hata bila 'Mkuu' mwenyewe.

BTW, ile presidential jet ya Komandoo Salmini, iliyo roll "yenyewe" (kwenye ground) na kupata ajali Lilongwe ilikuwa bahati mbaya au uzembe wa Rubani?
 
Nimekupata, nilimaanisha kwa mkuu hakuwa akifanya kazi ila kusafiri saana? kumbe ilikuwa angani bila ya hata yeye kuwepo.

Nani alikuwa anasafiri nayo? na kwa malengo yapi?
 
karume aliikuta zanzibar tajiri sana................ila maajabu badala ya kuipeleka mbele akairudisha nyuma!
 
karume aliikuta zanzibar tajiri sana................ila maajabu badala ya kuipeleka mbele akairudisha nyuma!

...hu ndio ukweli...na aliitumia pesa kwa vurugu sana .familia ya karume inamiliki property hadi marekani,amani na ali sio maskini wale hata kama wasingekuwa wanasiasa leo hii..na alipoongia aboud jumbe akazimalizia....

..hilo la kusema zanzibar ilifilisika kwa kutoa pesa kwenye vita kagera si kweli..kwani hata kama walitoa pesa hazingetosha kuendesha vita hata wiki moja..ila hatupuuzi mchango wao kwenye vita..lakini sio sababu ya kukauka hazina yao....
 
Picha Iiliyomwogopesha MKAPA ilipigwa Msikiti wa Mtambani baada ya mauaji ya Mwembechai

 
FMES said:
Hivi si nasikia kuna wakati serikali ya mapinduzi Zanzibar ilikuwa haidaiwi deni na serikali yoyote duniani, au?

FMES,mgirima,FairPlayer,Philemon Mikael,Kibunango,mchongoma,

..hata Tanganyika ilikuwa haidaiwi, na ilikuwa na akiba kwenye hazina, wakati tunapata uhuru 1961.

..serikali za mkoloni ilikuwa hai-invest kwenye huduma za kijamii[shule,barabara,hospitali,maji,...] ndiyo maana ikiweza kulimbikiza akiba wakati iko madarakani.

..serikali ya Sultani nayo ilikuwa haifanyi lolote lile kuinua hali ya Watumwa/Weusi kule Zanzibar.

..hebu tujiulize Wapemba wangapi walikuwa na access na hiyo TV ya rangi? Wazanzibari wangapi waliweza kwenda shule au hospitali, au walikuwa na access ya maji safi? i can go on and on.

..Karume naye alipokuja sidhani kama ali-invest zile fedha vizuri. alitakiwa kutoa kipaumbele ktk ujenzi wa viwanda, siyo nyumba za kutunza wazee bure.

..wakati Karafuu iko juu, Kahawa na Mkonge vilikuwa na bei nzuri sana. actually Tanganyika ilikuwa kati ya wazalishaji wakubwa wa mazao hayo mawili.

..miaka ya 70, kulipotokea OIL CRISIS ya kwanza, uchumi wa Tanganyika haukuyumba sana kwasababu ya mapato yaliyotokana na KAHAWA.

..kwa msingi huo hii minong'ono kwamba Tanganyika ndiyo imeifilisi Zanzibar ni ya kuitilia mashaka makubwa.

..Zanzibar imefilisika kutokana na kuanguka kwa zao la Karafuu. Pia serikali ya Zanzibar ni kubwa mno na mzigo kwa wananchi. zaidi Zanzibar wana imani potofu kwamba bandari yao itawasaidia kuliko viwanda.
 
wajameni tuseme ukweli japo unauma

Vita vya Uganda nini chanzo chake? na kwanini tulipitiliza mpaka tukafika hadi Sudan wakati tulihitaji kumuondosha adui nchini mwetu? hivi si kuivamia nchi ya watu kama sisi ndio wenyewe bila ya kutizama gharama? Kabla ya vita kulikuwa na silaha pale Zanzibar zilizokuja kutoka Urusi na zilinunuliwa na SMZ kwa pesa kamili sio mali kauli, zipo wapi silaha kutoka Tank mpaka ndege?
Tunaposema kuwa mtawala wa Zanzibar hakuwekeza kwenye maendeleo huko jee kina Aboud Jumbe na Ali Hassan walisoma wapi na serikali gani iliwasomesha, tutizame jee takwimu za 64 to go down (watu) kulingana na income na baada ya 64 to go up ipi ilikuwa juu? skuli ngapi zilizojengwa before Mapinduzi per population na standard ya elimu against school baada ya mapinduzi per population per standard?

Kweli tupinge ukoloni lakini mengi baada ya mapinduzi yaliyofanyika na kuendelea ni urudishaji nyuma wa maendeleo, baada ya mapinduzi kulikuwa hakuna audit na hayo tutizame nani walikuwa mawaziri na nani walikuwa wakiongoza? Mh Karume alikuwa hawapendi watu waliosoma, Muulizeni Mh Kassim Hanga, Othman Sharif na wengi kati yao ambao bila ya kosa isipokuwa usomi ndio ulowapeleka walipo

Aboud Jumbe, Hasnuu Makame, Othman Sharif, Kassim Hanga, Ali Hassan Mwinyi jee hawa walisomeshwa na nani na serikali gani
 
STATE DEPARTMENT nao katika kumbu kumbu mwaka 2002 walisema hivi:




Kisha wakaendelea kusema hivi:



Section II. Status of Religious Freedom

Legal/Policy Framework

The Constitution provides for freedom of religion, and the Government generally respects this right in practice, subject to measures that it claims are necessary to ensure public order and safety; however, there were a few limits on this right............

HALAFU patamu ni [anasema hivi kwenye hiyo ripoti ya STATE DEPT...



Restrictions on Religious Freedom


PATAMU NI HAPA:

A unique style of preventing suspects from running away. The police have tied up together the shirts of two highly respected Muslim leaders, Sheikh Ali Ali (71) and Sheikh Omar Mayunga (51) because the police found several copies of the Qur'an in their car on 30 March, 1998.
.

The Government does not designate religion on any passports or records of vital statistics; however, it requires an individual's religion to be stated on police reports, school registration forms, and applications for medical care.

Hivi hii ni halali? maana inaweza kutumika kama religious profiling au mnasemaje?



WAMAREKANI wanaendelea kusema hivi:






UTAMU ZAIDI uko hapa:

WACHUKIENI TUU HAWA WAAMERIKA LAKINI UKWELI WANAUJUA.....



Abuses of Religious Freedom


Kana kama hiyo haitoshi STATE DEPT WANAENDELEA KUSEMA HIVI....


In December 2001, police on Zanzibar arrested more than 20 leaders of the Muslim Answar Sunna group for conducting Eid el Fitr prayers on a day other than the one designated by the Government of Zanzibar.


Na kuhusus MWEMBECHAI STATE DEPT WANAMWAGA UPUPU KWA KUSEMA HIVI:


Sasa kama Ponda alikuwa charged for Muder mbona leo yuko free au ?

anyway STATE DEP waliendelea kusema hivi...another interesting part....:


State Dept walikuwa na haya ya kusema kuhusus BAKWATA:


The Muslim representative belongs to the BAKWATA; several urban Muslim leaders and a majority of urban Muslims believe that the BAKWATA is a government-imposed watchdog organization.

International Religious Freedom Report Home Page

ZAIDI INGIA HAPA:

http://www.state.gov/g/drl/rls/irf/2002/13859.htm
 
JF......be careful na watu wanaochezea mind za watu hapa......hawaitakii mema JF at the end of the day.............trust me........kuna watu wametumwa hapa.........!
 
JF......be careful na watu wanaochezea mind za watu hapa......hawaitakii mema JF at the end of the day.............trust me........kuna watu wametumwa hapa.........!

Well...hebu fafanua hapo juu mzeee

tukishamailiza hii tutaenda kuleta ripoti ya MAUAJI ya MERERANI na jinsi watawala walivyoreact hatuna haja ya kucelebrate positive tuuuu
 

Mkuu Son Of Alaska,

Heshima mbele, I mean kuna wakati ninakumbuka sana Zanzibar wananchi walikuwa na maisha bora kuliko sisi bara, na kulikuwa biashara nyingi sana za raba za mtoni, sabuni, na hata nguo kutoka kule kuja bara,

Binafsi nilishiriki sana kwenye usafirishaji wa raba za aina ya Tiger, sijui kama unazikumbuka, zilikuwa ni kutoka Japan lakini zilikuwepo Zenji tu kwenye duka la Uwanja wao mpya wa Mpira Tartan,

Ninakumbuka wananchi wa zenji walikuwa wakiishi kwenye ma-flat safi sana kama sio bure ilikuwa kwa bei ya almost bure, I mean kuna wakati wananchi wa kule walikuwa na maisha bora zaidi kulinganisha na wengi huku Bara, kwa hiyo kutokudaiwa kwao as a government ilikuwa ni sawia na maisha bora ya wananchi wao, ingawa baadaye sijui exactly what happened!
 
JF......be careful na watu wanaochezea mind za watu hapa......hawaitakii mema JF at the end of the day.............trust me........kuna watu wametumwa hapa.........!

Kwenye hilo mkuu, tutawaomba Mods na Invisible watusaidie, I mean what else can we do, hatuwezi kuacha kuelimishana kwa sababu ambazo ni nje ya uwezo wetu as members, wakuu leteni picha na habari za historia tunaendelea!
 
Binafsi nilishiriki sana kwenye usafirishaji wa raba za aina ya Tiger, sijui kama unazikumbuka, zilikuwa ni kutoka Japan lakini zilikuwepo Zenji tu kwenye duka la Uwanja wao mpya wa Mpira Tartan,
😀

...Spot on Mkuu, enzi hizo 'shoppingi' duka la michezo pale shangani! hizo raba ni brand ya ASICS


 
FMES,

..hizo raba mtoni, sabuni, na nguo, zilikuwa zinatengenezwa nchi gani?

..kilichotokea kwa wenzetu wa Zanzibar ni kutengeneza taifa la consumers.

..SMZ hawakujitahidi kuwekeza fedha zao ktk viwanda na uzalishaji.

..hata mapato ya Karafuu yalipatikana kutokana na karafuu ghafi, badala ya processed.

..watu milioni moja wanashindwa vipi kutumia soko la Watanganyika milioni 30 kwa manufaa yao?

..Wakenya hawana Muungano wowote ule na Tanganyika, lakini wametugeuza kuwa soko la bidhaa zao. kwa nini Wazanzibari washindwe wakati wanadai walikuwa na mapesa kibao ktk hazina yao?

..kuna nchi kibao zinalilia kuwa ktk position ya Zanzibar, yaani kuwa na majirani waliolala ambao unaweza kuwa-exploit Kiuchumi.
 


..hilo la kusema zanzibar ilifilisika kwa kutoa pesa kwenye vita kagera si kweli..kwani hata kama walitoa pesa hazingetosha kuendesha vita hata wiki moja..ila hatupuuzi mchango wao kwenye vita..lakini sio sababu ya kukauka hazina yao....

...Vita vya Kagera mpaka leo hii 2008 kuna wanaothubutu kulalamikia kutokana na kuporomoka kwa uchumi wetu, ingawa Donors countries thinks otherwise


...na kuhusu 'uchumi wa Zanzibar',...

 

Naheshimu kwa sababu kuna freedom of expression. Lakini huu ni ujinga, kama kuna mtu anaweza kupata data, anaweza kutukumbusha lawama na shutuma alizotoa Kitwana Kondo kwa Chuo Kikuu kuwa ali dico kwa sababu yeye ni muislamu lakini uzuri ni kuwa aliosahisha mitihani hawakujua jina lake na wala hawakuwa serikali na walikuwepo waislam, story kama hizi ni bollocks tu na media gibberish. Vizrui kama tukiendelea kufuatilia historia yetu na kuangalia imekuwaje viongozi wetu hao hao zamani walikuwa watu wa maana na sasa wamekuwa mafisadi, tuangalie ni kwa nini sasa hivi mzee Kingunge amekuwa hopeless kuliko zamani, kupitia kufuatilia historia yetu
 
1.
Mkuu mara ya mwisho nilipokuwa Singapore, au kama kwa lugha ya meli tulivyokuwa tuikiiita "Singapura", wao walikuwa exactly what unachosema yaani a consumer's state, hawakuwa na viwanda wala mashamba makubwa, lakini walikuwa wafanya biashara, to the point unaweza kwenda duka la nguo ukaulizia trekta watakuambia subiri na watakutafutia,

Japan walikuwa wan-dump all their rejects pale, kwa hiyo wale wakwawa taifa la biashara tu na consumers na wamefanikiwa sana, sasa labda tatizo kwa zenji limekuja kua utawala, otherwise ninaamini kuwa at one time waow alikuwa on the right track, kuliko sisi bara.

2.
There you go, labda kuwemo kwa Zenji kwenye muungano ndio hasa tatizo la wao kushindwa kutu-exploit kibiashara kama unavyotaka, au?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…