Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,540
...cha ajabu basi, wakati huo zilikuwa zinakuja ndege za mashirika makubwa kama PAN AM ya marekani, SABENA ya ubelgiji, AEROFLOT ya mrusi, ALITALIA ya muitaliani, LUFTHANSA ya mjerumani, hata AIRFRANCE ya mfaransa! ...Jumatatu mpaka jumapili kwa ratiba nilijua saa ngapi na siku gani ndege gani ingekuja pale Dar Airport, terminal 1
Ahhh sasa Jasusi mbona unaleta Utani mbele ya hadhara bwana? Unataka Mpaka Mwalimu Kichuguu naye ajue kuwa ni "mujukuu" wetu?
By the way alieandika ni Baba Mdogo!
Du! hii itakuwa zamani sana, mwaka gani huo?. Mimi British Airways ninayoikumbuka ni ile ilikuwa na kofia ya malkia, halafu ilikuwa Boing 747. Ilikuwa inafika saa 12 alfajiri, ikiwa inatua ilikuwa na madoido ya jinsi yake hivi tofauti na ndege nyingine. Ilikuwa raha kweli kiitazama, nakumbuka siku nilipopata bahati ya kuipanda ilikuwa kama nimeokota nyota ya jaha vile, kila mtu alinihusudu.
...ha ha ha... hillarious! 😀
Zamani undava/Utemi ilikuwa ndio desturi eeh!?... nakumbuka kipindi fulani madogo walisumbuliwa sana na yanki mmoja mitaa ya ilala/uwanja wa karume aliyekuwa anajiita eti Mtemi Sigasiga!
Mndava huyo kwanza alikuwa na tabia ya kuacha signature yale kutani kila anakopita mfano wa Graffiti, Sigasiga kapita hapa,... halafu madogo wakikutwa na raba mtoni lazima wamuachie,... 😀
Tabia ya ubabe zilikuja rithiwa mpaka mashuleni, 'Vita' baina ya shule za Tambaza na Kinondoni katika mechi za Mpira hususan pale Uwanja wa shule ya Muhimbili, enzi hizo kina Athumani China, Amasha, etc
mkuu heshima mbele kwa kumbukumbu kali.
ongezea stc/biashara jazz band
nakumbuka marijani rajabu (RIP) baada ya kutoka olympio primary ambako alikuwa nyanda/golkipa mzuri tuu na mpiga ngoma kubwa katika bendi ya shule
alikwenda bendi ijulikanayo kama stc jazz band na baada ya hapo ndipo akaanzisha safari trippers.
nawakumbuka pia familia ya akina kapinga (george, amato na abraham) ambao wote walikuwa katika timu ya waanzilishi wa bendi ya the barkeys.
kweli tumetoka mbali
Kuna Jamhuri Jazz ambao ndio chimbuko la Simba wa Nyika au Arusha Jazz, na Atomic Jazz. Nyimbo zao kama "Kipande cha Papa " = Jamhuri pamoja na "Joyce" = Atomic kwa kweli zilivuma sana miaka ile.
Ni kweli kabisa mkuu, Jamhuri Jazz ndio waliokuwa chanzo cha Simba Wanyika, hata wakulu George Peter na Wilson Peter, kina Luza mpiga sax, na kina Tom Malanda, walianzia Jamhuri na baadye walikuwa kuwa Simba Wa Nyika's big na Les Wanyika.
Sawa sawa.
Mkuu Mgirima,
Unajua binafsi nilikuwa ninamuona Dede kuwa ni very rough, unajua sometimes jamaa huachia midevu na huvaa rafu rafu sana, halafu ni mkorofi sana akilewa masanga, kwa hiyo sikua mpenzi sana wa nyimbo zake, nilikuwa ninazimia tu na wimbo wake alioutoa akiwa Bima Lee yaani ule wa "Samaki Baharini Huishi Vipi", halafu siku zote nilidhani kuwa Bitchuka, alikuwa akimu over promote mno as opposed na kipaji chake hasa, ingawa sio siri kwua jamaa alikuwa maarufu sana, au?
Asante sana mzee FMES kwa kutufahamisha mengi kuhusu huyu mwanamuziki mahiri tuliyewahi kuwa naye. Kuna mengi yaliyokuwa yanatokea Dar siyafahamu hasa kwa vile wakati huo mimi nilikuwa naishi huko Tabora, na nilikuwa nafika Dar kwa msimu tu kutumia treni inayosafiri siku mbili njiani usiku na mchana. Hata hivyo, naona ugumu sana kukubaliana nawe kuwa mtindo wa Koka Koka ulianza mwaka 1976, kwa vile mimi niliandika T-Shirt yangu neno Kokakoka mwaka 1975 nikiwa nalihusisha na Vijana Jazz. Inawezekana huo mtindo wa Kamata Sukuma ulitumika mwanzoni mwa mwaka 1974 na haukuvuma kabisa kwa vile mtindo wa kwanza kujulikana ulikuwa huu wa Koka Koka.
Turudi nyuma tena; kumbuka kuwa kati ya mwaka 1975 na 1976 Vijana Jazz walikuwa wanarekodi nyimbo zao kwa kutumia Label za Moto Moto na kama hii hapa.
Partial listing ya Catalogue ya Moto Moto inaoinyesha santuri zao kwa utaratibu ufuatao:
MOTO 7-907 : Sabina/Niliruka Ukuta - Vijana Jazz Band , 1975
MOTO 7-918 : Magdalina No 2/Miaka Mingi - Vijana Jazz Band , 1975
MOTO 7-922 : Koka Koka No 1/Ujirani Mwema - Vijana Jazz Band , 1975
MOTO 7-923 : Shangazi/Gwe Manetu Fii - Vijana Jazz Band, 1975
MOTO 7-928 : Pili Nihurumie/Zuhura Naondoka - Vijana Jazz Band, 1976
MOTO 7-930 : Unakufa Kiofisa/Wajue Vijana Jazz - Vijana Jazz Band, 1976
Unaona kuwa hata ule wimbo KokaKoka Namba 1 ulipigwa mwaka 1975, mwaka ambao wimbo wa Niliruka Ukuta ulipotolewa pia. Nina imani kuwa Zuhura Naondoka uliopigwa mwaka 1976 bado ulikuwa kwenye mtindo wa Koka Koka. Inawezekana nyimbo nyingine hazikuwekwa kwenye santuri, ila zilirekodiwa RTD tu. Unajua kuwa baada ya kuvunjika kwa EAC (1977,) kuna wakati mpaka wetu na Kenya ulikuwa umefungwa, na hivyo wanamuziki wengi wa Tanzania wakawa hawarekodi nyimbo zao huko Kenya tena; ndipo wakawa wanarekodia RTD kwa ajili ya kupiga redioni tu, wala hakukuwa na santuri tena. Nadhani hiyo ilipunguza sana mapato yao na hivyo kudororesha maendeleo ya Muziki kwa vile studio zote za kurekodi santuri zilikuwa Kenya.
Kwa wale ambao wanasikia jina la wimbo Niliruka Ukuta bila kuufahamu, nimefanikiwa kuupata online: Gonga hapa uusikilize na kuuangusha (download MP3) kwenye computer yako ukiependa.
Nadhani Simba wa Nyika ilikuwa jina la kutokea la Arusha Jazz, kwani baada ya Jamhuri Jazz kuvunjika, hawa 3 Peters ( George, Wilson and William)walihamia Arusha na kuunda hiyo Arusha Jazz. Jina la Simba wa Nyika nadhani origin yake ni ule wimbo wa Jamhuri Jazz wa "Mganga No 3" (kama sijakosea) ambao chorus yake ya instrumental ilitumika sana miaka ile kama kianzishio cha kipindi cha Jioni Njema cha RTD. Huo wimbo ulikuwa na sauti ya simba akinguruma.
Walipohamia Kenya ndipo walipoanza kutumia Les Wanyika.
Inaonekana miaka 20 ya Mzee Mwinyi na Mkapa ni kama vile historia ya Taifa letu ilisimama kidogo. Hakuna muziki wa maana uliopigwa wakati huo, hakuna mpira wa maana uliochezwa, hakuna Chuo KIkuu kilichojengwa mbali na kubadili majengo kuwa vyuo vikuu, hakuna kiwanda cha maana kilichojengwa.
Mkuu Kichuguu,
Hapa naowaona kwenye picha ni Tambwe Leya (Then Kocha wa Yanga toka Zaire), Gibbson Sembuli (RIP) (Then Nahodha wa Yanga), Joseph Mbwambo (RIP) aliyekuwa kiongozi wa Yanga, na Mzee Tabu Mangara Tabu (RIP) (Then Mwenyekiti wa Yanga),
Sikumbuki ulikuwa ni mwaka gani, lakini najua for a fact kuwa ilikuwa ni in the middle ya the 70s, ilikuwa ni kwenye uwanja wa ndege wa Dar, Yanga walikuwa wamerejea kutoka Zanzibar walikonyakua kombe la Afrika Mashariki na ya Kati kwa kuifunga Simba, magoli 2-1, yaliyofungwa na Sembuli na Sunday Manara, goil la Simba lilifungwa na Saad Ali kama sikosei.
Ubarikiwe mkuu!
Hii skando ya Taifa Star kucheza vifua wazi ilitokana na timu zote kuwa na jezi zenye rangi moja na Taifa Stars eti hawakuwa na jezi za ziada za rangi nyingine.
Inasemekana baada ya mechi hiyo, Julius "Kaizari" Nyerere alisusa kwenda mpirani!