Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha



.Zamani "kidooogo", mheshimiwa Mbowe alitumia helikopta kwenye kampeni ya uchaguzi 2005..kampeni ya aina hii ilikuwa haijapata tokea Bongo! ...2010 sijui itakuwaje
 
Last edited by a moderator:

Nikweli kabisa mkuu, huyu Zahiri alikuwa na vibao vingi sana vikali, hicho ulichokitaja ni Kristina namba moja, kuna Kristina namba mbili, halafu nafikiri unakumbuka "Kabwe", ziko namba moja na mbili, halafu kibao chake kingine "Twende Kijijini",

Zahiri aliweza pia kuandika jina kubwa sana la muziki hapa nchini, lakini baadye hali mbaya ya uchumi ikamfanya ahamie Nairobi, ambako kwa kweli sijawahi kusikia vibao vayke akiwa huko, lakini najua kuwa baadye alirejea bongo, na siku hizi anapiga solo, yaani peke yake kwenye hoteli moja kubwa hapa chini.
 
...kampeni ya aina hii ilikuwa haijapata tokea Bongo! ...2010 sijui itakuwaje

Mkuu Mchongoma,

Heshima mbele, mkuu kama hujali weka maelezo kidogo maana wengine tumebaki nje na hii helikopta, ni ya nani? Inatokea wapi? Inakwenda wapi? na hapo ipo wapi?
 

Kwi!!!!!!!!!!!! kwi!!!!!!!!!!!! kwi!!!!!!!!!!!!

Nadhani kuwa hii si kweli kwa sababu kuvuka kutoka Majita kwenda Singida ni lazima wapitie mbuza za wanyama ambazo zilikuwa zimetapaa kuanzia Mwibara hadi Serengeti. Wasingekula punda na kuacha kula nyama nyingine nzuri zaidi zilizokuwamo humo kwenye mbuga.

Halafu kwa nini walipata njaa? Je walishindwa kuvua samaki?
 
The Evolution Of Air Tanzania



The Original Air Tanzania



The Concubine Air Tanzania



The Frustrated Air Tanzania


 

Attachments

  • 2246451795_fb631eac00.jpg
    12.9 KB · Views: 704
  • Air_Tanzania_Boeing_Boeing_737-236.jpg
    14.5 KB · Views: 683
  • 2656258601_0020a032db.jpg
    10.1 KB · Views: 682
Hee jamani!, kuna mwaka Air Tanzania nayo iliwahi kwenda London sijui ilikuwa Heathrow au Gatwick!. Kufika huko ndege ikazuiliwa kuruka, ikawa kesi kurudi sijui ilikuwa mwaka gani ule!
 

Mwalimu Kichuguu,

Mbona unaleta "unafiki" na kusingiza mambo ya "ZiMpoku" na Samaki? Tangu lini umesikia tukifa njaa?😉

Hivi kuwaacheni kule porini jirani na Serengeti ndio mnakuwa na Kibri?

Ngoja turudi kuwakusanya mateka na kurudisha empire!
 

Hii nitamwachia Jasusi na Majita watoe jibu. Nani mwamba kati ya timu hizi: timu iliyokula punda na kuzamia Iramba ya Singida au timu iliyorudi na kuishi Iramba ya Majita karibu na wanyama wa mbugani; inachekesha kweli kweli. Mimi mpaka sasa hivi ni mzamiaji kwa hiyo naogopa kuweka jibu langu hapo: kwi!!!!!!!!! kwi!!!!!!!!! kwi!!!!!!!!!
 

Kafara.

Hii single nitaipata wapi? Ninaikumbuka kwa mbaali mno.
 

..wazee shabani dede ni mmanyema au muhaya wa kariakoo..nadhani mnanielewa ninaposema zamani kariakoo,kisutu, na gerezani kuna wahaya na wamanyema wa kuzaliwa...wakuu..
 
UDA- Usafiri Dar es Salaam

 

Attachments

  • UDA.jpg
    17.5 KB · Views: 317
Last edited:
Mkuu Mchongoma,

Heshima mbele, mkuu kama hujali weka maelezo kidogo maana wengine tumebaki nje na hii helikopta, ni ya nani? Inatokea wapi? Inakwenda wapi? na hapo ipo wapi?

...oooh, kumradhi mkuu. katika pekua pekua yangu ya historia ya nchi yetu hususan kuhusu vyama vya upinzani, nimeona kampeni ya mhesimiwa mbowe kwa kutumia helicopter 2005, ni moja ya mambo "yalopata kutokea" na kuwa kivutio sana zamani, japo si zamani hivyo.

Ule msemo wa "zidumu fikra za mwalimu na mwenyekiti wa CCM" uli create -void- kwenye historia ya mfumo wa vyama vingi vya siasa Tanzania, kwani historia ya vyama vya upinzani tangu 1967 mpaka 1995 ni karibia na -zero- na hii inachangia kwa kiwango kikubwa kwa ufinyu wa picha za historia hiyo.
 
Jemedari Mkuu FMES,

Masahihisho kidogo. Mtindo wa 'Sikinde Ngoma ya Ukae' (Sikinde Ngoma ya Nyumbani) asili yake ni uzaramoni kwa hiyo bila shaka wala wahka muasisi wa mtindo huo ni Maalim Gurumo kama alivyoasisi Ndekule. Sikinde na Ndekule zinaungana na ngoma zingine za kizaramo kama Tokomile, Gombesugu na Mnanda (Mchiriku).

Shukrani sana kwa kumbukumbu nzuri ya mpiganaji Abel Baltazar. Chidumule nakumbuka pia aliwahi kupigia Vijana Jazz akiwa na kina George Mpupua. Mpupua alipoacha kazi ya uimbaji alikuja kuwa Afisa Habari wa TAFICO. Sina hakika kama bado yuko hai.

Benno Villa naye kwa vipindi tofauti aliwahi kuwa na UDA Jazz (Bayankata) na Mwenge Jazz. Huko mwenge aliungana na kina Marehemu Msafiri Harubu, Kepteni Luza Elias John na wengine. Wimbo uliokuja kuwa maarufu pale Mwenge, "Kupatwa kwa Mwezi si Kiama" ni utunzi wa Benno ingawa aliyeimba wakati wa kurekodi alikuwa ni Msafiri kwa sababu Benno alikuwa kishaondoka.

Marehemu Francis Lubua aliyekuja kubadilisha dini na kuitwa Nasri Lubua alijiunga Sikinde akitokea bendi ya Tomatoma. Kule Tomatoma alikuwa na kina Marehemu Adam Bakari (Sauti ya Zege), Skassy Kasambula, Kasaloo Kianga na mmiliki wa bendi hiyo Tim Thomas (yuko hai?) Bendi hii ilizamia Botswana na taarifa nilizonazo huko walifilisiwa vyombo ikabidi kina Nasri warudi kwa kuungaunga. Wakati Nasri alijiunga na 'Nginde' Sauti ya Zege akaenda Pambamoto.

Kasaloo Kyanga habari za karibuni nilizonazo amejiunga na bendi ya Kalunde inayomilikiwa na Deo Mwanambilimbi. Kabla ya kujiunga na Kalunde alikuwa kule Mwanza na bendi ya Carnival pamoja na Benno. Kabla ya hapo yeye na mdogo wake walikimbilia Kenya baada ya kupewa misukosuko na Uhamiaji. Pacha wa Kasaloo, Kyanga Songa alishafariki siku za nyuma kule Nairobi na kuzikwa huko huko.

Tuko pamoja.
 

Ninaamini kuwa vyama vya upinzani vilikuwepo, hata wakati tunapata uhuru si TANU ilivishinda vyama vingine vya upinzani, au?

Wakuu wa Upinzani vipi historia huko mbona mnatuagusha jamani?
 
Joseph Batholomeo Mulenga amekwishatangulia kwenye njia ya haki. Mwanamuziki huyu mwenye asili ya Zambia baada ya kutoka Sikinde alikwenda Bima Lee. Kama unakumbuka kule Bima Lee walijulikana kama 'The Top Three' Mulenga (Solo), Gama (Rythm) na Mwanyiro (Bass). Bima Lee waliporomosha vibao kama Tugemaso, Neema (Nimesimama kwenye mnara wa Bismin. Barabara kubwa iendayo bandari ya salama, machozi yanimwagika....) na Makulata. Bima ya wakati huo ilikuwa imekamilika kweli kweli kwani safu ya waimbaji iliongozwa na Dede, Marehemu Jerry Nashon (Dudumizi), Roy Basshekanako (yu hai?) na Marehemu Othman Momba.

Baada ya kutoka Bima Lee, Mulenga alijiunga na Bendi ya MK Group. Kule alikuwa na kina Mbombo wa Mbomboka, Kasongo Mpinda Clayton na Marehemu Kalala Mbwembwe na kina Sid Morris (Barkeys?) Mafumu Bilal Bobenga. Wimbo maarufu pale kama unakumbuka ni 'Kibela Acha Chuki' Sina hakika ila nadhani huko ndiko umauti ulipomkuta. Kalala Mbembwe naye alifia Iringa na kuzikwa huko huko baada ya kuvunjika bendi ya Tancut alianzisha bendi yake (sikumbuki jina) ila moja ya nyimbo zake ni 'Lutandila' Kalala atakumbukwa pia kwa wimbo wake maarufu wa Fanta (Fanta unambie kama ninayo makosa mama... kumbuka tulivyopatana na wewe fanta... umesahau mema niliyokutendea mama .... Fanta wangu...)

Tuko pamoja.
 

Sawa sawa mkuu, ila nilifikiri "Ukae" ni neno la kusini linalotokana na neno moja la huko "Kukaye", najua for a fact kuwa Ndekule ni kizaramo, ila shukrani kwa masahihisho.

Shukrani sana kwa kumbukumbu nzuri ya mpiganaji Abel Baltazar. Chidumule nakumbuka pia aliwahi kupigia Vijana Jazz akiwa na kina George Mpupua. Mpupua alipoacha kazi ya uimbaji alikuja kuwa Afisa Habari wa TAFICO. Sina hakika kama bado yuko hai.

Cosmas Chidumule, mimi nilim-notice kwa mara ya kwanza yeye na Baltazari walipopiga wimbo unaioitwa "Birigita mtoto wa nyumbani", ambao ndio ulikuwa wimbo wa kwanza wa Dar International kabla hata Marijani Rajabu hajatoka Safari Trippers na kujiunga nao, baadaye nikawa mpenzi wake mkubwa sana kwa sababu ya Sikinde pale DDC siku za Jumapili mchana, maana alikuwa mtungaji mkubwa sana hasa kile kibao cha "Sasa naijibu telegram" halafu nyimbo zake zote zilkuwa na maana na zimetulia sana.

Alitoka Sikinde akaingia Matimila na Remmy, na lakini sasa hivi yupo hai na ni muimbaji wa nyimbo za dini na amekuwa mlokole wa kutupwa kama Remmy mwenyewe na Mzee Makassy, Cosmas siku hiziz anaimba kwaya ya Magomeni.


Sawa sawa tupo ukurasa mmoja.


Timmy Thomas, alikuwa ni former Msela yaani baharia, na pia alikuwa na kipaji cha kupiga solo gitaa aliposhuka jahazini akanunua vyombo vya muziki na kurudi navyo, akaanzisha bendi ya Orch. Toma Toma na mtindo wa "Tamba Tamba", akawachukua wa-Zaire mapacha Skassy na Kasaloo Kyanga, alitamba kidogo jijini wakati mmoja, lakini akaamua kwenda South Botswana na Zimbabwe, alifilisikia Zimbabwe na kunyang'anywa vyombo, sijawahi kumsikia tena since! lakini najua kuwa alikuwa ni mtoto wa Chang'ombe.


Sawa sawa mkuu saafi sana, je unaikumbuka bendi ya Sola TV ya Chang'ombe na kibao chao kimoja kikali sana enzi zile "Mama Leya"?

Otherwise, unaonekana mkulu una historia nzito za bendi zetu weka mkuu tule elimu ya bure.
 
Mkulu Shaaban Dede si mmanyema ni mhaya
Anachanganya damu! Mzazi wake mmoja ana asili ya Kigoma. Taaluma yake kabla hajawa mwanamuziki ni 'Fundi Gereji' alijifunzia kule Muleba.
 
Mkuu FMES,

Nakubaliana na wewe kabisa. 'Nginde' bado ni sehemu ya UwT. Ninapovinjari hapo Dar hupenda kwenda pale DDC Kariakoo (Old Traford) Ukiwa pale unachoweza kuona ni ustaarabu wa hali ya juu uliopo. Huwezi kukutana na mambo ya kutembea na 'mukaka' na kucheza shati likiwa mfuko wa nyuma wa suruali. Hapo utawakuta kina mama wengi ambao wamekuja bila hata mapatna wao. Ikitokea vurugu muziki huzimwa haraka sana na wababe hujitokeza na kutuliza ghasia hizo.
 
The Evolution Of Air Tanzania




The Original Air Tanzania



The Concubine Air Tanzania


The Frustrated Air Tanzania


i like this post and its comments. this is real evolution of Air Tanzania. can u predict what next?
 
Tukumbuke kidogo Nginde





Bitchuka

Dede
 

Attachments

  • ddc.bmp
    ddc.bmp
    461.9 KB · Views: 185
  • ddc2.bmp
    ddc2.bmp
    427.3 KB · Views: 163
  • ddc3.jpg
    27.5 KB · Views: 172
  • bitchuka.jpg
    5.5 KB · Views: 168
  • dede.jpg
    7.9 KB · Views: 167
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…