Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
mkuu unanikumbusha zahir ally na wimbo wake wa "christina (sina hakika kama ndio ilikuwa title ya wimbo). wimbo wenyewe chorus unamaneno yafuatayo;
"kitu mapenzi kilianza samani tokea enzi za mababu zetu, na hata wao
mapenzi waliyakuta tokea enzi za adamu na eva. yalianza zamani nasi
tuliyakutaa"
...kampeni ya aina hii ilikuwa haijapata tokea Bongo! ...2010 sijui itakuwaje
To this day in Majita there is a place called Iramba. Kitundu and Magembe are Bajita names.
Rev. Kishoka upo hapo?
There are more of us who came from Burundi than we realize.
Historia inasema kuwa,hapo zamani za kale,kuna watu walikuwa wanaishi Mara,as wajita wakurya nk.Baadae ikatokea njaa miongoni mwa wajita,baasi wajita hao wakapangana jinsi ya kwenda kutafuta chakula.likaanza kundi la kwanza la wajita hao wakachukua Punda zao wakazunguka huko na huko Wakarudi Mara.Hao ndo wajita wa sasa wa Majita.Likaenda kundi la pili la wajita,nao kama kawaida wakachukua punda wakazunguka huko na huko.Lakini hawakupata chakula na njaa ikawauma SANA.Hivyo hawakuwa na jinsi ikabidi wachinje Punda wakala.Baada ya kula punda hao wakaogopa kurudi Mara kwani wangeulizwa punda na wangeadhibiwa kwa kuwala punda ho.KWA HIYO IKABIDI WAENDELEE NA SAFARI HADI WAKAFIKA SINGIDA wakatia nanga.baada ya kufika Singida Wajita hao waliokuwa wametokea majita sehemu za Kwiramba wakaa sehemu moja na wakaiita IRAMBA nao wakajiita Wanyiramba.hiyo ndo maana kuna kufanana kwa majina kati ya Iramba,kwiramba,magembe,nk.
Haya wanyiramba nawapa changamoto rudini kwenu Majita hatutawadai punda wetu tena.Tulishawasamehe manake sasa tunajua ukali wa njaa.Hahahahaha
Kwi!!!!!!!!!!!! kwi!!!!!!!!!!!! kwi!!!!!!!!!!!!
Nadhani kuwa hii si kweli kwa sababu kuvuka kutoka Majita kwenda Singida ni lazima wapitie mbuza za wanyama ambazo zilikuwa zimetapaa kuanzia Mwibara hadi Serengeti. Wasingekula punda na kuacha kula nyama nyingine nzuri zaidi zilizokuwamo humo kwenye mbuga.
Halafu kwa nini walipata njaa? Je walishindwa kuvua samaki?
Mwalimu Kichuguu,
Mbona unaleta "unafiki" na kusingiza mambo ya "ZiMpoku" na Samaki? Tangu lini umesikia tukifa njaa?😉
Hivi kuwaacheni kule porini jirani na Serengeti ndio mnakuwa na Kibri?
Ngoja turudi kuwakusanya mateka na kurudisha empire!
jamaa si ndio alitoa ile singo yenye maneno
dada-kachote maji ernesti, enersti
frank- na nini?
dada- na mtungi, ernesti, ernesti, na mtungi, enesti,enesti
frank- una shimo
dada- kazibe enesti, enesti...
kibao hiki kilipewa tafsiri tata mtaani lol
."
GOTTEE
Unanikumbusha mbali sana kuhusu huyu shaaban dede
Mmanyema huyu pamoja na ukorofi wake mwingi maranyingi huwa hataki kuwa chini ya mtu ukubwa ana upenda na ni mwingi saaana wa mambo ya ndumba huyu jamaa
Napia niniulizia mpigasolo ambaye nilikuwa ninampenda sana joseph Mulenga ameishia wapi huyu mkulu?kama katika ile nyimbo ya nginde NALALA KWA TABUMIYE WALISEMAWATU LISEMWALO KAMA HALIPO LAJA
Mkuu Mchongoma,
Heshima mbele, mkuu kama hujali weka maelezo kidogo maana wengine tumebaki nje na hii helikopta, ni ya nani? Inatokea wapi? Inakwenda wapi? na hapo ipo wapi?
Jemedari Mkuu FMES,Mkuu Abel Baltazari, kama ninakumbuka vizuri,
Alianzia Msondo Afya, alipotoka yeye na Marijani Rajabu "Mwana-manyema", Chidumule, Beno, Chris Kazinduki, Gama, na wengineo walianzisha Dar International "Super Bomboka",
Marijani alikua na tabia ngumu sana kuelewana na wenziwe, ndipo Abel Baltazari, Cosmas Chidumule, King Enock michael (Msondo afya), na Hamis "Kumbakisa" wakaenda kuanzisha Mlimani Park, na jina Sikinde lililetwa na Chidumule kutoka Songea, unakumbuka ule wimbo "...usitumie pesa kama fimbo"
Baadaye naye Gurumo, Bitchuka nao wakaenda huko na ndio kwa mara ya kwanza wakaifanya Sikinde kuwa on the top, na later on Dede naye akaenda huko, sasa Bitchuka akarudi tena Msondo Afya, na kuungana kwa mara ya kwanza na Mkulu William Moshi TX (RIP).
ila uko sawa kabisa kuwa huyu alikuwa gwiji wa solo, na aliimba sauti ya kuongoza kwenye wimbo wa 'Magreti Mama" akiwa na Dar International.
Ule msemo wa "zidumu fikra za mwalimu na mwenyekiti wa CCM" uli create -void- kwenye historia ya mfumo wa vyama vingi vya siasa Tanzania, kwani historia ya vyama vya upinzani tangu 1967 mpaka 1995 ni karibia na -zero- na hii inachangia kwa kiwango kikubwa kwa ufinyu wa picha za historia hiyo.
Joseph Batholomeo Mulenga amekwishatangulia kwenye njia ya haki. Mwanamuziki huyu mwenye asili ya Zambia baada ya kutoka Sikinde alikwenda Bima Lee. Kama unakumbuka kule Bima Lee walijulikana kama 'The Top Three' Mulenga (Solo), Gama (Rythm) na Mwanyiro (Bass). Bima Lee waliporomosha vibao kama Tugemaso, Neema (Nimesimama kwenye mnara wa Bismin. Barabara kubwa iendayo bandari ya salama, machozi yanimwagika....) na Makulata. Bima ya wakati huo ilikuwa imekamilika kweli kweli kwani safu ya waimbaji iliongozwa na Dede, Marehemu Jerry Nashon (Dudumizi), Roy Basshekanako (yu hai?) na Marehemu Othman Momba.GOTTEE
Unanikumbusha mbali sana kuhusu huyu shaaban dede
Mmanyema huyu pamoja na ukorofi wake mwingi maranyingi huwa hataki kuwa chini ya mtu ukubwa ana upenda na ni mwingi saaana wa mambo ya ndumba huyu jamaa
Napia niniulizia mpigasolo ambaye nilikuwa ninampenda sana joseph Mulenga ameishia wapi huyu mkulu?kama katika ile nyimbo ya nginde NALALA KWA TABUMIYE WALISEMAWATU LISEMWALO KAMA HALIPO LAJA
Jemedari Mkuu FMES,
Masahihisho kidogo. Mtindo wa 'Sikinde Ngoma ya Ukae' (Sikinde Ngoma ya Nyumbani) asili yake ni uzaramoni kwa hiyo bila shaka wala wahka muasisi wa mtindo huo ni Maalim Gurumo kama alivyoasisi Ndekule. Sikinde na Ndekule zinaungana na ngoma zingine za kizaramo kama Tokomile, Gombesugu na Mnanda (Mchiriku).
Shukrani sana kwa kumbukumbu nzuri ya mpiganaji Abel Baltazar. Chidumule nakumbuka pia aliwahi kupigia Vijana Jazz akiwa na kina George Mpupua. Mpupua alipoacha kazi ya uimbaji alikuja kuwa Afisa Habari wa TAFICO. Sina hakika kama bado yuko hai.
Benno Villa naye kwa vipindi tofauti aliwahi kuwa na UDA Jazz (Bayankata) na Mwenge Jazz. Huko mwenge aliungana na kina Marehemu Msafiri Harubu, Kepteni Luza Elias John na wengine. Wimbo uliokuja kuwa maarufu pale Mwenge, "Kupatwa kwa Mwezi si Kiama" ni utunzi wa Benno ingawa aliyeimba wakati wa kurekodi alikuwa ni Msafiri kwa sababu Benno alikuwa kishaondoka.
Marehemu Francis Lubua aliyekuja kubadilisha dini na kuitwa Nasri Lubua alijiunga Sikinde akitokea bendi ya Tomatoma. Kule Tomatoma alikuwa na kina Marehemu Adam Bakari (Sauti ya Zege), Skassy Kasambula, Kasaloo Kianga na mmiliki wa bendi hiyo Tim Thomas (yuko hai?) Bendi hii ilizamia Botswana na taarifa nilizonazo huko walifilisiwa vyombo ikabidi kina Nasri warudi kwa kuungaunga. Wakati Nasri alijiunga na 'Nginde' Sauti ya Zege akaenda Pambamoto.
Kasaloo Kyanga habari za karibuni nilizonazo amejiunga na bendi ya Kalunde inayomilikiwa na Deo Mwanambilimbi. Kabla ya kujiunga na Kalunde alikuwa kule Mwanza na bendi ya Carnival pamoja na Benno. Kabla ya hapo yeye na mdogo wake walikimbilia Kenya baada ya kupewa misukosuko na Uhamiaji. Pacha wa Kasaloo, Kyanga Songa alishafariki siku za nyuma kule Nairobi na kuzikwa huko huko.
Tuko pamoja.
Anachanganya damu! Mzazi wake mmoja ana asili ya Kigoma. Taaluma yake kabla hajawa mwanamuziki ni 'Fundi Gereji' alijifunzia kule Muleba.Mkulu Shaaban Dede si mmanyema ni mhaya
Mkuu FMES,Ni kweli mkuu, hii bendi nayo ilikuwa ni ya zamani sana, na ilikuwemo pia kwenye list wakati mmoja, ikiongozwa na Juma Ubao, aliyekuwa akipiga solo na kuimba pia, kwa mtindo wa "Kumbakisa Imejipa", hawa nao walitoa vibao vingi sana safi, kama "Kasome Paule" na "Opresheni Maduka", aliziimba akishirikiana na Hamisi Kumbakisa, aliyehamia Sikinde, na Roy aliyekuwa kiongozi wa Bima Lee na kutoka baada ya Dede, kuingia Bima Lee yeye alirudi Biashara Jazz.
Kuhusu Sikinde na uwt, ninajua kuwa once uwt ni forever uwt kwa hiyo basi Sikinde bado ni uwt hiyo DDC ni kanyaboya, au?
The Evolution Of Air Tanzania
![]()
The Original Air Tanzania
![]()
The Concubine Air Tanzania
![]()
The Frustrated Air Tanzania