Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha

Ninaamini kuwa vyama vya upinzani vilikuwepo, hata wakati tunapata uhuru si TANU ilivishinda vyama vingine vya upinzani, au?

Wakuu wa Upinzani vipi historia huko mbona mnatuagusha jamani?

Miaka ya vyama vya upinzani ilikuwa kabla na baada ya uhuru kwa Tanganyika na Zanzibar... Hii ni kati ya miaka ya 1950-1960

Tanzania Bara
  • UTP -United Tanganyika Party
  • ANC-African National Congress
  • AMNUT- All Muslim National Unity of Tanganyika
  • TANU-Tanganyika African National Union

Huko Zenj Vyama vikumbwa vilikuwa
  • ZNP-Zanzibar Nationalist Party
  • ZPPP-Zanzibar and Pemba Peoples Party
  • ASP- Afro - Shirazi Party
 
Last edited:
Hivi nani anayejua mtu aliyeimba kwa mara ya kwanza kabisa na ambaye ni mtunzi wa wimbo wa MALAIKA? Maana watu wanakopi tu miaka nenda, miaka rudi sijui kama familia yake inapata chochote!
 
kumekuwa na claims na counterclaims kuhusu who really gave the world this song,but all in all,the buck stops with FADHILI WILLIAMS,who legally put the song under is name. could this song be the mother of all songs to ever come out of EAST AFRICA?
 
kumekuwa na claims na counterclaims kuhusu who really gave the world this song,but all in all,the buck stops with FADHILI WILLIAMS,who legally put the song under is name. could this song be the mother of all songs to ever come out of EAST AFRICA?

Huyo Fadhili Williams ni Mtanzania?
 
as far as i understand fadhili williams ni mkenya.inasemekana huu mwimbo ulipigwa tanzania mwanzo,nakumbuka hadi picha ya huyo so called malaika,akiwa mtu mzima nimashaiona katika magazeti,huyo malaika ni mwenyeji wa kilimanjaro,lakini kama hujuavyo wakenya ni mijitu sharp,kabla sisi hatujajua copyright ni nini,fadhili akatumia vacuum iliyoibuka,ya wimbo kupigwa na kila mtu,yeye aka u copyright.the rest is history
 
kUNA ZILE SEMI ZA ZAMANI AMBAZO NI ZA KISANII ZILICHANGAMSHA SANA LUGHA YETU:

1. DU KINAA - POA TU
2.KATA NGWALA- PIGA MTAMA
3.PEKOSI- SURUALI PANA CHINI
4.RAIZONI -VIATU VIREFU
5. NYAPU - Msichana
6.SHADA - Bangi
 
kumekuwa na claims na counterclaims kuhusu who really gave the world this song,but all in all,the buck stops with FADHILI WILLIAMS,who legally put the song under is name. could this song be the mother of all songs to ever come out of EAST AFRICA?

nakumbuka wakati wa bunge la bajeti. naibu waziri Bendera alilijibu swali la mtunzi wa wimbo huu, ngoja nikipata muda wa kupekenyua makabrasha nitawaletea lakini kama unaweza kupekuwa kwenye tovuti ya Bunge, nadhani ipo kwenye hansard, tatizo zikumbuki ilikuwa tarehe gani.
Lakini kimsingi wimbo ulitungwa na mtanzania mzaliwa wa mkoa wa kilimanjaro (kama sikosei). Huyu mkenya fadhili williams alifanikiwa kuurekodi na kujiwekea hati miliki ndio maana unajulikana kama wake
 
Katambuga

Kuna wakati hivi vilikuwa viatu vya kawaida kabisa kwa Watanzania. siku hiz watu huvaa kwa madoido tu

 

Attachments

  • Katambuga.JPG
    30.6 KB · Views: 470


Namuona hapa Choggy Sly (RIP) akiwa kazini enzi hizo huko Silversands:



Nadhani alikuwa akivinjari zaidi mitaa ya Rungwe Oceanic, siyo Rungwe Beach, au vipi mkuu FMES. Hivi Rungwe Oceanic iliishia wapi?
 

Attachments

  • ChoggySly.jpg
    31.2 KB · Views: 412
Inasikitisha kuona idadi ya vijana mashuhuri wa Kitanzania waliofariki hata kabla ya kufikia umri wa 40 au 50. What happened? Is it only AIDS that took such a toll on our youths or what? The late Marijani was a year behind me at Aga Khan. Ray Abdul was my classmate. Patrick Balisidya was a friend. And all these DJ's who came years later.
 
tancat almasi ya kasoloo na kyanga songa...ilikuwa ikinisuuza sana ...kweli hiizi raha jamani....kuna ule wimbo..wao..

...".safari sio kifo"

safari sio kifoooo.,mama watoto...
subiri nitarudiii mama watoto..
nikirudi mama nitakuletea zawadi..
..zawadi mama ,mama watotoo..
nikirudi mama ..pokea mikono miwili...

YELELE ooh mama ..yelele...

alfu inaendelea rap..yao..

eee kebba kebba kebaa..kebaaaa.

fimbo..fimbo..fimbo...logoda..logoda ...

mangalaaaa!!!!

mangala dance!!!![MSISAHAU KUNA SOLO KALI SANA LINAPIGWA KWENYE WIMBO HUU...

baada ya pacha kutoka walikuja kuungana na kina chunusi na kuunda bendi ya NGORONGORO HEROES BAND..ikaja kufa...

wazee MNAONAJE SERA YA VIWANDA YA MWALIMU.....KWELI TUTARUDI KULE KWELI...???MAANA ILIKUWA SERA YA KUHAKIKISHA KILA MKOA UNAKUWA NA VIWANDA ...ILI WATU WASIKIMBILIE MJINI..AU DAR ES SALAAM WOTE....DISTRIBUTION OF NATIONAL RESOURCES....

IDADI YA VIWANDA ALIVYOJENGA NYERERE NDANI YA MIAKA 20...KWANINI SIKU HIZI VIONGOZI WETU WANAOTAWALA MIAKA 10 WANASHINDWA KUJENGA HATA NUSU YAKE????
 
Mkuu kichuguu,



Hii kiatu imenikumbusha mbali sana. Hahaha, kuna ambazo zinaonekana kwa mbali nakumbuka mamangu alikuwa anapenda kutinga kwa sana!
 

Kula tano mkuu....... Ukiondoka mokasini na kishati cha kubana.....dah!! Longi mkulu...
 
Huyu Ike akatukatia umeme juzi ikabidi kuchemsha maji ya moto na kuweka kwenye ndoo kwenda kuoga. Nilipochukua lile bakuli na kuanzia kujimwagia nikajikuta nacheka na kusema "there nothing more Tanzanian than this".... Hata umeme uliporudi I just had to do it one more time, najiuliza hivi pamoja wale tunaokaa ughaibuni hasa katika nchi hizi za kimagharibi bado tunaweza kuswitch ule uswahili wetu on demand?

a. Kutengeneza kata na kuweka ndoo kichwani
b. Kubeba kuni
c. Kupulizia moto ili upike
d. Kuchinja kuku bila kusahau Bismillah na kuelekeza Kibla au kutafuta mtoto wa Kiislamu aje akuhalalishie?
e. Kutengeneza kamba ndefu halafu watoto wote wa kiume (sometimes na wakike) mnaingia na mmoja wenu kujifanya yeye dereva wa Uda!
f. Kuhakikisha unatoa kitanda cha "telemka nikukaze" jua likitoka ili kipigwe pigwe najua na kuua kunguni?
g. Kutegea tegea wachuuzi wa samaki wapite, kule Tanga kulikuwa na jamaa anapitaga na dagaa kwenye tenga la basikweli; leo utamuona Kwaminchi ukikatakata kona utakutana naya Chumbageni! anapiga kelele "aeeeeh daggaaaaaa"! No 1 800 number!
h. Kwa wale wa kijijini jinsi gani tunaswitch kutoka kwenye gari na kusubiri usafiri wa baskeli au wa mguu kwenda kuwaona wazazi. Na hakuna kitu cha kukumbushia kama wale tuliosafiri na mabasi yale ya "Kauru"! na hata malori ya Tumbaku!
i. Lakini kabla ya kuletewa haya makompyuta na makideo bwelele mambo yote yalikuwa "kijiweni" literally. Hakuna mahali watu walikuwa wanapigana fix kama kijiweni! Na always kuna yule jamaa mmoja ambaye asipotokea jioni hiyo kijiwe hakinogi!
j. Halafu yupo yule jamaa ambaye mtaa mzima mnamjua kuwa ni "bishoo"! Na huwezi kumsahau yule binti ambaye kila msela mtaani anamfukuzia halafu ndo mgumu kichizi!
k. Kule Mwanza kama kuna vitu vilikuwa vinasisimua ni kwenda ziwani kuoga; upande mmoja kina dada wanaoga kivyao na kwingine vijana tena mchana kweupe msiniulize kwanini? Nenda ushuhudie hasa mitaa ya watani zetu kule UK a.k.a Ukerewe na UZ a.ka Uzinza!
 
Mwakjj,
Somethings will never change. Ninaporudi nyumbani siku za kwanza huwa naona shida sana kuoga maji ya baridi. Lakini after a few days naenjoy sana tu. Pia umetambua kuwa nyama iliyopikwa kwenye jiko la mkaa ni tamu kuliko iliyopikiwa kwenye jiko la umeme?
 

l. Ongezea ya kule Unguja na Pemba, kwenda baharini kuogelea na kujisaidia haja kubwa. Kazi inakuwa ni kuogelea kuyakimbia yasikufuate.




---------------
 
Yaani huu uzi "thread" unanikumbusha kwa kunikumbusha. Kuna siku hadi machozi yanatoka mamsapu anauliza kulikoni; mbona ukiingiaga kwenye tovuti hiyo unakuwa so emotional? namwambiaga ni kukumbuka kuleee nilikotoka.
Mkuu MKJJ ahsante sana na dondoo zako hapo ni kweli.
Kutengeneza kamba ndefu halafu watoto wote wa kiume (sometimes na wakike) mnaingia na mmoja wenu kujifanya yeye dereva wa Uda!
mi ndo nilikuwa mwekaji wa hizi kamba hadi kuna wakati fulani maza akaja kuzitupa, nilimmaindi...
Kutegea tegea wachuuzi wa samaki wapite, kule Tanga kulikuwa na jamaa anapitaga na dagaa kwenye tenga la basikweli; leo utamuona Kwaminchi ukikatakata kona utakutana naya Chumbageni! anapiga kelele "aeeeeh daggaaaaaa"! No 1 800 number!
Hii nayo kwa saanaa tu na hata mchuuzi mwenyewe alijua target area zake; wapi wananunua na saa ngapi. Hakukuwa na telemaketaz wala nini; na biashara ilikuwa inakwenda....Lakini tu kukuweka sawa ukitokea kwa minchi sio straight Chumbageni lazima upitie kisosora kidogo maana ukila juu kwa juu ni lazima upitie barabara ya kapiko ambako hakuna wanunuzi...
Mie nafanyaga once in a blu moon. Kuoga kwa ndoo tena na kata hasaa. Kukuna nazi kwa mbuzi sio za makopo ya Walmart.
Yaani we acha tu nyumbani ni nyumbani tu.......
 
l. Ongezea ya kule Unguja na Pemba, kwenda baharini kuogelea na kujisaidia haja kubwa. Kazi inakuwa ni kuogelea kuyakimbia yasikufuate.




---------------

😀
Bara mpaka majuzi mito inatumika kwa mtindo huo... sasa kazi kwa yule aliyekuwa upande wa mto unapoelekea...
 
Last edited:
jasusi,umenikumbusha hii mutu ray abdul,hivi huyu alikuwa undercover cop au janja yake. i remember alikuwa friends na mtoto mmoja wa nyerere,hivyo ikulu alikuwa anaingia kama kwake,alaafu jamaa could talk,he had more then hundred names
 
kwenye picha ya choggy sly kulia kwake nadhani ni abdul shalamar,bingwa wa kucheza ROBOT,jamani ni ajabu na kweli but how come no one has mentioned ADDY SALLY,i believe he was allready in the game before all them Dejays
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…