Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 10,448
- 8,705
Ilikuwa ukivivaa halafu jua likakuwakia mchana inakuwa ni kasheshe.
Nadhani wengi mtakumbuka .....mambo ya raizoni, bugaluu na afro.....bila kusahau mambo ya breakdance ....
Afro
View attachment 2451
Raizoni
View attachment 2452
Bugaluu
View attachment 2453
Breakdance - from YouTube
[media]http://www.youtube.com/watch?v=UYFDYX4i2EY[/media]
Basi na wewe umekula chumvi kama mimi. Kwi!kwi!kwi!Nakumbuka suruali za mchinjo na viatu vya mkuki! Nakumbuka Twist na Salum Abdallah (R.I.P.) Nakumbuka mashati ya slimfit na dog collar!
harsui ya nani hiyo mkuu?
Hata akiwa hapa hapa nchini Zahir Ally baada ya kutoka Kimulimuli aliweza kujiunga na bendi kadhaa nchini na kuendelea kutoa vibao kadhaa vilivotokea kupendwa sana kama pale miaka kama minane ama kumi iliyopita aliposhiriki kuunda bendi mpya ya 'Mass Media le Dance' na kuimba kuimba kiba kikali cha 'Beatrice' akishirikiana na 'Mtoto wa Malaika' (RIP).
steve hebu imerge na hii thread
https://www.jamiiforums.com/entertainment-forum/8100-hawa-wako-wapi-sasa-15.html
Masahihisho kidogo, kumbe hata serikali haijui mtunzi wa wimbo huu. Majibu ya Bendera haya hapa:
Na. 160
Asili ya Wimbo Maarufu wa Malaika
MHE. PARMUKH SINGH HOOGAN aliuliza:-
Kwa kuwa, Wimbo maarufu wa ‘Malaika' asili yake ni Mkoa wa Kilimanjaro – Tanzania; na kwa kuwa, waimbaji wengi wa kigeni kama vile Bonny M, Mariam Makeba n.k, wamekuwa wakiimba wimbo huo:-
Je, nchi yetu inanufaika vipi na wimbo huo kutoka kwa waimbaji wageni?
NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI NA MICHEZO alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Parmukh Singh Hoogan, Mbunge wa Kikwajuni, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali yetu inanufaika kwa njia mbalimbali pale ambapo waimbaji wengi wakiwemo wa ndani na nje ya nchi wanapoimba wimbo wa Malaika na nyimbo nyingine nyingi zinazohusu nchi yetu ya Tanzania. Kwa kutumia mfano alioutoa Mheshimiwa Parmukh Singh Hoogan, ambapo waimbaji wa kigeni kama vile Bonny M, Mariam Makeba n.k ambao wamekuwa wakiimba wimbo maarufu wa Malaika, Serikali inanufaika sana kutokana na wimbo huo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa, wimbo huo unaitangaza nchi yetu duniani. Lakini pia kwa vile wimbo huo umeimbwa kwa lugha ya Kiswahili, hivyo basi wanaitangaza lugha yetu ya Kiswahili. Kwa namna nyingine, pindi wimbo huo unaposikika, wasikilizaji wanatambua kama kuna lugha ya Kiswahili na asili yake.
Aidha, wasikilizaji wa wimbo huo hushawishika kujifunza lugha ya Kiswahili. (Makofi)
MHE. PARMUKH SINGH HOOGAN: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na faida hizo alizozisema Mheshimiwa Naibu Waziri, lakini nina taarifa kuna nchi moja jirani inanufaika kifedha. Mheshimiwa Naibu Waziri anasema nini kuhusu hilo?
MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri majibu. Sasa nchi hiyo sijui ni nchi gani. Nafikiri tuendelee na swali lingine la nyongeza. Mheshimiwa Mbunge, kama unaijua nchi hiyo nitaomba umnong'oneze Mheshimiwa Naibu Waziri ili basi aende akafuatilie yatusaidie hayo mapato yaweze kuja katika nchi yetu ya Tanzania pia.
MHE. HAROUB SAID MASOUD: Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya majibu mazuri sana na ya kuridhisha ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nina swali moja la nyongeza.
Kwa kuwa, sisi wengine humu ndani Bungeni tulikuwa waimbaji ni vyema tukamjua huyo mtunzi wa wimbo huo na yeye mwenyewe anafaidika na nini huyo mtunzi? (Makofi)
MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, nafikiri Mheshimiwa Naibu Waziri amesikia swali hilo au kama anamfahamu hebu atwambie huyo mtunzi. Mheshimiwa Naibu Waziri majibu.
NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI NA MICHEZO:
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kwamba wimbo huo unaojulikana kwa jina la Malaika ulitungwa na Mtanzania ambaye alikuwa anamsifia mpenzi wake anayeitwa Malaika, na kwa bahati mbaya kwa utafiti wote na wataalam wote wamefanya mpaka sasa hivi jina la huyo aliyeutunga halijajulikana, lakini ni Mtanzania anayetoka Kilimanjaro. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini anafaidikaje? Kwa bahati mbaya kama walivyosema Mheshimiwa Parmukh Hoogani na Mheshimiwa Haroub Masoud, aliyefaidika na kupata hakimiliki na mirahaba ya wimbo huo ni mzee mmoja ambaye amefariki ni Mkenya anaitwa Fadhili Williams, yeye ndiye aliyekuwa anafaidika na wimbo huo kwa sababu yeye ndiye aliyeurekodi. Sasa Sheria za hakimiliki ni kwamba anayerekodi kwa Sheria za Kenya ndiye anayepata mirahaba. (Makofi)
MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, labda tumsikie Mheshimiwa Teddy Kasella-Bantu kwa sababu ni Mbunge wa siku nyingi anaweza akawa anamjua huyo mtunzi.
MHE. TEDDY L. KASELLA -BANTU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kukiri kwamba pamoja na kwamba ni Mbunge wa siku nyingi simfahamu.
(Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pamoja na majibu mazuri ya nyongeza naomba niulize swali moja la nyongeza dogo. Kwa kuwa, wimbo wa Malaika na nyimbo 10 nyingine huwa zinatakiwa ziendelee hivyo hivyo bila kubadilisha lafidhi au maneno na sasa vijana wa siku hizi wanauimba wimbo huo wanaubadilisha. Je, Serikali inasemaje kuhusu ubadilishwaji huo?
MWENYEKITI: Mheshimwia Teddy Kasella-Bantu swali lako kwa kweli kulijibu kwa haraka ni swali ngumu sana. Nitaomba uwasiliane na Mheshimiwa Naibu Waziri ili muweze kusaidiana.
Waheshimiwa Wabunge, tuendelee na swali linalofuata. Lakini leo kwa kweli ni challenge kwa wimbo huo na nadhani Wizara yetu ya Habari, Utamaduni na Michezo inatakiwa kufanya kazi ya ziada kwenye eneo hilo.
7. Mgogoro - WoWowo
8. Salama au macho? Tutakula au Fitina? - Maamboo?
9. Basi Haya/Basi Ok - Hamna noma!
1o. Tutayafiksi - Nitayashughulikia!
Tuendelee...!!
jamani naamini wengi wetu tumekaa vijiweni/maskani,ambavyo in one way or another vilishape destiny zetu.mimi ni mwana HARLEM,kijiwe shule ya msingi muhimbili,tulikuwa na football team vilevile,me i was only a cheerleader.ujana unasumbua kwa hiyo vitu kama wee ilikuwa kama kazi,nakumbuka tukielekea madebeni mbowe tulipitia MISSISSIPI(nyuma ya library)kwa mzee musa.Those were the days,unfortunately washikaji wengi,with time,they just fell off the rails
Umewahi kusikia Masai Barefoot Technolgy? Angalia MBT :: HISTORY! Mhandisi wa kiswiss anasema alichunguza wamasai wanavyotembea akagundua kuwa design ya kutembea kwao inaondoa maumivu ya mgongo! Ingawa yeye anadai aliona wanavyotembea peku peku lakini nina wasiwasi alikwiba design ya kata mbuga. Sasa hivi, hivi viatu vya MBT vinauzwa kwa bei mbaya sana! Anasema aliangalia wamasai wanavyotembea akagungua kuwa viatu tunavyovaa vyote feki. Jamaa anapeta!
Hya ngoja sisi wa Pango Disco la wakina Sunburst ( maarufu kwa wimbo wao wa ukuti ukuti)tukae pembeni!
jamani naamini wengi wetu tumekaa vijiweni/maskani,ambavyo in one way or another vilishape destiny zetu.mimi ni mwana HARLEM,kijiwe shule ya msingi muhimbili,tulikuwa na football team vilevile,me i was only a cheerleader.ujana unasumbua kwa hiyo vitu kama wee ilikuwa kama kazi,nakumbuka tukielekea madebeni mbowe tulipitia MISSISSIPI(nyuma ya library)kwa mzee musa.Those were the days,unfortunately washikaji wengi,with time,they just fell off the rails
unanikumbusha kuna wakati baadhi ya jamaa walikuwa wakialikwa
kila mnuso kwa sababu walitegemewa wangekuja na santuri
kali. hata ma-gate crushers walikuwa wanashika santuri mkononi
hivyo wanakaribishwa bila tatizo.
mkuu kijiwe cha harlem ndio kile kilikuwa kwenye njia ya kupandisha
muhimbili hospital (kati ya muhimbili primary na makaburi ya
tambaza)ambapo kuna vijana "marastafari" walikuwa na
kitu kama kigenge hivi?
ebwanaaaa eeehh! chini ya mkwaju mpaka alipokuja yule mwalimu 'mnoko' wa shule ya muhimbili, Mwl Ndossi ndipo ulipokatwa, kisa, Pius Makene alimpa kibano mpaka akaishia kuitafuta wrist watch yake ipo mavumbini!,.... duuuh, enzi hizo kuna yule mgiriki Brian, kijiwe cha kujifundishia magitaa ya kina kina Andy Swebe, kina Galinoma nk... safi sana!