Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha

Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha

Ilikuwa ukivivaa halafu jua likakuwakia mchana inakuwa ni kasheshe.

Umewahi kusikia Masai Barefoot Technolgy? Angalia MBT :: HISTORY! Mhandisi wa kiswiss anasema alichunguza wamasai wanavyotembea akagundua kuwa design ya kutembea kwao inaondoa maumivu ya mgongo! Ingawa yeye anadai aliona wanavyotembea peku peku lakini nina wasiwasi alikwiba design ya kata mbuga. Sasa hivi, hivi viatu vya MBT vinauzwa kwa bei mbaya sana! Anasema aliangalia wamasai wanavyotembea akagungua kuwa viatu tunavyovaa vyote feki. Jamaa anapeta!

Hya ngoja sisi wa Pango Disco la wakina Sunburst ( maarufu kwa wimbo wao wa ukuti ukuti)tukae pembeni!
 
Nadhani wengi mtakumbuka .....mambo ya raizoni, bugaluu na afro.....bila kusahau mambo ya breakdance ....

Afro
afro2.jpg

Raizoni
raizoni2.jpg

Bugaluu
green-suit-bugaloo.jpg

Breakdance - from YouTube

[media]http://www.youtube.com/watch?v=UYFDYX4i2EY[/media]
 
hayo makatambuga uchunguzi umebaini,yanatoa mionzi,ambayo in the long run,inaweza kusababisha upofu kwa mtumiaji
 
BRAZAMENI alipokuwa anakamua about a year ago......

Mtanisamehe lakini najua wengi wenu humu JF mlikuwa Joni visomi na najua pia kuwa ambao hawakusoma mlikuwa mabaharia,na of course wengi wenu mnatokea mikoani na Dar mekuja miaka 1- iliyopita... lakini vile vile nilitaka kuwafahamisha kuwa early 80's kulikuwepo hili kundi la KU na sie wengine tulikuwepo siku ile ya jumamosi walipokuja CINE CLUB kurekodi video yao ya MSELA

ku1.jpg

176069136.img.jpg

176069062.img.jpg



Masela hawa wako wapi sasa...!!

Kwa wale tuliokuwa tukifwatilia kwa karibu muziki huu wa kizazi kipya wakati unaanza kuchipua,tutaungana mkono kuwa vijana walitokea mbali kiana na bila shaka katika harakati zao za kuukuza muziki huu walikutana vizingiti vingi na vya kila aina,mfano naweza kumtolea rafiki yangu Robert ambaye ilifikia wakati wazazi wake wakawa wanaingia na Radio zao chumbani ilimradi tu kumnyima bwana mdogo haki zake za msingi tena za kikatiba za kusikiliza muziki aliokuwa akiuf*gilia eti kwa maelezo kuwa muziki huo ni wa kihuni na usiokuwa na maadili hata kidogo.

Hapa kushoto ni KU Crew,katikati ni Terry kutoka HBC na kulia ni Mr II.Enzi hizooooo

Lakini kadri miaka ilivyokuwa ikizidi kusonga na wasanii kuendelea kuwa wabishi na kuachia mipini mipya tena kwa hela ya ngama waliyokuwa wakiidunduliza kwa taaabu kubwa, huku wakiwa hawapati maslahi yoyote ya maana zaidi ya ujiko tu...hatimaye wasanii walianza kuongezeka taratibuu jambo lililokuwa likiwachanganya zaidi wazazi wengi waliohisi vijana wamechanganyikwa.

Left ni Saigon na katikati ni Dola Soul kutoka the Diplomatz,kulia kwao ni Mr Paul...enzi hizoooooo

Yote hayo yalichangiwa na wengi tu kuanzia waandishi,vituo vya radio, mapromoter na kadhalika.....Jambo kubwa la kujiuliza wengi wa waanzilishi wa vita hiyo kubwa ya kuupigania muziki huu hawajulikani walipo.

Na leo hii itakuwa si vibaya hata kidogo tukiweza kuwakumbuka kwa pamoja wachache tu ambao mchango wao hata kama ni mdogo lakini umeweza kuifikisha Bongo Flava hapa tulipo na kuweza kuufanya muziki huu uwe kioo cha muziki wa vijana kwa Afrika Mashariki na Kati.

Hapa kushoto ni Caz T kutoka (BANTU POUND GANGSTER),katikati ni Bonny Harmony kutoka(AFRO REIGN),na kulia ni Rashid Ziada (KR) kutoka GWM ambaye pia ni mwasisi wa kundi la Wanaumeela TMK.

Kati ya tutakao wakumbuka wengine wanaendelea na muziki na wengine hatuko nao duniani kwa sasa, wengine hatujui walipo na wanafanya nini! tunajua wengi wangependa kujua wako wapi maselaaaa?


JE UNAWAKUMBUKA MASELA HAWA ?

Saleh Jabir
Adili a.k.a. Nigga One (R.I.P)
Afro Reign
K. U Crew
Bantu Pound
4 Kreuz Flava
Hard Blasters
Weusi Wagumu Asilia3
Sos B (ameongezwa na tony-serena znz)
Rhymson (KU Crew)
E-Attack
Fresh X
Kool Mooccc
Columba Mwingira - mawingu Band
OJ - Mawingu Band
Sindila
De-Plow-Matz
II Proud
G.W.M.

WATANGAZAJI WA RADIO (RADIO 1)
Master t
Mike mhagama

MAPROMOTER
Kim Magomelo (Kim & the Boyz)

STUDIOS
Container la Master J
Don bosco Studios
Sound Crafters

Je unazikumbuka video hizi za kwanza kwanzaaaaaa ?
1.Oyaa Msela oyaaaaa (Mawingu Band)
2.Usiige mambo ya mjini (Hard Blasters)
3.Kukurukakara zako (Sos B)


KUMBI
Kilimanjaro pool side
FM Club (zamani Lang'ata Social Hall)
Silent Inn club (umeongezwa na Frank Suura)

attachment.php
 

Attachments

  • kwanza.jpg
    kwanza.jpg
    44.9 KB · Views: 260
wale wanawake waliokuwa wakifanya kazi hapa walikuwa wajinga sana walikuwa na mashine ya Credit Card mbovu watu wamewalia sana pesa hawa jamaa...ulikuwa unaweza kulipa holiday ya ZENJI na kadi yoyote ile bila wao kustukia kitu
attachment.php
 

Attachments

  • 332510550_f070efb9fe_b.jpg
    332510550_f070efb9fe_b.jpg
    72.9 KB · Views: 247
Hata akiwa hapa hapa nchini Zahir Ally baada ya kutoka Kimulimuli aliweza kujiunga na bendi kadhaa nchini na kuendelea kutoa vibao kadhaa vilivotokea kupendwa sana kama pale miaka kama minane ama kumi iliyopita aliposhiriki kuunda bendi mpya ya 'Mass Media le Dance' na kuimba kuimba kiba kikali cha 'Beatrice' akishirikiana na 'Mtoto wa Malaika' (RIP).

Sawa sawa mkuu, lakini alivipiga hivyo vibao baada ya kurudi toka Nairobi, kwa sababu hata kwenda alitoroka kwa muajiri wake JKT, alirudi mwanzoni mwa kati kati ya 90s, baada ya JKT kufa, maana bila hivyo angeenda moja kwa moja munga'nda, hivi vibao ni kweli ameshirki kuvipiga tena ule wa Cleopatra na mimi ninao mkuu, lakini ilikuwa ni baada ya kurudi, otherwise uko sawa na mengine yote na shukrani!
 
GAME THEORY,hiyo video ya MSELA ilirecordiwa early 80's sasa sisi watoto wa mjini tulikuwa wapi?au ni early 90's wakati sisi wengine tumeshaanza
 
Masahihisho kidogo, kumbe hata serikali haijui mtunzi wa wimbo huu. Majibu ya Bendera haya hapa:

Na. 160
Asili ya Wimbo Maarufu wa Malaika
MHE. PARMUKH SINGH HOOGAN aliuliza:-

Kwa kuwa, Wimbo maarufu wa ‘Malaika' asili yake ni Mkoa wa Kilimanjaro – Tanzania; na kwa kuwa, waimbaji wengi wa kigeni kama vile Bonny M, Mariam Makeba n.k, wamekuwa wakiimba wimbo huo:-

Je, nchi yetu inanufaika vipi na wimbo huo kutoka kwa waimbaji wageni?

NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI NA MICHEZO alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Parmukh Singh Hoogan, Mbunge wa Kikwajuni, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali yetu inanufaika kwa njia mbalimbali pale ambapo waimbaji wengi wakiwemo wa ndani na nje ya nchi wanapoimba wimbo wa Malaika na nyimbo nyingine nyingi zinazohusu nchi yetu ya Tanzania. Kwa kutumia mfano alioutoa Mheshimiwa Parmukh Singh Hoogan, ambapo waimbaji wa kigeni kama vile Bonny M, Mariam Makeba n.k ambao wamekuwa wakiimba wimbo maarufu wa Malaika, Serikali inanufaika sana kutokana na wimbo huo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa, wimbo huo unaitangaza nchi yetu duniani. Lakini pia kwa vile wimbo huo umeimbwa kwa lugha ya Kiswahili, hivyo basi wanaitangaza lugha yetu ya Kiswahili. Kwa namna nyingine, pindi wimbo huo unaposikika, wasikilizaji wanatambua kama kuna lugha ya Kiswahili na asili yake.

Aidha, wasikilizaji wa wimbo huo hushawishika kujifunza lugha ya Kiswahili. (Makofi)

MHE. PARMUKH SINGH HOOGAN: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na faida hizo alizozisema Mheshimiwa Naibu Waziri, lakini nina taarifa kuna nchi moja jirani inanufaika kifedha. Mheshimiwa Naibu Waziri anasema nini kuhusu hilo?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri majibu. Sasa nchi hiyo sijui ni nchi gani. Nafikiri tuendelee na swali lingine la nyongeza. Mheshimiwa Mbunge, kama unaijua nchi hiyo nitaomba umnong'oneze Mheshimiwa Naibu Waziri ili basi aende akafuatilie yatusaidie hayo mapato yaweze kuja katika nchi yetu ya Tanzania pia.

MHE. HAROUB SAID MASOUD: Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya majibu mazuri sana na ya kuridhisha ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nina swali moja la nyongeza.

Kwa kuwa, sisi wengine humu ndani Bungeni tulikuwa waimbaji ni vyema tukamjua huyo mtunzi wa wimbo huo na yeye mwenyewe anafaidika na nini huyo mtunzi? (Makofi)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, nafikiri Mheshimiwa Naibu Waziri amesikia swali hilo au kama anamfahamu hebu atwambie huyo mtunzi. Mheshimiwa Naibu Waziri majibu.

NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI NA MICHEZO:
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kwamba wimbo huo unaojulikana kwa jina la Malaika ulitungwa na Mtanzania ambaye alikuwa anamsifia mpenzi wake anayeitwa Malaika, na kwa bahati mbaya kwa utafiti wote na wataalam wote wamefanya mpaka sasa hivi jina la huyo aliyeutunga halijajulikana, lakini ni Mtanzania anayetoka Kilimanjaro. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini anafaidikaje? Kwa bahati mbaya kama walivyosema Mheshimiwa Parmukh Hoogani na Mheshimiwa Haroub Masoud, aliyefaidika na kupata hakimiliki na mirahaba ya wimbo huo ni mzee mmoja ambaye amefariki ni Mkenya anaitwa Fadhili Williams, yeye ndiye aliyekuwa anafaidika na wimbo huo kwa sababu yeye ndiye aliyeurekodi. Sasa Sheria za hakimiliki ni kwamba anayerekodi kwa Sheria za Kenya ndiye anayepata mirahaba. (Makofi)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, labda tumsikie Mheshimiwa Teddy Kasella-Bantu kwa sababu ni Mbunge wa siku nyingi anaweza akawa anamjua huyo mtunzi.

MHE. TEDDY L. KASELLA -BANTU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kukiri kwamba pamoja na kwamba ni Mbunge wa siku nyingi simfahamu.
(Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pamoja na majibu mazuri ya nyongeza naomba niulize swali moja la nyongeza dogo. Kwa kuwa, wimbo wa Malaika na nyimbo 10 nyingine huwa zinatakiwa ziendelee hivyo hivyo bila kubadilisha lafidhi au maneno na sasa vijana wa siku hizi wanauimba wimbo huo wanaubadilisha. Je, Serikali inasemaje kuhusu ubadilishwaji huo?

MWENYEKITI: Mheshimwia Teddy Kasella-Bantu swali lako kwa kweli kulijibu kwa haraka ni swali ngumu sana. Nitaomba uwasiliane na Mheshimiwa Naibu Waziri ili muweze kusaidiana.

Waheshimiwa Wabunge, tuendelee na swali linalofuata. Lakini leo kwa kweli ni challenge kwa wimbo huo na nadhani Wizara yetu ya Habari, Utamaduni na Michezo inatakiwa kufanya kazi ya ziada kwenye eneo hilo.

loh lahaula! naona waheshimiwa wamejichangaya hapa. nadhani ingebidi
waende copyright society of tanzania (cosota) wakapate majibu kuhusu hakimiliki.

kuhusu mtunzi, nakumbuka kuna kipindi mzee mmoja kutoka moshi alijitokeza gazetini (sikumbuki ni gazeti gani ila kati ya uhuru au mzalendo) na kudai yeye ndiye mtunzi wa wimbo huo na kwamba alikuwa anafahamiana na fadhili william. alidai kunasiku alimuimbia fadhili huo wimbo na fadhili akaunasa na mengine yaliyofuatia ni historia.
 
Last edited:
7. Mgogoro - WoWowo
8. Salama au macho? Tutakula au Fitina? - Maamboo?
9. Basi Haya/Basi Ok - Hamna noma!
1o. Tutayafiksi - Nitayashughulikia!

Tuendelee...!!

hapo kwenye "salama au macho? tutafika au fitina" kulikuwa na kiendelezo cha
"ndege itatua au kiwanja kimejaa topee" lol
 
nakumbuka kwenye miaka ya 75-76 kuna meli nadhani ya kijapani ilitia nanga bandarini halafu kwa nyuma ilikuwa imeandikwa "KISHTOBE". wasela wakatoka na msemo "kishtobe nibebee" na wadada wenye uani (wowowo) kubwa walikuwa wakikatiza sehemu sehemu utasikia watu wakisema "kishtobeee mwanangu!)
 
jamani naamini wengi wetu tumekaa vijiweni/maskani,ambavyo in one way or another vilishape destiny zetu.mimi ni mwana HARLEM,kijiwe shule ya msingi muhimbili,tulikuwa na football team vilevile,me i was only a cheerleader.ujana unasumbua kwa hiyo vitu kama wee ilikuwa kama kazi,nakumbuka tukielekea madebeni mbowe tulipitia MISSISSIPI(nyuma ya library)kwa mzee musa.Those were the days,unfortunately washikaji wengi,with time,they just fell off the rails

unanikumbusha kuna wakati baadhi ya jamaa walikuwa wakialikwa
kila mnuso kwa sababu walitegemewa wangekuja na santuri
kali. hata ma-gate crushers walikuwa wanashika santuri mkononi
hivyo wanakaribishwa bila tatizo.

mkuu kijiwe cha harlem ndio kile kilikuwa kwenye njia ya kupandisha
muhimbili hospital (kati ya muhimbili primary na makaburi ya
tambaza)ambapo kuna vijana "marastafari" walikuwa na
kitu kama kigenge hivi?
 
Umewahi kusikia Masai Barefoot Technolgy? Angalia MBT :: HISTORY! Mhandisi wa kiswiss anasema alichunguza wamasai wanavyotembea akagundua kuwa design ya kutembea kwao inaondoa maumivu ya mgongo! Ingawa yeye anadai aliona wanavyotembea peku peku lakini nina wasiwasi alikwiba design ya kata mbuga. Sasa hivi, hivi viatu vya MBT vinauzwa kwa bei mbaya sana! Anasema aliangalia wamasai wanavyotembea akagungua kuwa viatu tunavyovaa vyote feki. Jamaa anapeta!

Hya ngoja sisi wa Pango Disco la wakina Sunburst ( maarufu kwa wimbo wao wa ukuti ukuti)tukae pembeni!

unanikumbusha jamaa wa sunburst walikuwa na wimbo unasema
"sikitiko mpenzi, mola ataumbua
mapenzi jama yamenitoka hivi,
kukosa mwana kimpenzi cha roho,
sikutambua hayo yotee, dua njema mwenzangu n
nakuombea

kosa langu mwenyewe, sikulima shamba
ningelima shamba, mazao bora ningepata
ningelima shamba chakula bora ningepata
ooh kosa langu kubwa...

pia walikuwa na wimbo wanasema
"kipapa kipapapa kipapa kipa
kinyunyu kinyunyunyu kinyunyu kinyu"

aah acha tu.
 
jamani naamini wengi wetu tumekaa vijiweni/maskani,ambavyo in one way or another vilishape destiny zetu.mimi ni mwana HARLEM,kijiwe shule ya msingi muhimbili,tulikuwa na football team vilevile,me i was only a cheerleader.ujana unasumbua kwa hiyo vitu kama wee ilikuwa kama kazi,nakumbuka tukielekea madebeni mbowe tulipitia MISSISSIPI(nyuma ya library)kwa mzee musa.Those were the days,unfortunately washikaji wengi,with time,they just fell off the rails

...ebwanaaaa eeehh! chini ya mkwaju mpaka alipokuja yule mwalimu 'mnoko' wa shule ya muhimbili, Mwl Ndossi ndipo ulipokatwa, kisa, Pius Makene alimpa kibano mpaka akaishia kuitafuta wrist watch yake ipo mavumbini!,.... duuuh, enzi hizo kuna yule mgiriki Brian, kijiwe cha kujifundishia magitaa ya kina kina Andy Swebe, kina Galinoma nk... safi sana!

unanikumbusha kuna wakati baadhi ya jamaa walikuwa wakialikwa
kila mnuso kwa sababu walitegemewa wangekuja na santuri
kali. hata ma-gate crushers walikuwa wanashika santuri mkononi
hivyo wanakaribishwa bila tatizo.

mkuu kijiwe cha harlem ndio kile kilikuwa kwenye njia ya kupandisha
muhimbili hospital (kati ya muhimbili primary na makaburi ya
tambaza)ambapo kuna vijana "marastafari" walikuwa na
kitu kama kigenge hivi?

...hapana mkuu, makaburi ya Tambaza ni huku nyuma, barabara ya Maliki, kijiwe cha Harlem ni karibia na uwanja wa barafu, kati ya Muhimbili Primary na Tambaza Secondary, unapandishia juu unatokea mitaa ya Silver Oak, nk...

Hicho kijiwe unachosema wewe labda ni kile mbele ya Scout, ...yeah, kina "Jah Toto" na Vw Combi lao, ha ha ha...😀

Historia
Enzi hizo kuna mambo ya balozi wa nyumba kumi kila mtaa, balozi shurti awajue wageni wote wanaoingia mtaani/ hata kama ni wageni was iku mbili lazima ajulishwe! na bendera ilikuwa inapepea nyumbani kwake!
 
ebwanaaaa eeehh! chini ya mkwaju mpaka alipokuja yule mwalimu 'mnoko' wa shule ya muhimbili, Mwl Ndossi ndipo ulipokatwa, kisa, Pius Makene alimpa kibano mpaka akaishia kuitafuta wrist watch yake ipo mavumbini!,.... duuuh, enzi hizo kuna yule mgiriki Brian, kijiwe cha kujifundishia magitaa ya kina kina Andy Swebe, kina Galinoma nk... safi sana!

Duh! mkuu leo umenikumbusha washikaji lontime hawa, vipi mkuu nipenyezeee kwa PM akam una wamasiliano nao mpaka leo, maana Pius Makene "Mario Kempes" nilikula naye shule kule Kwiro Secondary, na Anisile Swebe "Bichwa" nilikula naye pimary, duh long time! Galinoma nakumbuka enzi zake pale NBC Posta ya zamani! bitozi sana!

Mkuu Ahsante Sana!
 
Wakubwa mimininaulizia baadhiya timu zetu za mitaani ambazo zilikuwa niwaka sana miaka hiyo napia zimetoa baadhiya wachezaji wazuri na taifa kwa ujumlamoja kwa moja niaelekea upande wa wilaya ya kinondoni wakati huo pale manzese kulikwa na timu kama vile SIFA utd Ambayo imetoa wachezaji wengi kama vile madaraka suleman,idd suleman kibode,hawa walikuwa simba kama sikosei pia abdallah waswa,hamis mbuzi ,hiitimu ilikuwa makaaziyake nipale tiptop [kwa alibay]au kwa yusuf mkimbizi
Pia kulikuwa timu za wababe kama vile faru hawa faru kwa hakika ilikuwa timu moja ya wahuni kiasi refarii lazima kwanza onyeshe kisu kwenye kiuno ndio awacheshe hawa jamaa sijui hii timu kama bado ipo
ninakumbuka sana enzi za chakacha la wakina faruku,
pia kuna mzee mmoja alikuwa maarufu sana ukanda wa kinondoni akiitwa mzee mwinyihija.
mwenye kujua chochote niwakuu mwageni katrika huu uwanja
 
Back
Top Bottom