Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha


nimekupata mkuu. baadhi ya washkaji wa harlem nawafahamu sana

andy swebe si ndo yule alijiunga na king kiki vijana wakawa wanamwita
"ambassador" yaani mwakilishi wa vijana wa "upanga" kwenye muziki wa dansi.
sijui sasa yuko wapi. ndugu yake alikuwa anaitwa mpeli au?
galinoma bado yupo us pamoja na akina onesmo kibira wanaendeleza libeneke lol
duh unajua naweza kuwa nakufahamu kwani mitaa ya upanga nilikuwa nakatiza sana

brian mgiriki alisoma salvatorian sio. nasikia kaka yake tony (rip) alitangulia mbele za haki. dah ngoja nisiseme mengi manake naona vi-flashback vinakuja kwa kasi tu.
 

haya mambo bongo yalikuwepo siku nyingi. niliwahi shuhudia faruku
akigombaniwa na wakware kwenye chakacha maeneo ya kijitonyama.
noma kweli.
 
...ndugu yake alikuwa anaitwa mpeli au?
galinoma bado yupo us pamoja na akina onesmo kibira wanaendeleza libeneke lol

...Swadakta, alikuwa anajiita Mpe-sly! LOL...


...kila jambo na wakati wake, Umri ulipoingia kila mmoja alichukua njia yake. Miaka mingi sana ishakatika sijasikia tena habari zao hawa waheshimiwa. Naamini kutawanyika kwa kina Makene/Tibenda family, pia kulichangiwa baada ya kufariki Profesa.
 
Naona itabidi tuanze kujitaja majina! Wengi inaelekea tulikuwa hatuchezi mbali!
 
mchongoma,brian yuko jeshi,ugiriki.pius makene yuko dar galinomas,inno yuko states,akina mpeli wako dar,inasikitisha that baadi ya watu hapo ni wateja,thats life anyway
 


...flash back 1964 kuadhimisha muungano, for some reasons, picha hii inanikumbusha mauaji ya JFK...


Muziki Asilia;



 
Last edited by a moderator:
Duh! yaani bongo enzi hizo tulishakuwa na magari ya namna hii, mbona ilikuwa mapema mno ndio maana tuko hapa tulipo nini? au tuliachiwa na wazungu tu?

Mkuu Mchongoma saafi sana, tupo wote hapo!
 
Duh! yaani bongo enzi hizo tulishakuwa na magari ya namna hii, mbona ilikuwa mapema mno ndio maana tuko hapa tulipo nini? au tuliachiwa na wazungu tu?

Mkuu Mchongoma saafi sana, tupo wote hapo!
FMES,
Hiyo gari ni 1963 Ford Galaxie. Tulipewa 2 zawadi ya uhuru na serikali ya Canada.
 
Kwenye muziki Asilia, kulikuwa na lile kundi dada la Sikinde, DDC Kibisa wakiwa na yule jamaa Nobert Chengula na mijoka yao. Mzee Mwinamila na sauti yake kali na Mzee Nyunyusa akipiga zile ngoma zake!

Ile intro ya taarifa ya habari hakuna tena mfano!
 
Kwa wale waliowahi kuishi Mwadui. Mnakumbuka timu ile ya soka ilivyokuwa ikizichachafya timu kubwa za Dar es Salaam? Baadhi ya wachezaji waliowahi kuvuma kwa nyakati tofauti ni:

Ibrahim Ismail, Iddi Mshangama, Bernad Madale, Mgongo, Mathias Salugole, Isinika, Joseph Mbelwa, Emmanuel Mwambete (RIP), Prosper Mboya, Chia Massonga, Elijah Kategile (RIP), Salu Sammy, James Ng'ong'a, David Mwakalebela, Edmund Mannongi, Uncle Shubet, Kamis Kamaka, Mathias Mataluma, Alfred Kategile, Yahaya Mwandambo, Michael Mngodo, Abdallah Shebe, Kessy Manangu, Justin Simfukwe, Willy Kiango, Zubeir Kaiwanga, na wemgine wengi...

Tujikumbushe baadhi ya picha za Mwadui.


 

Attachments

  • Mwadui1.jpg
    29.4 KB · Views: 264
  • mini minor.jpg
    51.7 KB · Views: 210
  • training school.jpg
    41.3 KB · Views: 216
  • williamson.jpg
    35.5 KB · Views: 325

Maganzo kimtindo, umenikumbusha ile mibuyu.
 
...ama kweli, 'Ujana ni moshi...!'



...Hassan Dalali enzi zake...



...(shoto) kwenye benchi la ufundi la 'mnyama mkali'!
 
mchongoma,ndipo kabisa,yaani hilo motorcade la nyerere na karume,ungeziba sura,mimi ningejua ni JFK akielekea kukutana na risasi ya lee harvey oswald
 
...ama kweli, 'Ujana ni moshi...!'


kwenye benchi la ufundi la 'mnyama mkali'![/SIZE][/COLOR]
Kulia katika picha hii ni Omar Gumbo, aliwahi kuichezea Simba miaka ya Sabini na baade kuja kuwa Meneja TBL Dodoma katika miaka ya themanini
 
Last edited:
this song just came to my mind..

"Oh Selina piga moyo konde Oh Selina
Oh Selina utafanikiwa, Oh Selina"..!
 
Ngoja nitumie TANO bora zangu vizuri hapa.



(1) Kwa wapenzi wa Muziki, je mnakifahamu kikosi hiki ni akina nani na walikuwa akifanya nini katika picha hii na sasa hivi wako wapi?

(2)Kwa waliokuwa wapenzi wa Vijana Jazz; mnaweza kusema hawa ni akina nani na kwenye picha hii walikuwa wakifanya nini na sasa hivi wako wapi?

(3) Kwa waliokuwa wafuasi wa Marquiz na Double "O," je mnafahamu huyu dada ni nani na alikuwa akifanya nini kwenye picha hii, na sasa hivi yuko wapi?
(4) Kwa waliokuwa wafuasi wa kandanda, je mnamfahamu huyu mchezaji mwenye sharafa ni nani na kwenye picha hii alikuwa akifanya nini na sasa hivi yuko wapi
?
(5) Kwa waliokuwa wafuasi wa muziki tena, na mnakifahamu kikosi hiki kilikuwa kinajulikanaje na leo hii wapigaji wake wako wapi?

Ili kupata majibu ya maswali yenu, nipeni mji.
 

Attachments

  • KidawazirinaNanaNjige.jpg
    68.6 KB · Views: 439
  • Tanzanites.jpg
    58.7 KB · Views: 205
  • Tabiamwanjelwa.jpg
    42.8 KB · Views: 446
  • TanzaniaAllStars.jpg
    64.8 KB · Views: 450
  • Muchacho.jpg
    29.3 KB · Views: 434

Mbona majibu umeyaweka hapo chini!
 
wow!!!!

kumbukumbu safi sana,...! naruhusiwa kutoa majibu kwa kuigilizia mwalimu?... nimekuja na mlungula wangu huu .hapa chini..😀


katika picha zote imenifurahisha hiyo ya Tanzania All stars, kina Chongo, Jabali,...
 
Ngoja nitumie TANO bora zangu vizuri hapa.



(1) Kwa wapenzi wa Muziki, je mnakifahamu kikosi hiki ni akina nani na walikuwa akifanya nini katika picha hii na sasa hivi wako wapi?
.

Mwaka 1987, kampuni ya Film Tanzania iliwaunganisha wapigaji mziki maarufu kutoa wimbo kwa ajili ya kurekodiwa na kampuni hiyo. Kikosi hicho kilijulikana kama Tanzania All Stars. Waliopo pichani
kutoka kulia ni Muhidin Maalim Gurumo (aliyekuwa JUWATA-Msondo), Max Bushoke (aliyekuwa DDC Mlimani Park-Sikinde), Marijani Rajab (Jabari- aliyekuwa (Dar International, Super Bomboka), Melisa na Zahir Ally (waliokuwa JKT- Kimulimuli), Fresh Jumbe (aliyekuwa Dar International, Super Bomboka), Nana Njige (aliyekuwa Vijana Jazz- Pambamoto Awamu ya Pili), Mabruki (aliyekuwa Mwenge Jazz, Panselepa) na Hamisi (aliyekuwa JKT, Kimbunga). Aliyeko nyuma kulia DJ Seydou.
 
jamani,mnakumbuka,ile soo ya muheshimiwa DIRIA kusachiwa airport eti kwa tuhuma ya kubeba mzigo(cocaine) nadhani ilikuwa british airways.hii mnaionaje,hii si dharau kwa nchi,airport yetu wenyewe,wakamleta BA manager toka kenya kumsachi,ilibidi diplomatic passport ikae pembeni na mtu mzima akapigwa sachi-hii habari sent shockwaves hapa nchini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…