Kafara
JF-Expert Member
- Feb 17, 2007
- 1,396
- 425
...ebwanaaaa eeehh! chini ya mkwaju mpaka alipokuja yule mwalimu 'mnoko' wa shule ya muhimbili, Mwl Ndossi ndipo ulipokatwa, kisa, Pius Makene alimpa kibano mpaka akaishia kuitafuta wrist watch yake ipo mavumbini!,.... duuuh, enzi hizo kuna yule mgiriki Brian, kijiwe cha kujifundishia magitaa ya kina kina Andy Swebe, kina Galinoma nk... safi sana!
...hapana mkuu, makaburi ya Tambaza ni huku nyuma, mfano wa barabara ya Maliki, kijiwe cha Harlem unapandishia juu unatokea mitaa ya Silver Oak, nk...
Hicho kijiwe unachosema wewe labda ni kile mbele ya Scout, ...yeah, kina "Jah Toto" na Vw Combi lao, ha ha ha...😀
Historia
Enzi hizo kuna mambo ya balozi wa nyumba kumi kila mtaa, balozi shurti awajue wageni wote wanaoingia mtaani/ hata kama ni wageni was iku mbili lazima ajulishwe! na bendera ilikuwa inapepea nyumbani kwake!
nimekupata mkuu. baadhi ya washkaji wa harlem nawafahamu sana
andy swebe si ndo yule alijiunga na king kiki vijana wakawa wanamwita
"ambassador" yaani mwakilishi wa vijana wa "upanga" kwenye muziki wa dansi.
sijui sasa yuko wapi. ndugu yake alikuwa anaitwa mpeli au?
galinoma bado yupo us pamoja na akina onesmo kibira wanaendeleza libeneke lol
duh unajua naweza kuwa nakufahamu kwani mitaa ya upanga nilikuwa nakatiza sana
brian mgiriki alisoma salvatorian sio. nasikia kaka yake tony (rip) alitangulia mbele za haki. dah ngoja nisiseme mengi manake naona vi-flashback vinakuja kwa kasi tu.