Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha


Nakumbuka wimbo aliotunga waliporudi toka Japan. Kila ninapokwenda Japan tunapoelekea kutua Narita airport huwa nauimba sana wimbo huu kimoyomoyo;

Sasa tunatoa shukurani
Kwa serikali yetu ya Tanzania
Kutupatia nafasi
Ya kwenda mpaka Japan...

Chorus

Maonyesho Japan yalifana sana
Mataifa yote yalifurahi sana
Banda la Tanzania limetia fora, oyeee

Maonyesho Japan yalifana sana
Likembe Mahoka na ngoma za Taifa
Wacheza midimu na wachezea nyoka
Mzee Morris na ngoma zake kumi, oyeee!

Maonyesho Japan yalifana sana
Bwana Mayagila na bendi ya polisi
Wana wa sanaa wa chuo kikuu Dar oyee!

Sayonara Osaka!
Sayonara Tokyo
 
Aaah Mbunge wa ukweli Kino -Bryson! si baadaye akaja hading'oka , kwa mujibu wa baba akili ziliwang'oka!
 
Njaa kitu kibaya sana. You can sell your soul to the devil. Dr. Faustus anyone?

Mkuu huyu jamaa si ana ile blog yake anayodai inamuingizia 10ml per month, sasa njaa inatokea wapi tena?
 
Enzi ya UDA ulikuwa hukai kituoni na mzembe anajulikana mapema.kweli ilikuwa TANZANIA ya babau wa Butiama.
 
HADING'OKA alikuja piga kampeni yake shuleni kwetu mwananyamala B tukakatiza masomo baada ya "aff time" na kupigiwa debe na wazee wa mji kwani walimchoka "mzungu" BRISON.
 
Nimeshangaa sana nilipopitia thread hii tena na kukuta kuwa picha nyingi sana tulizoweka wakati ule hazipo tena. Vipi mkuu Invisible, mbona mmetuangusha sisis tuliochimba habari wakati ule na kuweka picha za uhakika kusaidia ukali wa post zetu wakati huo?
 
Last edited by a moderator:
Cha kale kiheshimiwe kwani HUWEZI KUFIKA 3 BILA KUPITA 1 & 2....so R.I.P MAKAMANDA WOTE MLIOTANGULIA MBELE ZA HAKI.
 

What a great thinker. Perfect. Why I can't foresee Africa changing from a misery ridden continent to a prosperous one is until learned brothers and sisters turn around from their sheaths of cowardice and apathy, take the plunge and become leaders of Africa. Worst as it may be, African leadership is left in the hands of mediocre, puppet and blood-thirst individuals. These craps cannot think beyond past midnight, all they think is their huge bellies and their packs of children.

Thanks JF Rweyemamu
 
Hata Shaban Robert tumemsahau, wakati yeye naweza kumfananisha na William Shakespear kwa Waingereza
 
Mie naamini tuna watu wazuri katika hizo fani wenye uwezo kutatua matatizo mbali mbali yanayotuandama, tatizo ni wanasiasa kwani ndio wanaoamua vipaumbele katika mipango yetu. Kwa mfano, kama serikari ingeamua kuelekeza nguvu kwenye swala la umeme kwa dhati, wataalamu wetu wanaouwezo wa kulitatua kabisa tatizo hili.
 
Mimepitia huu Uzi toka mwanzo hadi mwisho kwa muda wa wiki nzima kiukweli ,nimejifunza mengi kuhusu uchumi,siasa,utamaduni, muziki na kila kitu kihusucho nchi yetu hongera sana mkuu FMES, Kichuguu, Son Of Alaska, na malegendary wote wa Uzi huu ambao sijawataja, kingine very interesting na special n kuwa wale waropokaji na wadini wachafuao hali ya Uzi wameogopa kuingia huu Uzi , kwani unaheshima zake

Mkuu FMSE tunaomba sasa tupate hicho kitabu kinachotungwa ili iwe kumbukumbu na kuwapa watoto wetu wajifunze historia yetu

Heshima kwenu wote,,,,
 

mpuuzi
 
serikali yetu ya ccm.

bajeti ya WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA ni Sh bilioni 81.87, kati ya fedha hizo Sh bilioni 41 sawa na asilimia 51 ya bajeti ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Sh bilioni 40 sawa na asilimia 49 ya bajeti kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.
tuwe pamoja, tujenge pamoja!
 
Kila kizazi na enzi zake, pamoja na kwamba sasa hivi tunasema tumepiga hatua lakini wazee wetu walikula bata hata kama tunawaona washamba kwa sasa lakini ukifanya tathimini utagundua component ya entertainment waliitendea haki na ndio maana haya maneno "STRESS" sijui "NIMEKWAZIKA" hayakuwepo, kila mtu alikuwa anapata burudani anayotaka kutokana na ela yake japokuwa burudani haikuwa anasa kivile kwa watu wachache yaani mtu wa soka atakwenda kwenye soka, band halikadharika ngoma, ngumi (za ridhaa na kulipwa), riadha mpaka kwaya ili mradi kila mtu ameburudika. Siku hizi tunajifanya tumepiga hatua but only few wana access / afford issue za entertaining na ukiwa mtu wa burudani sana unaonekana kama mpenda anasa na soon utapotea. (na ndio maana magonjwa ya moyo na msongo wa mawazo hautoki kwa kuwa kutwa ni kazi na migongano na migogoro na hakuna hata kujirusha kidogo)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…