Yaani huoni kama hizi picha ni nuksi tupu ,hata ukitazama kwa kina utaona haziendani na hii Jamii forum inabidi ulete tambala lile lililokuwa linatumika na zile senema za bure akina Omo na Fakcho ,si mnazikumbuka ,wakituletea filamu kwenye viwanja vya mpira.
hawa ndio waliokuwa wakihimiza siasa za ujamaa na kujitegemea ,hebu angalia Madini ya Shinyanga yalianza kuchimbwa lini ,ni wakati huo huo wa siasa zao.
Kama kukumbukwa basi tukumbusheni mengi na ya kukumbuka sio picha hizi ambazo sasa zinaelekea kurithishana makampuni . Vizazi vya hawa ndivyo hivi hivi vinavyofanya biashala Ikulu ,watu hawa na siasa zao ni walemavu wa kuendeleza wananchi walio wengi ,hawa ni watu wa kusemwa na kupingwa kila kukicha ,mambo ya kuwakumbuka wayapeleke kwenye Chama chao ambacho kilitangaza kushika hatamu za Dola ,hivi wamejimilikisha kila kitu kwa faida ya nani kama sio yao yenye maslahi binafsi ila sasa tunaona akina Butiku wameanza kukana na kukanwa hii ni dalili mbaya sana.
Mwananchi anaekumbuka watu hawa bila ya shaka yeyote akiyapima maisha yake leo hii ataona ukweli kuwa hawa mnaoonyesha mapicha yao ndio walioidumaza Tanzania.
Tanzania ilipata uhuru ikiwa bado Bikira ,tofauti na akina Zimbwambwe,na wengineo ,hawa wangekuwa na uelewa maana ya kugombea Uhuru leo hii tungekuwepo mbali na maisha ya kutafutana na mlo wa siku.
Kila kukicha wanasifiwa kuwa Tanzania ni kisiwa cha Amani ,kumbe amani yenyewe ni moto unaowaka kwenye majivu ,wameitafuna Tanzania miaka 44 sasa yameanza kubaki mashimo ,wakati hao mnaowatazama wamishakufa na walio hai wanakimbiza vijisenti wanahama nchi na wengine ndio hao wanaenda kufia Ulaya na hazina na mahesabu yake hayajulikani yamepotea potea vipi ,wanasema eti fedha na mahesabu yapo katika hali ya kutatanisha toka Balali yupo hapa mpaka amepata ugonjwa mpaka wengine wanasema hajakufa na wengine amekufa ,mwisho serikali ya hawa mnaoonyesha picha zao ,haijui wafanye nini ? Hao ni CCM na waliopo ni CCM mnawakumbuka kwa misingi ipi ya uongozi na ufundishaji upi wa Uongozi tunao uona leo hii ,mwizi kusafishwa tena bungeni ,kama si aibu ni kitu gani kwao ?
Halafu mnaleta mapicha ya maiti eti tukumbuke ? hivi mkisikia kulogwa ,jamani si ndio huku ? baada ya kuzungumza mambu ya maana na maisha haya ambayo yanayokwenda na kupanda kwa kasi ya Kikwete ,mnaleta picha sasa niwaulize hivi mnafaidika na kitu gani na picha hizo wakati mpo kwenye ziki za kimaisha ? Au ndio mnajiliwaza ? Sasa kujiliwaza mngetafuta angalau mapicha mazuri yanayoburudisha moyo lakini si picha za waliotuzamisha ,mpo ?
Upinzani hauwezi kwenda mbele kwa kutazama picha za watawala au Chama cha walioko madarakani au waliokufa.
Tuna msemo wa kiswahili usemao samaki akioza mmoja ndio wameoza wote.CCM wameoza wote waliokufa na hawa waliokuwepo hai ndio usiseme ni harufu mbaya tupu.