Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha

mambo yamebadilika sana mkuu
 
Wapi DJ Hakim Magomelo Kim and The Boyz???
 
Nilikuwa nagoogle topic fulani, nikalaletewa thread hii. Nikaikumbuka kuwa nilichangia hapa zaidi ya miaka kumi iliyopita, na kwa bahati mbaya picha nyingi zimepotea. Nitatafuta picha ambazo nilitumia kwenye posts zangu ili niziupdate. Nawaomba wote waliochangia kipindi hicho kama wanaweza kiupata picha walizotumia wasaidie kuifanya thread iwe active tena; kuna posts zilikuwa zina make sense tu zikihusishwa na picha zake ambazo sasa hivi hazipo. Najua hiyo itakuwa ni project ya muda mrefu ila nawaomba wanachama husika wafanye kila wawezalo kuipa uhai tena thread hii.
 
Field Marshall...
Nina picha za za kihistoria ambazo nami ningependa kuziweka hapa kama kumbukumbu ya Baba wa Taifa na wazalendo wenzake walipogania uhuru wa nchi yetu.

In Shaa Allah nitaziweka hapa naanza na na hii ya kwanza:

Kulia ni Bi. Tatu bint Mzee, Bi. Titi Mohamed na kulia ni Bi. Chiku bint Said Kisusa Julius Nyerere hawa akina mama ndiyo wanachama wa mwanzo kabisa katika TANU hapa wapo Uwanja wa Ndege Dar es Salaam wakimsindikiza Mwalimu Nyerere safari ya kwanza UNO Februari, 1955.
 
Field Marshall,
Naweka picha ya pili nikijaribu kufuata mtitiririko wa kuiunganisha picha ya kwanza na hii ya pili:


Kushoto ni Iddi Faiz Mafungo, Sheikh Mohamed Ramia, Julius Nyerere, Saadan Abdu Kandoro na Haruna Taratibu Dodoma Railway Station, 1955.


Kushoto ni Rashid Sisso, Robert Makanga, Zuberi Mtemvu, Iddi Faiz Mafungo, Julius Nyerere, John Rupia na Titi Mohamed safari ya kwanza ya Julius Nyerere UNO 1955

Huyu Iddi Faizi Mafungo alihudhuria mkutano kwa kwanza wa TANU Ukumbi wa Arnautoglo mwezi Agosti, 1955 na kadi yake ya TANU ni no. 25.

Pamoja na haya alikuwa Mweka Hazina wa kwanza wa TANU na pia Mweka Hazima wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika na yeye ndiye alikuwa mkusanyaji wa fedha za safari za Mwalimu Nyerere UNO.

Mwaka wa 1954 wakati TANU inaasisiwa Iddi Tosiri na ndugu yake Iddi Faiz Mafongo walikuwa na umri wa miaka 40 na zaidi kidogo na tayari walikuwa katika siasa za TAA na Al Jamiatul Islamiyya.

Ndugu hawa wawili ni kati ya wanachama wa mwanzo kabisa kujiunga na TANU. Iddi Tosiri kadi yake ya TANU ni no. 24 na Iddi Faizi kadi yake ni no. 25.

Iddi Tosiri alikuwa akiishi Mtaa wa Livingstone na Amani mwendo wa kama dakika 10 hivi kufika ofisi ya TANU New Street. Ndugu hawa wawili walikuwa na kaka yao mkubwa Sheikh Mohamed Ramia wa Bagamoyo, Khalifa wa Tariqa Qadiriyya.

Katika kuipa nguvu TANU na kumtambulisha Nyerere kwa watu maarufu, Iddi Tosiri na Iddi Faizi walimchukua Julius Nyerere hadi Bagamoyo kwenda kumtambulisha kwa kaka yao Sheikh Mohamed Ramia.

Sheikh Mohamed Ramia alikujakuwa rafiki mkubwa sana wa Nyerere wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika. Nimebahatika kuonyeshwa na mtoto wa Iddi Tosiri, Maulid ‘’Chubby’’ Tosiri picha alizoacha marehemu baba yake Mzee Tosiri zikumuonyesha yeye mwenyewe na Nyerere wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.

Nami kwa hisani ya familia hii naziweka hapa kama kumbukumbu ya mashujaa wa uhuru wa Tanganyika picha hizi tatu zilizofuatana:



Iddi Tosiri


Wakwanza kushoto mbele ni Iddi Tosiri, watatu ni Julius Nyerere akifuatiwa na Kaluta Amri Abeid. Mstari wa mwisho wapili kulia ni Rashid Sisso. Picha hii ilipigwa miaka ya mwishoni 1950 New Street mbele ya ofisi ya TAPA (Tanganyika African Parents Association)


Mkutano wa kwanza wa TANU Ghandhi Hall Dar es Salaam 1955 katika mkutano huu ulihudhuria ujumbe wa watu wawili kutoka Southern Province - Salum Mpunga na Ali Mnjale. Hawa walikuja na ujumbe maalum wa kutaka Nyerere afike Lindi kueleza madhumuni ya TANU kwani serikali na Kanisa walikuwa wanawatisha watu kujiunga na chama.


Tawi la TANU la Magomeni Mapipa alilofungua Ali Msham nyumbani kwake Mtaa wa Jaribu 1954 Ali Msham ni wa pili kushoto waliosimama na watatu kushoto waliokaa ni Bi. Titi Mohamed na pembeni yake ni mwanae Halima.


Ali Msham kulia wa kwanza siku alipomwalika Rais wa TANU Julius Nyerere kwenye tawi la TANU nyumbani kwake kumkabidhi samani alizomtengenezea kwenye kiwanda chake kwa ajili ya ofisi yake New Street 1955.


Tawi la TANU Magomeni Mapipa lilikuwa na nguvu sana kulia ni Sheikh Suleiman Takadiri Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU kushoto ni John Rupia ambae amemziba Julius Nyerere na huyo aliyeshika tama ni Zuberi Mtemvu Katibu wa TANU.

 
Field Marshall,
Hivi nyerere alikufanya nini?
Field Marshall,
Picha hiyo hapo chini ni Abdulwahid Kleist Sykes na mkewe Bi. Mwamvua bint Mrisho maarufu kwa jina la Mama Daisy.

Hawa ndiyo walimpokea Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam mwaka wa 1952 na mwaka wa 1955 baada ya Mwalimu kujiuzulu kazi ya ualimu waliishinae kwenye nyumba yao Mtaa wa Stanley na Sikukuu.

Picha hii ilipigwa Government House kwenye Garden Party ya Mr. na Mrs. Edward Francis Twining miaka ya 1950s.

 
Asante nimekumbuka history katika moja ya vitabu nilivyosoma

Kulia Abdulwahid Kleist Sykes (1924 - 1968) Hamza Kibwana Mwapachu (1913 - 1962)
Wazalendo hao wawili hapo juu wana historia ya kusisimua ukiisikia kwani hawa wawili ndiyo waliomleta Julius Nyerere katika ulingo wa siasa za TAA Dar es Salaam. Ukijua historia za wazalendo hawa utakuwa umefungua mlango mpya katika historia ya Mwalimu Nyerere, TANU na historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika.
 
Shida zsko na matatizo yako usiysfanye kuwa ya nchi nzima,baki nayo mwenyewe,wewe unaonekana ni lofa mpka kichwani kwako.
 
Shetani ktk ubora wako
 
Natafuta picha ya Mwalimu Nyerere ya 1983 akipokea tuzo ya Nansen aliyopata kutokana na msaada wake mkubwa kuhifadhi wakimbizi Tanzania. Mwenye nayo tafadhali naomba msaada.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…