Kweli, huyo wa kushoto kafanana sana na Mzee Pinda japo si yeye.Mkuu Kichuguu,
Hapo msaaada, najua kuna Mwalimu, Mkapa lakini huyu wa pembeni amefanana na Pinda ila sijui ni nani mkuu weka msaaada!
niko na hili toleo la TIME. Nimeipata EbayNasubiri Comments za NN(Joke)
Mar. 13, 1964
Nyerere akiwa na BEBERU
TAZARA
Asante sana.
Huyo aliyekunjiana na Mohammedi Alikuwa alikuwa anaitwa mwmabungu, nadhani alikuwa mkurugenzi wa idara ya michezo kwenye wizara ya utamaduni
Swala la tetesi kwel lipo nmeona kabisaaa umenena kweli .Mzee muhammed said Hongera kwa kuweka mambo ya historia bayana.
Watu wema na wenye nia safi watafurahia,
lakini wengi wenye nia ovu wanaochukia histori ya kweli,
wanachukia kuona wazee wetu hawa wenye Vubarakhashia kwa jinsi walivyojitolea kuutafuta uhuru wa nchi hii ,
Na hatimae wengi wao baada ya uhuru walitupwa nje ya siasa na hata kutajwa kwenye historia ya uhuru wa nchi hii.
Wengine kupewa bahshish ya viwanja kariakoo na magomeni.
lakini kwenye Serikali walitengwa na udini ukachukua mkondo wake.
Hadi leo Nafasi ya uwakilishi kwa watu wetu wa aina hii ya vibalaghashia imekuwa teteserikalini na kwenye taasisi za umma
Mwalimu nyerere wala hakuonana nae..aliwaambia ageuze aendelee na safari yake kwingine alikotumwa.Hiyo picha ya Michael Jackson na Rais Mwinyi imenikumbusha mie mwaka 1979 wakati Mohammed Ali alipokuja Tanzania kwa niaba ya serikali ya Marekani kutushawishi tususie michezo ya olimpiki ya mwaka 1980 iliyokuwa inafanyika Moscow. Pale uwanjani alikumbana na Mheshimiwa Mwambungu ambaye nadhani alikuwa mkurugenzi fulani kwenye wizara iliyokuwa inahusika na michezo, wakakunjiana mashati kama ionekanavyo kwenye picha mojawapo hapa.
View attachment 1181168
View attachment 1181170
Huyo aliyekunjiana na Mohammedi Alikuwa alikuwa anaitwa mwmabungu, nadhani alikuwa mkurugenzi wa idara ya michezo kwenye wizara ya utamaduni
Tuwalaumu wakoloni jana, Leo na hata kesho. Kiongozi mjanja anafikiria kuhusu nchi yake na watu wake walimuua. Hii ndiyo hali ya Africa yote Leo inafanana kiuchumi na kimaendeleo, hii haiko hivi kwa bahati mbaya. Wakoloni waliwakumbatia viongozi wezi nabwasiokuwa kizuizi kwa uporaji wa Mali za umma. Bila kupepesa macho wakoloni waliwapenda zaidi viongozi wakatoliki kuliko wa madhehebu mengine, labda baadae tuanzishe Uzi mpya kuhusu hili lakini ndugu zangu wakoloni hawakutoa Uhuru kwa nchi zetu kwa huruma au kuzidiwa nguvu bali walifanya vile kwakuwa walibuni mfumo mwingine Bora zaidi wa ukoloni kuliko ule wa Berlin wa kugawanga physical makoloni. Mfumo mpya unawafanya kututawala bila kulazimika kuumwa na mbu huku kwenye nchi za ukanda wa joto.Yaani huoni kama hizi picha ni nuksi tupu ,hata ukitazama kwa kina utaona haziendani na hii Jamii forum inabidi ulete tambala lile lililokuwa linatumika na zile senema za bure akina Omo na Fakcho ,si mnazikumbuka ,wakituletea filamu kwenye viwanja vya mpira.
hawa ndio waliokuwa wakihimiza siasa za ujamaa na kujitegemea ,hebu angalia Madini ya Shinyanga yalianza kuchimbwa lini ,ni wakati huo huo wa siasa zao.
Kama kukumbukwa basi tukumbusheni mengi na ya kukumbuka sio picha hizi ambazo sasa zinaelekea kurithishana makampuni . Vizazi vya hawa ndivyo hivi hivi vinavyofanya biashala Ikulu ,watu hawa na siasa zao ni walemavu wa kuendeleza wananchi walio wengi ,hawa ni watu wa kusemwa na kupingwa kila kukicha ,mambo ya kuwakumbuka wayapeleke kwenye Chama chao ambacho kilitangaza kushika hatamu za Dola ,hivi wamejimilikisha kila kitu kwa faida ya nani kama sio yao yenye maslahi binafsi ila sasa tunaona akina Butiku wameanza kukana na kukanwa hii ni dalili mbaya sana.
Mwananchi anaekumbuka watu hawa bila ya shaka yeyote akiyapima maisha yake leo hii ataona ukweli kuwa hawa mnaoonyesha mapicha yao ndio walioidumaza Tanzania.
Tanzania ilipata uhuru ikiwa bado Bikira ,tofauti na akina Zimbwambwe,na wengineo ,hawa wangekuwa na uelewa maana ya kugombea Uhuru leo hii tungekuwepo mbali na maisha ya kutafutana na mlo wa siku.
Kila kukicha wanasifiwa kuwa Tanzania ni kisiwa cha Amani ,kumbe amani yenyewe ni moto unaowaka kwenye majivu ,wameitafuna Tanzania miaka 44 sasa yameanza kubaki mashimo ,wakati hao mnaowatazama wamishakufa na walio hai wanakimbiza vijisenti wanahama nchi na wengine ndio hao wanaenda kufia Ulaya na hazina na mahesabu yake hayajulikani yamepotea potea vipi ,wanasema eti fedha na mahesabu yapo katika hali ya kutatanisha toka Balali yupo hapa mpaka amepata ugonjwa mpaka wengine wanasema hajakufa na wengine amekufa ,mwisho serikali ya hawa mnaoonyesha picha zao ,haijui wafanye nini ? Hao ni CCM na waliopo ni CCM mnawakumbuka kwa misingi ipi ya uongozi na ufundishaji upi wa Uongozi tunao uona leo hii ,mwizi kusafishwa tena bungeni ,kama si aibu ni kitu gani kwao ?
Halafu mnaleta mapicha ya maiti eti tukumbuke ? hivi mkisikia kulogwa ,jamani si ndio huku ? baada ya kuzungumza mambu ya maana na maisha haya ambayo yanayokwenda na kupanda kwa kasi ya Kikwete ,mnaleta picha sasa niwaulize hivi mnafaidika na kitu gani na picha hizo wakati mpo kwenye ziki za kimaisha ? Au ndio mnajiliwaza ? Sasa kujiliwaza mngetafuta angalau mapicha mazuri yanayoburudisha moyo lakini si picha za waliotuzamisha ,mpo ?
Upinzani hauwezi kwenda mbele kwa kutazama picha za watawala au Chama cha walioko madarakani au waliokufa.
Tuna msemo wa kiswahili usemao samaki akioza mmoja ndio wameoza wote.CCM wameoza wote waliokufa na hawa waliokuwepo hai ndio usiseme ni harufu mbaya tupu.
Hii labda ilikuwa 1973 au 1963. Dar haikuwa na magari dizaini hiyo 1983.
Kutembea kwake kuliugharimu umma kiasi gani?Nyingine ambayo huwa naiangalia sana ni pale Nyerere alipotembea kwa mguu kutoka Butiama hadi Mwanza ati akiwa anaunga mkono Azimio la Arusha. Nadhani kuwa haya yalikuwa ni matumizi mabaya kabisa ya mali za umma.