Tukumbushane Mila na Desturi za Kiafrika zilizopitwa na wakati

holoholo

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2023
Posts
1,859
Reaction score
2,986
Wakuu,
Mila na desturi ni mtindo wa maisha wa jamii waliojiwekea wanajamii kutoka kizazi kimoja hadi kingine.

Mila na desturi zinaweza kuwa ni mtindo wa maisha wa mwanadamu kama mavazi, chakula, heshima, malezi na vitu vingine

Wakuu, zipo mila na desturi ambazo kwa namna moja ama nyingine zinaweza kuwa zimepitwa na wakati.

Mila na desturi hizi zinaweza kuwa ni kandamizi kwa jinsia moja dhaifu na kuwa "favour" pendelea jinsia nyingine, jambo ambalo ni baya na la kupingwa linapokuja suala la usawa na haki za binadamu!

Wakuu, mfano wa mila na desturi hizi ni pamoja na FGM au ukeketaji, miiko ya vyakula, kuwapiga wanawake, ndoa za mitara, ndoa za utotoni nk

wakuu,tujadili kwa pamoja ni njia gani zinaweza kutumika kupunguza kama si kumaliza mila hizi kandamizi na zilizopitwa na wakati.

karibuni.
 
Activepeleka uzi huu ktk jukwaa la habari na hoja mchanganyiko.
 
Kitendo wanachofanyiwa wahdzabe kama sehemu ya kudumisha Mila na utamaduni wao siyo sahihi , hatuwezi kuwafanya ndugu zetu kivutio cha watalii.

Tuwakomboe kwenye ule utumwa ingawa wanajiona wapo sahihi.

Sidhani kama wanapata huduma hizi

-Maji safi na salama
-Matibabu bora
-Elimu

Na mahitaji mengine mengi ili tu wakae kwenye ramani ya Dunia
 
dah bado una utumwa wa fikra jikomboe
 
Kitendo wanachofanyiwa wahdzabe kama sehemu ya kudumisha Mila na utamaduni wao siyo sahihi , hatuwezi kuwafanya ndugu zetu kivutio cha watalii.

Tuwakomboe kwenye ule utumwa ingawa wanajiona wapo sahihi.

Sidhani kama wanapata huduma hizi

-Maji safi na salama
-Matibabu bora
-Elimu

Na mahitaji mengine mengi ili tu wakae kwenye ramani ya Dunia
wahadzabe hawatendewi haki kama jamii zingine,mfano,wamasai wanadumisha tamaduni zao kwa mavazi,vyakula,nk lakini wanapata zile huduma muhimu za jamiii kama maji,elimu,afya lakini kwa wahadzabe hilo halipo.
 
»»Kuoa wanawake wengi ni mila iliyopitwa na wakati, lakn kuolewa na mwanaume mwenzako{ushoga ni haki za binadamu eti?} Acheni mwenye uwezo wa kuoa wake zaidi ya mmoja aoe kuliko kujikita kwenye ushoga

»»unaweza kuniwekea hapa ndoa za utoton zinaanzia miaka ngapi halafu rejea sheria ya ndoa ya nchi yako.

KUHUSU FGM, huo ni wivu tu maana waliokeketwa hawajawahi kuzidiwa chochote na abhasaghane.

KIKUBWA TUNGEWEKEZA KWENYE KUPINGA USHOGA, USAGAJI, KULA MAVYAKULA YA KIZUNGU {TUKUZE TAMADUNI ZA KWETU TUACHANE NA UFALA WA KIMAGHARIBI}
 
True,wamasaai wapo njema kidogo,hata kielimu baadhi wapo vizuri
 
tufanye nini kama taifa tukomeshe suala hili Kiranga ?
Tuongeze elimu, tuongeze fursa za kiuchumi, tuongeze utamaduni wa kuhoji tamaduni zetu ili kuboresha maisha zaidi, tuongeze utamaduni wa kuishi na tamaduni za kutatua matatizo, si kuishi kwa mazoea tu.
 
»»Kuoa wanawake wengi ni mila iliyopitwa na wakati, lakn kuolewa na mwanaume mwenzako{ushoga ni haki za binadamu eti?} Acheni mwenye uwezo wa kuoa wake zaidi ya mmoja aoe kuliko kujikita kwenye ushoga

»»unaweza kuniwekea hapa ndoa za utoton zinaanzia miaka ngapi halafu rejea sheria ya ndoa ya nchi yako.

KUHUSU FGM, huo ni wivu tu maana waliokeketwa hawajawahi kuzidiwa chochote na abhasaghane.

KIKUBWA TUNGEWEKEZA KWENYE KUPINGA USHOGA, USAGAJI, KULA MAVYAKULA YA KIZUNGU {TUKUZE TAMADUNI ZA KWETU TUACHANE NA UFALA WA KIMAGHARIBI}
tamaduni kama hizi ulizozitaja ni mbaya zaidi kuliko za kwetu zilizopitwa na wakati,ila ueneaji wake ni wa kasi na nguvu mno kuliko hizo za kwetu, kiukweli, hili la ushoga,usagaji, ndoa za jinsia moja linahitajika jambo moja tu kufanya, ni apatikane rais shupavu mfano wa YOWERI K. MUSEVENI wa Uganda
 
Kama ulishasikia wakisema....Ngariba haogopi mkojo...😜
 
Waafrika tushatawaliwa kifikra hadfi mila zetu tunaziona zimepitwa na wakati..what a waste!
 
Tuongeze elimu, tuongeze fursa za kiuchumi, tuongeze utamaduni wa kuhoji tamaduni zetu ili kuboresha maisha zaidi, tuongeze utamaduni wa kuishi na tamaduni za kutatua matatizo, si kuishi kwa mazoea tu.
Ahsante mkuu, Ushimen anakusalimia sana.
 
»»Kuoa wanawake wengi ni mila iliyopitwa na wakati, lakn kuolewa na mwanaume mwenzako{ushoga ni haki za binadamu eti?} Acheni mwenye uwezo wa kuoa wake zaidi ya mmoja aoe kuliko kujikita kwenye ushoga

»»unaweza kuniwekea hapa ndoa za utoton zinaanzia miaka ngapi halafu rejea sheria ya ndoa ya nchi yako.

KUHUSU FGM, huo ni wivu tu maana waliokeketwa hawajawahi kuzidiwa chochote na abhasaghane.

KIKUBWA TUNGEWEKEZA KWENYE KUPINGA USHOGA, USAGAJI, KULA MAVYAKULA YA KIZUNGU {TUKUZE TAMADUNI ZA KWETU TUACHANE NA UFALA WA KIMAGHARIBI}
Hapo kwenye FGM nakupinga mpaka naingia kaburini huo ni ukatili wa hali ya juu yan umeanza vizuru ila kuja kusupport FGM nimekukataa mazima.
 
Back
Top Bottom