Tukumbushane riwaya za kusisimua

Tukumbushane riwaya za kusisimua

Jamani hizi riwaya za zamani nazitafuta sana pia

Dah..!Mkuu si peke yako,hata mimi nazihitaji sana riwaya hizi hasa za Elvis Musiba nazipenda sana ila sijui zinapatikana wapi,anayejua anijuze tafadhari..!
 
Tumgidie b.w.e.ge.
Pesa zako zinanuka.
Lazima ufe joramu.
Kamlete akibisha mlipue.
Sifi mara mbili.
Akuanzae mlipue.
Bado mmoja.
Malaika wa shetani.
Sanda ya jambazi.
Salamu toka kuzimu.
Tutarudi na roho zetu.
Kabwe makanika jitu kumbuka.
Usiku wa balaa.
Buriani.
Hofu.
Kikosi cha kisasi.
Kufa na kupona.
Operesheni sukuma namba nane.
 
Samahani kwa kuchelewa kuendelea kuleta uhondo. Niliamua kutafuta kazi za watunzi wachanga ambao wanakuja juu. Nimeanza na huyu anaitwa Ahmad Mniachi. Tafadhali rejea juu ili uweze kusoma miongoni mwa kazi zake ambazo anaandaa kitabu halafu tutamwangalia Juma Kidogo. Tuwape moyo UNDER GROUND.

ooh,kwenye underground nami nafagilia kazi yangu.
HEKAHEKA.
Pia english novel.
HOTSOUP.
 
Baadhi ya Riwaya kama kufa na kupona, Njama na Kikomo.

kiongozi nimeipenda sanaaaaa iyo riwaya yako ya MHANGA WA IKULU, sijui utaimalizia lini? napendekeza sehemu ya pili yaani PARTY TWO iitwe MAJERUHI WA IKULU.
 
Siri ya sifuri :Bwana Msa
Mpenzi 1 na mpenzi 2: Kajubi Mukajanga
Dogodogo wanitesaaa Niko ye mbajo
Hiba ya wivu
Nataka iwe siri ( au siri sirini )
Nyota ya Rehema
Kasri ya Mwinyi Fuad
Ushindi wa mahaba
Tutarudi na roho zetu
Kurwa na Doto
kikomo
kikosi cha kisasi
after 4.30 😀Avid Mailu
The flesh
unfit for human consumption
my dear bottle
Animal farm

Hapo kwenye red hiyo kitu ni hatari sana. Yaani unasoma halafu kijasho chembamba kinakutoka kisha unagundua unasoma kitabu na siyo muvi ya kweli. Hahaaaa!! Miss those dayz! Sterling: Willy Gamba, Kazi yake Ben R. Mtobwa
 
Hapo kwenye red hiyo kitu ni hatari sana. Yaani unasoma halafu kijasho chembamba kinakutoka kisha unagundua unasoma kitabu na siyo muvi ya kweli. Hahaaaa!! Miss those dayz! Sterling: Willy Gamba, Kazi yake Ben R. Mtobwa

Willy Gamba Siyo Muhusika mkuu katika Vitabu vya Ben R MTOBWA ,bali ni vya Alistablus Musiba ( Njama, Kikosi cha Kisasi, Kikomo na Hujuma)
 
mmenikumbusha mbali kipindi kile kilikuwa na waandishi wazuri kwa sasa ni beka mfaume na Tuwa ambao wanajitahidi ukiacha wengine ambao ni story za mapenzi kwa waandishi wa nje ni mario puzo alieandika godfather,sicilian,robert ludlum born identity,supreme na fredrick fosth day of the jackal na odesa file,sidney sheldon na master of the game and if tommorow comes,daniele steel na perfect strangel.susan isaac na almost in paradise.doctors na erich segal wako wengi ila hao wachache nawapa salute
 
mkuu 22nd katika maktaba yako unavyo vipi nije kuazima!!nilivipenda sana vitabu vya msiba!ila sijui nitavipata wapi,nilivisoma nikiwa shule ya msingi!sivikumbuki vizuri!!!
 
Last edited by a moderator:
Ngoswe😛enzi kitovu cha uzembe
Alfulela ulela
Dar es salaam usiku
Wagagagigikoko
machimbo ya mfalme sulleiman
 
Adili na nduguze -Riwaya ya kusisimua na kusikitisha mno
 
"BADO MMOJA", ambacho sterling wake ni Marcus Sayuki. Jamaa ilikuwa kila alipoua mtu alikuwa anaweka kikaratasi juu yake kilichoandikwa, Bado Mmoja. Duu, ni riwaya bomba kwelikweli na matukio yote yalitokea pale jijini Mwanza, hasa maeneo ya Nyakabungo S/M.

Sijui naweza pata wapi Kitabu hiki....
 
Sitoweza kukisimuli coz sikijuwi vizuri.
Nilitokea kuazimwa na demu tukiwa safarini.
Nilikisoma ktk kurasa zake za mwanzo tu na
kutokea kukikipenda sana.
Kiliandikwa kwa lugha ya kifaransa na kimetafsiria ktk lugha 18 (pengine zimeshaongezeka. Na kimechapishwa kwa mara tofauti. Kinaitwa BARUA NDEFU KAMA HII.
kiliandikwa na Mariama Ba ni kitabu kilichomchora sana mwanamke wa kiafrika na aina ya maisha yanamzunguka!
maskini jakilini!
nilimpenda sana Aisatu mkubwa!
 
"Usinijue" mwandishi nimemsahau,pia ni kitabu kinachovutia na kinatoa ONYO kwa wanaume wanaopenda kudandia MAPENZI
 
"Maajabu ya Mlima kolelo"
"Usiku wa balaa"
"Somo kaniponza"
bila kusahau "Ua jekundu"
 
Back
Top Bottom