Kipindi kile DSM haikuwa ajabu kusikia matukio matatu mpaka manne kwa wiki halafu yote ya hatari lazima damu imwagike,mimi huwa nashangaa mtu anaposema ujambazi umerejea leo 2022 unajiuliza huyu ana umri gani?ilikuwepo miaka mtu kutembea na 500K mfukoni unakuwa hatarini.
Nakumbuka siku ilianzwa kwa majibizano makali ya risasi pale Kariakoo mtaa wa Swahili na Mafia ambapo polisi waliondoka na point zote tatu hiyo ilikuwa mapema tu saa 8:35 asubuhi,mchana majira ya saa saba mtaa wa Livingston na Mkunguni ule muda wa kwenda msikitini jamaa wakaingia sonara moja ilikuwa kubwa sana wakati ule.
Wakauwa mlinzi mwarabu boss wakamvunja nyonga wakachukua vyao wakaondoka,huku mitaa ya Jangwani na Congo kwa wale wauza vipodozi likapigwa tukio kupishana kama dk 40 hivi alikuwaga bwashee kaambiwa akabidhi fuko la hela yeye macho yamemtoka jamaa wakaona anawachelewesha wakamchapa ya mbavu wakachukua fuko wakaondoka (huyu alipona)
Pale police Msimbazi siku hii pale counter askari walibaki wawili tu wote waliingia mtaani kipindi hiki RPC alikuwa Alfred Tibaigana nakumbuka kumuona ndani ya defender pale mtaa wa Msimbazi akiongoza kikosi.
Funga kazi ni hiyo ya Ubungo jamaa waliuwa stuff wa Nmb na askari,attacker wao alikuwa kijeba hivi amejazia amevaa kawoshi na bukta ana kipisi anamimina njugu kama ana-act movie halafu mweusii kichwani ana kipara kinang’aa!
Yupo jamaa yangu aling'ang'aniwa baada ya kuonekana pikipiki iliyoshiriki lile tukio imeingia nchini kwa jina lake alikaa jela miaka nane na matukio mengi kipindi kile wapigaji walikuwa wanashirikishwa na wabongo refer tukio la kupigwa bomu kwa ATM machine pale Temeke hospital jamaa walivyofanyiwa ambush na askari Chang'ombe waliuwawa sikumbuki idadi but mmoja wao alikuwa na id ya Rwanda.