Tukumbushane tuliowapokea mashujaa wa vita vya Kagera

Tukumbushane tuliowapokea mashujaa wa vita vya Kagera

Alienda baba yangu huko, huwa anatupa story ilikuwa inapiga mizinga ya maadui mpaka baadhi ya wajeda wa kibongo wanalia kama watoto....

Akagusia wajeda hao walikuwa haswa makabila ya.........

Sitaki bifu wazeee huwa nacheka sana
 
Kuna mzee alipigana hiyo vita tunaishi naye huku hali yake ya maisha daaah na watoto wanamuita Sungura.
Bado wapo hai, japo wengi wao hatunao tena. ila JWTZ katika kumbukumbu za siku hii ya mashujaa ingefanya mpango wa kuwatambua kila wilaya nchi nzima angalau wapewe nishani ya heshima lakini siku za kumbukizi za siku ya mashujaa Basi wawe wanakutanishwa kwenye wilaya zao kwa pamoja, itawapa faraja Sana Hawa wazee wetu mashujaa.
 
alienda baba yangu huko hua anatupa story ilkuwa inapiga mizinga ya maadui mpka baadhi ya wajeda wa kibongo wanalia kama watoto....

akagusia wajeda hao walikuwa haswa makabila ya.........


sitaki bifu wazeee huwa nacheka sana
[emoji23][emoji23][emoji23],hasa makabila ya wasukuma,wanyakyusa,wangoni
 
Sikumbuki mwaka vizuri Ila nilikuwa darasa la 4 Kati ya 78 au 79. Ilitangazwa kuwa Vita imeisha na MASHUJAA wetu wanarudi nyumbani.

Tulienda kuwapungia mkono stesheni wakati walipopita na treni nakumbuka tuliimba nyimbo za kizalendo za kumsifu Baba wa Taifa hili na kumkashifu Dikteta Idd Amini Dada. Ulikuwa ni uzalendo wa kwenye damu kabisa.

Tukio moja ambalo sitalisahau kuna Shujaa ( Mwanajeshi) alituona tuko kikundi watoto wa kike akatuuliza ' Nani mchumba wangu' wote tukajibu Mimi, Mimi akatupa biskuti. Biskuti zao zilikuwa za chumvi. Tulifurahi Sana maana tulikuwa tunaenda kishule hata watu binafsi walikuwa wanakuja.

Uzalendo huu natamani ungekuwepo leo. Karibuni mliobahatika kuwaenzi MASHUJAA WA Taifa hili.
Hujatuambia uliolewa na miongoni mwa wale mashujaa? au ulizingua
 
Nilikuwa kortini nijitetee kama kuna umuhimu nije kuwa mtoto wa nne
Nilishinda kesi
 
Mashujaa wengi walirudi na gridi ya Taifa toka UGANDA aiseee. Baada ya vita babu yangu na wazee wengine walikwenda kufundisha huko. Baba wa shemeji yangu ndo alikuwa mkuu wa kitengo cha ulinzi idara moja muhimu huko Uganda, alinipa michapo jinsi askari wa Jwtz walivyozipiga kachabari papuchi za banyankole kwa sana. Ananiambia Uganda kuna wanawake wazuri ila sio wale wa kabila la obote la Bachori hao walikosa soko.
 
bado wapo hai,japo wengi wao hatunao tena.ila jwtz katka kumbukumbu za siku hii ya mashujaa,ingefanya mpango wa kuwatambua kila wilaya nch zima,angalau wapewe nishani ya heshima,lakini siku za kumbukiz za siku ya mashujaa Basi wawe wanakutanishwa kwenye wilaya zao kwa pamoja,itawapa faraja Sana Hawa wazee wetu mashujaa.
Ni kweli mkuu watakuwa wamethaminiwa wao na mchango wao.
 
Back
Top Bottom