Aiseee nakumbuka mshua alikuwa zaidi ya mkoloni, nina dogo langu lilikuwa linapenda kujisaidia kwenye uzio kisa choo kipo mbali, siku ya siku mzee akamfuma alikula stick za kufa mtu na akamlazimisha kula mavi yake toka siku hiyo aliona choo kipo karibu ata kama ni night.
Mimi mwenyewe alileta stand mpya ya tv hizi za kichina sasa muda asiokuwepo uwa tunatoa tv tukalia juu mwingine anakusuma inakuwa kama starehe fulani hivi kwa ilikuwa na maraisi, sasa mwisho wa siku. nikiwa juu naendeshwa huku narukaruka ikavunjika, mzee aliporudi kauliza kila mtu kimya, akatuita chumbani alizungusha waya nne nne kwa kila mtu wenzangu uvumilivu ukawashinda wakanitaja, aiseee nilipigwa sijapata ona hadi leo alama ipo. Baada ya kipigo ikawa kila ikifika kipindi cha taarifa ananiita nashikilia tv kichwani mpaka amalize kuangalia taarifa ndio natua, it takes almost 3months ndio akaleta stand nyingine