Tukumbushane ukoloni uliowahi fanyiwa na wazee wako

Tukumbushane ukoloni uliowahi fanyiwa na wazee wako

Nakumbuka tukiwa wadogo nilivunja remote ya tv ila mama alikuwa kasafiri. Baaada kurudi kuuliza nani kaavunja akambiwa mimi basi mdogo wangu akaambiwa akaavunje fimbo akaleta fimbo kubwa kweli. Basi nikaitwa wacha nipewe fimbo na mama halafu huku naruka kichura mpaka kwenye tv.Dogo baada yakuona napewa fimbo siakacheka mama akesema mjinga wewe yani baadala umuombe msamaha ndugu yako unmcheka njoo na ww nkuchape dogo akakimbia wee nkaambiwa mlete hapa laaa sivyo fimbo zake nakuchapa wewe. Nilikimbiza nikiwa na machungu ya kuleta fimbo kumbwa nilimshika nikamburuza zaidi ya mwanafunzi wa mbeya basi wote tukaanza chapwa na kuruka vichura na mdogo wangu baadaye akatuambia kaogeni kurudi tukanunuliwa soda. RIP mama ila alinifunza kutunza na kuheshumu vitu kiwe changu au cha mtu mwngine mpaka Leo.
Pole sana
 
Du wakuu long time sana. Ila hiyo ya kutumika kama stendi ya tv for 3 months ilikuwa ni zaidi ya ugaidi!
 
Aiseee nakumbuka mshua alikuwa zaidi ya mkoloni, nina dogo langu lilikuwa linapenda kujisaidia kwenye uzio kisa choo kipo mbali, siku ya siku mzee akamfuma alikula stick za kufa mtu na akamlazimisha kula mavi yake toka siku hiyo aliona choo kipo karibu ata kama ni night.
Mimi mwenyewe alileta stand mpya ya tv hizi za kichina sasa muda asiokuwepo uwa tunatoa tv tukalia juu mwingine anakusuma inakuwa kama starehe fulani hivi kwa ilikuwa na maraisi, sasa mwisho wa siku. nikiwa juu naendeshwa huku narukaruka ikavunjika, mzee aliporudi kauliza kila mtu kimya, akatuita chumbani alizungusha waya nne nne kwa kila mtu wenzangu uvumilivu ukawashinda wakanitaja, aiseee nilipigwa sijapata ona hadi leo alama ipo. Baada ya kipigo ikawa kila ikifika kipindi cha taarifa ananiita nashikilia tv kichwani mpaka amalize kuangalia taarifa ndio natua, it takes almost 3months ndio akaleta stand nyingine
Haahahahhahahahahhahahhaha
 
Zile shuruba(suruba ),seleka za waqt ule ukizifanya kwa vijana wetu wa leo murder case nyingi na pale muhimbili (moi )wateja wataongezeka.
Kuna siku bimkubwa kampelekea dogo vile visahani vya chai vya udongo kwanza nakumbuka maana kilirushwa kwa ueledi mkubwa kama olimpic medal ingemuhusu basi kilikwenda na kumkosa dogo kikapiga ukutani najaribu kulikumbuka tukio hilo.
 
Mzee alikua na.adhabu mbaya kisaikolojia...Sikukuu ya Idd umenunuliwa nguo mpya ukitoka masjid ukaenda kuzurura kabla yakurejea home tu..ukija unavua nguo anakwambia chukua jembe kalime pilau ya idd itakufuata huko shamba alaf wenzio wanaenda kutembea daaah mpaka nasisimka nikikumbuka
 
1. Mimi na bro tulikuwa tunatoroka shule na solution pekee ya mzee ilikuwa kutuwekea daftari la mahudhurio shule na nyumbani. Yani ukiingia asubuhi unaenda kusign na ukitoka unasign, ukifika nyumbani una sign umefika saa ngapi halafu kila mwisho wa mwezi anaenda kulinganisha! Ilikuwa aibu sana siku mwalimu alipotufuata class na daftari anatuambia tu-sign ndo tuondoke!!!

2. Yeye mbinu yake ya kujua kama TV imewashwa ni kupitisha mkono pale mbele ya screen...ole wenu akisikia kile kimlio (hata sijui nikielezeeje)

3. Pamoja na kutuchapa sana mpaka nyakati nyingine majirani walikuwa wakija kutombea msamaha (na hii baadaye tuliitumia kama defence tukiona kiboko kimezidi potelea mbali tunaanza kulia kwa nguvu mpaka majirani wanakuja wanagonga dirishani) alikuwa anaweza kutumudu wawili..yani anatukamata anatuweka katikati ya mapaja yake tunakula fimbo mpaka tufurahi.

4. Kuamka ni saa kumi na mbili...iwe likizo au siku ya shule...anasema, "Hata wagonjwa KCMC ni lazima waamke asubuhi wanyweshwe dawa!" Kulala ni saa nne. Kurudi nyimbani ni 6pm.

5. Hakuna kuvaa malapa ya dukani..zetu zilikuwa 'maraaiyoo/matairi' kisa ndo yanadumu zaidi.
Kumbe utundu umeuanza siku nyingi!!
 
Come to think of it, vimbwanga vingi vya madingi wa enzi zetu haikuwa ukoloni as such, bali walikuwa wanainstall discipline kwa watoto wao na kuwafunza tabia njema. Siku hizi wazazi wanachekacheka sana na vitoto vyao to the extent unaweza kutembelea nyumbani kwa mtu na kitoto kikakufukuza tu au kukwambia maneno ya aibu sana, na mzazi wake yupo akiangalia tu na kukuomba samahani. Sasa hivi dingi anaweza kupark mkoko wake na mwanae akauchukua na kuudrive tuuu bila hata ruhusa. Thubutu enzi zile uone. Kugusa hata baiskeli tu ilikuwa kama umefanya murder vile.

Mzee wangu alikuwa mkali pia. Mimi nilikuwa mtundu wa wastani kiasi kwamba akikuta tunacheza na watoto wengine labda mmoja akaumizwa na kuanza kulia, nilikuwa napewa kisago tu bila kuuliza, akiassume mimi ndo nimefanya ule msala. Kupitia hayo mapito nilijifunza ''negotiation/facilitation/peace building skills'' toka enzi hizo na nilikuwa naamua ugomvi wa watoto wenzangu mapemaa kabla mmoja hajaanza kulia..
Umenikumbusha siku moja tulikwenda kumtembelea dada mmoja, wageni tukakaribishwa na kupewa vinywaji kadri ya tulivyotaka, mie nikawa nakunywa maji na mwenzangu anakunywa soda, mtoto akaja akamnyang'anya mwenzagu soda eti 'lete soda yetu' akaondoka nayo na yule mama yupo tu 'jamani huyu mtoto mkorofi'
Nikawaza hivi enzi zile za wazazi wetu sijui tukio gani lingefuata hapo!!
 
Yupo mtoto wa swahiba yangu Ilikuwa ndo mara ya kwanza tunakutana sasa mzee wake akaingia ndani kwenda kunitafutia kitu nilichofuata dogo akaanza mambo hayo mara kanirukia mara hivi basi nilimvizia kisha nikamkamata uzuri na kumsina waqt huo navuta kumbukumbu wale mabibi zetu walivyokuwa wakisina kama nusu dakika hivi nikamuachia wacha apige yowe bimkubwa wake kaja junior unalilia nini? dogo analia tu hakusema kitu sijui labda nilipoondoka ila ilisaidia maana baada ya hapo alikuwa akiniona adabu ilichukua mkondo wake .
 
Umenikumbusha siku moja tulikwenda kumtembelea dada mmoja, wageni tukakaribishwa na kupewa vinywaji kadri ya tulivyotaka, mie nikawa nakunywa maji na mwenzangu anakunywa soda, mtoto akaja akamnyang'anya mwenzagu soda eti 'lete soda yetu' akaondoka nayo na yule mama yupo tu 'jamani huyu mtoto mkorofi'
Nikawaza hivi enzi zile za wazazi wetu sijui tukio gani lingefuata hapo!!

huwezi jua kilichofuata baada ya nyie kuondoka!

Hata sisi hatukuwahi kupigwa wageni wakiwepo ila sasa subiri waondoke...!!!! utaomba warudi...
 
Hahaha madingi wa Kiafrika magaidi sana ila poa tu vitendo vyao vilisaidia kukuza watu katika heshima na maarifa pia

Nasoma uzi humu nakumbuka msala wa dingi yake Domokaya na Mandojo

Sijui nini sufuria kazitia misumari

Kumkomoa maza housegirl si kamtia mimba.........
 
Daah nakumbuka kipindi tukiwa wadogo mzee wetu alikua na tabia ya kutuchapa kila anunuapo bidhaa mpya na kuileta nyumbani.Mfano Nakumbuka siku moja alinunua chupa ya chai kabla hata haijaanza matumizi akatutia bakora huku akitusihi na kutukanya kuwa tukiichezea inaweza kupasuka,Basi ikawa kila akinunua kitu chochote akikileta nyumbani lazima tuchapwe!![emoji22] [emoji22] [emoji22] [emoji22]

Duuh,huyo alikuwa mjerumani pure.
 
Mzee alikua na.adhabu mbaya kisaikolojia...Sikukuu ya Idd umenunuliwa nguo mpya ukitoka masjid ukaenda kuzurura kabla yakurejea home tu..ukija unavua nguo anakwambia chukua jembe kalime pilau ya idd itakufuata huko shamba alaf wenzio wanaenda kutembea daaah mpaka nasisimka nikikumbuka
dah kweli mzee mkolon kinoma
 
Tulikuwa na jirani yetu mzee digalile yeye akiamka alfajiri akienda msalani kuna mtungi kule anakuta maji ni ya baridi sana kuliko mtungi wa sebuleni nadhani alivumilia sana hali ile ikamshinda siku isiyo na jina kamwita bint yake mkubwa akatoe mtungi wa msalani akamwambia aukoshe uzuri baada ya hapo wa sebuleni ukapelekwa msalani na wa msalani ukahamia sebuleni maisha yakaendelea
 
Nilikua nachukia kishenz...

Wakat niko Primary, nikiwa wa pili na kuendelea darasan basi dingi ananipiga stick "kwanini umekua wa pili??? Huyo wa kwanza anakuzidi nini???"

Basi nikawa na mind kishenz yaan. Maana rafik yangu Lombiza yeye hata akiwa wa 30 huko dingi yake hata hamchapi...

Thanks for that attitude, maana nilijengwa kuwa wa kwanza class from darasa la nne mpaka namaliza form six nilikua nakimbiza tuu...

Bila stick za dingi leo hii nisingelikua Engineer.

[HASHTAG]#Chief[/HASHTAG] Eng
 
Daah nakumbuka kipindi tukiwa wadogo mzee wetu alikua na tabia ya kutuchapa kila anunuapo bidhaa mpya na kuileta nyumbani.Mfano Nakumbuka siku moja alinunua chupa ya chai kabla hata haijaanza matumizi akatutia bakora huku akitusihi na kutukanya kuwa tukiichezea inaweza kupasuka,Basi ikawa kila akinunua kitu chochote akikileta nyumbani lazima tuchapwe!![emoji22] [emoji22] [emoji22] [emoji22]
Haha
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] nadhani hii itafunika zote aiseee.
 
Back
Top Bottom