Kiona
JF-Expert Member
- Feb 3, 2012
- 933
- 240
Hivi Gazeti la Mwanahalisi liko wapi?
Naye Dr.ulimboka amehamia nchi gani?
Hivi mgomo wa walimu lini?
Na mafisadi wa EPA watanyongwa lini?
Hivi unakumbuka mbunge analipwa posho kiasi gani kwa siku?
Unakumbuka bunge liliamuru bwana jairo na philimon Luhanjo wafukuzwe kazi iliishia wapi?
Unakumbuka mazishi ya Balali yalivyokuwa?
Je unakumbuka kifo cha mwandishi wa habari Daudi mwangosi?
Hivi sakata la Richmond,Dowans linaendaje?
Hivi twiga walioibiwa na wageni wamerudishwa?
Tafakari tusiwe wepesi wa kusahau jamani, sisi ndio wajenga nchi.
Nisaidieni majibu hayo yote yameishia hewani