Tukumbushane Wakuu wa Mikoa wa miaka ya nyuma

Tukumbushane Wakuu wa Mikoa wa miaka ya nyuma

Mjukuu wake ndio yule msanii anaitwa Athuman Kabongo aka Dark Master aliyeimba na Mangwea wimbo wa She Got Gwain
Hivi kwao asilia ni Mkoa gani, nadhani yule mzee alipohama Iringa miaka ya 1980+ alikwenda Dodoma kama sijakosea sana
 
Huu uzi ungenoga ungekuwa hao ma RC wanatajwa kwa makundi kimikoa, nahisi baadhi ya mikoa ingekuwa blank kwakuwa ma RC wao walikuwa passive sana kiasi hata wananchi wao hawakujua kama walikuwepo
 
magesa mlongo,mzee wa kutoa macho. Hakika serikali haina shukrani,huyu jamaa sijuji alienda wapi
 
Jambo la kusikitisha ni pale hawa Vijana na MaDC wa Jiwe wasivyokuwa na adabu kuwaheshimu hawa wazee waliowatangulia na kuwasafishia njia. Siku moja nilikwenda kwenye ofis ya Mkuu wa wilaya mmoja nikamkuta Mkuu wa Mkoa mstaafu amewekwa benchi anamgoja mkuu wa wilaya aliyekuwa ndani ya ofisi ili apate kumuhudumia!!!

Kuna umuhimu wa kuwapa darasa hawa Vijana kuwa hawa wazee wanapokwenda kupatiwa ufumbuzi wa shida zao wahudumiwe kwa heshima kwani kazi walizofanya huko Nyuma ni za kutukuka!!! Waziri Mkuu ana wajibu wa kuwaandikia circular hawa walioteuliwa sasa kuwa wana wajibu wa kuwajua wale waliowatangulia; wajue kuwa wanasimama juu ya mabega ya hawa watangulizi wao hivyo ni lazima kuwapa heshima yao.

Na kuwafahamu watangulizi wao hakuna shida kwani kuna utaratibu wa kuorodhesha majina ya wote waliopitia ofisi hizo ikiwa ni mikoani na wilayani. Ukiingia katika ofisi hizo kulikuwa na vibao vimetundikwa ukutani vikiwa na orodha hizo; sijui pengine huu utawala wa Jiwe umepiga marufuku utamaduni huo!!!
 
Back
Top Bottom