Jambo la kusikitisha ni pale hawa Vijana na MaDC wa Jiwe wasivyokuwa na adabu kuwaheshimu hawa wazee waliowatangulia na kuwasafishia njia. Siku moja nilikwenda kwenye ofis ya Mkuu wa wilaya mmoja nikamkuta Mkuu wa Mkoa mstaafu amewekwa benchi anamgoja mkuu wa wilaya aliyekuwa ndani ya ofisi ili apate kumuhudumia!!!
Kuna umuhimu wa kuwapa darasa hawa Vijana kuwa hawa wazee wanapokwenda kupatiwa ufumbuzi wa shida zao wahudumiwe kwa heshima kwani kazi walizofanya huko Nyuma ni za kutukuka!!! Waziri Mkuu ana wajibu wa kuwaandikia circular hawa walioteuliwa sasa kuwa wana wajibu wa kuwajua wale waliowatangulia; wajue kuwa wanasimama juu ya mabega ya hawa watangulizi wao hivyo ni lazima kuwapa heshima yao.
Na kuwafahamu watangulizi wao hakuna shida kwani kuna utaratibu wa kuorodhesha majina ya wote waliopitia ofisi hizo ikiwa ni mikoani na wilayani. Ukiingia katika ofisi hizo kulikuwa na vibao vimetundikwa ukutani vikiwa na orodha hizo; sijui pengine huu utawala wa Jiwe umepiga marufuku utamaduni huo!!!