Tukumbushane Wanasoka wastaarabu na wapole wawapo dimbani

Robbie Fowler...

Huyu jamaa aliwahi kumkatalia refa kwamba penalty aliyopewa siyo sahihi kwa sababu hajafanyiwa madhambi, ilikuwa game ya LFC vs Arsenal.

Refa aliendelea na msimamo wake, Fowler alikosa ila kuna mchezaji alifunga rebound.
 
Samli Ayoub beki mstaarabu. Watakaomjua ni wachache sana
Jamaa alikua beki kisiki wa Majimaji ya Songea, Majimaji ya kina Peter Mhina, Octavian Mrope, Selestin 'Sikinde' Mbunga(R.I.P), Peter Tino, Madaraka Selemani na wengineo. Alikua anatoka uwanjani bila vumbi wala tope japo kazi aliyokua anafanya uwanjani si yakitoto
 
Egyptian king
Kweli Moh Salah ni mstaarabu sana, akishaitundika goli timu aliyowahi kuichezea e.g. Chelsea, Roma huwa hashangilii kuonyesha heshima, bali hunyanyua mikono juu kuomba radhi..Tofauti na wengine ndio huonyesha kejeri hasa kwa kujipiga kifuani n.k.
 
Jamaa anaujua mpira na nidhamu uwanjani anayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…