Tukumbushane: What is your childhood memory?

Papa Mobimba

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2018
Posts
1,153
Reaction score
1,359
Nilianza darasa la kwanza nikiwa mkubwa kidogo, nilikuwa na miaka. Nikiwa darasa la pili nilikuwa naweza kucheza karata kwa ustadi mkubwa. Ikafikia point nikatega shule nikawa nakwenda kijiweni nachezea watu wananilipa.

Baada ya kupigwa mkwara nyumbani nikaamishia karata darasani. Siku hiyo kuna jamaa akanisema kwa mwalimu nimekwenda na karata. Mwalimu alivyoniita, nikapitia dirishani nikakimbia.

Kesho yake, Mwalimu Mkuu akanisemea kwa mjomba ambaye alikuwa mwalimu pia kwenye hiyo shule. Aisee mjomba alinichapa kama anaua paka shume.

Nilichapwa nikachapika mpaka nikajikolea. Mjomba alipokuja nyumbani jioni akanipa pesa niende kununua panadol.

Mpaka leo nina kovu la fimbo kwenye paja.. nikanyooka kuanzia siku hiyo.

What is your childhood memory. Unakumbuka nini wakati wa utoto wako?
 
Nilikua darasa la sita
Nakumbuka tulikua tumepewa homework ya hesabu mwalimu akawa anapita kusahisha basi katika usahihishaji mwalimu akanikosesha swali ambalo nilikua nimepata( I was best in maths) nikaanza kulalamika kwamba mwl umenikosesha naona mwl haelewi kilichofata.

Nlimtwanga mwalimu konzi πŸ˜”πŸ˜” as alikua ameinama kwenye desk anasahisha
Yanii darasa Zima waliona.

Kilichofata nikaambiwa nipige magoti mbele kwanza hakuna aliyetegemea mi mwenyewe hata sijui nikipata wapi Ile akili nikala stick za kutosha sema na ujembe ulisaidia kuonewa huruma.

Ila sijawahi kurudia TenaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Yani primary na utoto wangu Ina historia nyingi Sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…