Papa Mobimba
JF-Expert Member
- Dec 6, 2018
- 1,153
- 1,359
Nilianza darasa la kwanza nikiwa mkubwa kidogo, nilikuwa na miaka. Nikiwa darasa la pili nilikuwa naweza kucheza karata kwa ustadi mkubwa. Ikafikia point nikatega shule nikawa nakwenda kijiweni nachezea watu wananilipa.
Baada ya kupigwa mkwara nyumbani nikaamishia karata darasani. Siku hiyo kuna jamaa akanisema kwa mwalimu nimekwenda na karata. Mwalimu alivyoniita, nikapitia dirishani nikakimbia.
Kesho yake, Mwalimu Mkuu akanisemea kwa mjomba ambaye alikuwa mwalimu pia kwenye hiyo shule. Aisee mjomba alinichapa kama anaua paka shume.
Nilichapwa nikachapika mpaka nikajikolea. Mjomba alipokuja nyumbani jioni akanipa pesa niende kununua panadol.
Mpaka leo nina kovu la fimbo kwenye paja.. nikanyooka kuanzia siku hiyo.
What is your childhood memory. Unakumbuka nini wakati wa utoto wako?