Balanta....! unaweza shusha mistari hapa as well + ile kibao cha Monica........kukimbilia Zambia etc etc....?
Mkuu lyrics hizi hapa
1.Sauda
Sauda,Sauda oooh,Sauda dada
Tangu tuwe wapenzi tumependana kikweli pendo letu la moyoni,
Mioyo tusibadili wangu kipenzi dada tuepuke ushauri
Kwa mahasidi wa penzi ooh Sauda kwa mahasidi wa penzi mama ooh Sauda

Sauda ooooh mama,Sauda ooooh mamaaa
Mv Mapenzi meli ya wapendwa nao,moyo kama bahari manahodha mimi na wewe

(Gurumo) Duniani kuna mengi sawasawa na bahari,kuna papa na nyangumi tena wale wa hatri,hawapendi kuiona meli yetu baharini watafanya kila njia waifupishe safari
Mv Mapenzi meli ya wapendwa nao,moyo kama bahari manahodha mimi na wewe
Mv Mapenzi meli ya wapendwa nao,moyo kama bahari manahodha mimi na wewe
(Gurumo) Duniani kuna mengi sawasawa na bahari,kuna papa na nyangumi tena wale wa hatri,hawapendi kuiona meli yetu baharini watafanya kila njia waifupishe safari Sauda eeh
2.Kesi ya Khanga(Monica)-ZAITA Musica
Mama nipe nauli nikamfuate Monika ee,amekimbilia Zambia na treni ya mizigo ee,kisa cha kukimbia madeni yamemzidi doti kumi za khanga alizokopa hajalipa ee,anatafutwa na Polisi popote hapatikani,na mimi rafiki yake nipo nje kwa mdhamana ee,nililala rumande siku mbili kituoni,usumbufu nilioupata kwa kweli sina raha ee

Naona bora niende Zambia nikamtafute Monika,nimlete Daresalama apambane na kesi yake,e Monika eeh uko wapi

Mahakamani wameshapanga siku ya kusikiliza kesi,asipokuja nitapelekwa jela kutumikia kifungo,ee Monika eeeh uko wapi ee,Monika eeh

Naona bora niende Zambia nikamtafute Monika,nimlete Daresalama apambane na kesi yake,e Monika eeh uko wapi eeeeh