Tukumbushane ya Pugu Sekondari

Long live pugu boys! Nilipiga PCB pale.... Enzi za Shirima, maisha yalikua magumu sana, chakula ni mihogo na machungwa, kudrop kula wali kwa mama ntilie gomz, aisee acha tu
 
Long live pugu boys! Nilipiga PCB pale.... Enzi za Shirima, maisha yalikua magumu sana, chakula ni mihogo na machungwa, kudrop kula wali kwa mama ntilie gomz, aisee acha tu
Me nilipiga O level pale kipimdi cha Shelimoh. Nilivotoka pale nikatupwa Ndanda High School kule Ndanda msosi ilikuwa raha sana na maji ya kumwaga.
 

Mimi nilikuwa Pugu kwa miaka miwili ya High School (Form 5 & 6). Huo mwaka nilioingia hapo ndio ulikuwa wa kwanza tangu shule kuchukuliwa na serikali na shule ikawa inaitwa "Pugu Secondary School" badala ya "St. Francis Pugu Secondary School". Hata majina ya mabweni yalibadilishwa kutoka ya kidini kuwa ya kisiasa. Mimi nilikuwa nakaa bweni la Azimio ambalo wale waliosoma hapo toka Form 1 walituambia bweni hilo lilikuwa likiitwa Charles Lwanga. Mwalimu Mkuu alikuwa Hokororo ambaye baada ya miezi michache tu alihamishwa na kupelekwa kwenye ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa. Nafasi yake ikachukuliwa na mwalimu Kategile ambaye hatukupenda sana uongozi wake.
 
Je kipindi hiko mlichokuwa mnasoma niambie sifa za bweni la Mapinduzi maana nasikia lile bweni hostoria yake haijabadilika kwa kukaa wanafunzi watoro na madoja.
 
PUGU PUGU PUGU.
Nimesoma pale chini ya uongozi wa mkuu wa shule anaitwa Mwero.Mwenyew anadai kirefu cha Pugu ni Pata Ujuzi Gawia Umma.
Huwezi taja chemistry bila kuwataja walimu kama Shilondinga (sijui jina lake halisi),mwl Kaundula,mwl Anjelo na Master plan Kibiriti.
Physics na wakali kama mzee Nzoe,Senzota n.k huku hesabu ikibebwa na wakali kama Madamu Muchunguzi na Shoki wa EGM..
Nakumbuka kuna mwalimu alikuwa ana watoto wake wa kike watu walikuwa wanoawatumia tu bila kujali haha,mi pia nilikuwa na mchepuko wangu wa kizaramo chini kidogo ya nyumba za walimu uliitwa Grace siku moja Mabagala alinikuta nao usiku tukakimbizana sana (alikuwa hachoki huyu mzee)

Kuna wakali kama Rwezahula (R.I.P) na wababe kama Nampanda na yule mwalimu mlemavu jina simkumbuki.
Kuna wanafunzi wasiosahaulika kama babu wa mapinduzi 7 bila kumsahau Pendeka haha Pugu acha iitwe Pugu.
Mama Mzula,Mama Amina na wengine ndo waliolainisha kidogo maisha ya pugu kwa kuuza vitu vidogo dogo.

Pugu na pondi....DH na kumiss chakula...... Kibiriti na Prac...... Lamboto na kudrop.......beto na harufu.......

Yote tisa,kumi ni yule Chatu wa Mapinduzi 7 kwenye mti mkubwa haha...huyu chatu watu wanadai bado yupo hadi leo.

Kwa sasa mimi ni injinia lakin ni zao la Pugu kabisa,proudly Pugu boy......Ita polisiiiiiiiii hahahaha
 
Dah.....
aisee nilisoma pale kipindi cha Magambo....
Tukaandamana hadi Wizara ya Elimu
Aka hamishwa....
 
Huyo Kaundula mimi ni Baba yangu Mlezi(Baba wa Kambo), kwenye masomo ya Chemistry na Physics alikuwa akinisaidia sana vitabu kama una namba zake niPM mkuu maana nilivurugana nae ndo nikatoka kwake kwa hasira nikaenda zangu Bush kujipanga, lakini namwombea kwa Mwenyezi Mungu apate Baraka tele, na Mr.Mabagala alikuwa ni best yake, dah! Umenikumbusha mbali mkuu
 
Pugu ni chuo kikuu tosha,Unajufunza kujisimamia
Maisha magumu sana lakini purukushani zake zinakufanya kuwa strong.
Kwanza pugu boys tunapendana sana, haijalishi mtu alisoma lini na kidato kipi,.
 
Pugu ni chuo kikuu tosha,Unajufunza kujisimamia
Maisha magumu sana lakini purukushani zake zinakufanya kuwa strong.
Kwanza pugu boys tunapendana sana, haijalishi mtu alisoma lini na kidato kipi,.
Sure ...Ile hali ya kukaa mchanganyiko ili tusaidia Sana



Viva PuGuuuuuuu
 
 
Hahahaha pugy boy dah kuna mwalimu mmoja alikuwa mswahili sana sijui anaitw juma sikumbuki vizuri hivi shile bado yupo pale shoki magesa etc
 
Mama P alikuwa anauza viazi na mihogo. Kuna veteran mwingine Mama G kwenye maji, kumbuka Nzoih na physics alikuwa ananyuka bakora mpaka PCB tukaipenda physics kwa lazima.

Mr Ogesa, Madame S Mtuwa Biology. Mimi niliripoti tarehe 28 april siku ya alhamis nikapangiwa Mapinduzi 7 na tarehe 30 wakaniibia viatu kisha nikahamia Azimio 2 the same day.

Kulikuwa na madogo wa O level wezi kinoma kule. Darasa letu la Form six F nililipenda kwa sababu tulikuwa tunawaona waschana wakipita kwenda kanisani na hivyo kila mtu alitaka kukaa upande wa kushoto kwenye dirisha. Daaaa Pugu shule tamu sana.

Kuna kitu kilikuwa kinaitwa P.E (Pumb.u Erotion) ni hatari sana kila mda unajikuna na ukienda Mchikichini Mkandawile anakuumbua labda usijishike mfukoni.
 
Mpaka natoka Pugu huyu Anjelo hakuwahi kumpenda mtu anaitwa Mkandawile kwa maana tulikuwa tunapiga tuition kwa Mkanda ila Anjelo akiita watu hatutokei
 
Wazee wa Five Z!!

Long live Nzoi...


Nilikua naelewa Sana mikwara yake...

siku Shile akiwa on duty asembo Ina jaa faster!!
 
Hivi haya maneno DOCEBIT VOS OMNIA yanamaanisha nini? Yameandikwa kwenye ule ukuta una-oface parade ground, halafu kwa juu yake kuna picha ya Njiwa/Hua
Hayo maneno yanamaanisha "atakaposhuka (hua/njiwa/roho mtakatifu) Atawafundisha yote.... (vos omnia - everything )
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…