Tukumbushane ya Pugu Sekondari

Tukumbushane ya Pugu Sekondari

Long live pugu boys! Nilipiga PCB pale.... Enzi za Shirima, maisha yalikua magumu sana, chakula ni mihogo na machungwa, kudrop kula wali kwa mama ntilie gomz, aisee acha tu
 
Long live pugu boys! Nilipiga PCB pale.... Enzi za Shirima, maisha yalikua magumu sana, chakula ni mihogo na machungwa, kudrop kula wali kwa mama ntilie gomz, aisee acha tu
Me nilipiga O level pale kipimdi cha Shelimoh. Nilivotoka pale nikatupwa Ndanda High School kule Ndanda msosi ilikuwa raha sana na maji ya kumwaga.
 
Si vibaya mtu ukikumbuka ulipotoka.

Nakumbuka siku ya kwanza kukanyaga Pugu ilikuwa tarehe 5 mwezi februari. ilikuwa ni siku ya mapumziko (public holiday), siku ya kuzaliwa CCM(Kwa miaka hiyo tarehe ya kuzaliwa CCM ilikuwa inaadhimishwa kitaifa na inakuwa ni mapumziko).

Nilipangiwa bweni la Maendeleo 2 na baada ya muda nilichaguliwa kuwa dom monitor. Kipindi kile pale Pugu mbele kidogo ya jiko kulikuwa na mradi wa nguruwe ambapo wanafunzi walikuwa wanawahudumia bila kujali wewe ni wa dini gani, mimi na wenzangu tulisimama kidete kupinga mradi ule hadi ukafutwa.

Nakumbuka shida ya maji ya kunywa pale shuleni na ilikuwa inatupasa twende pondi ya mzee wa shamba kuchota maji na kuja kuyafungia katika makabati yetu maarufu kama lockers.

Maisha ya bweni yalikuwa ni mazuri sana, ratiba ya chakula ilikuwa ni kama ifuatavyo: Tulikuwa tunakunywa uji saa 4, saa nane ugali maharage na usiku pia isipokuwa siku ya jumatano usiku ilikuwa ni siku ya wali maharage na alhamisi mchana tunapewa matunda(ndizi) na usiku wa alhamisi ni ugali kwa nyama(kipindi kile nyama tulikuwa tunaita kishoka).

Vyoo vya Pugu maarufu kwa jina la bettle vilikuwa vina harufu kali sana na ilikuwa inatupasa tuvue mashati kabla ya kuingia vinginevyo utanuka mpaka bwenini/darasani kwa harufu.

Pugu!!!!!!! nakumbuka mengi, walimu wangu akina Cobra "hilo ni jina la utani, jina lake halisi silikumbuki", mwl Charwe(huyu aliwahi kuninyang'anya viatu vyangu vya ngozi nilivyokuwa nimepewa na mzee wangu ambaye alikuwa ni afisa wa jeshi), mwl Juma Wasiwasi, Mwl Maliki, Mwl Shangwe, Mwl mukuru, marehemu mwl Swai, mabagala(sijui yupo wapi siku hizi), Mwl Mamilo, huyu alinikamata na "feki" la Physics NECTA na hatimae nikafutiwa matokeo yangu ya NECTA. Nimekumbuka sana shule yangu, ambayo imesaidia kujenga historia yangu.

WANA PUGU, MNAKUMBUKA NINI PUGU!!!! LET'S SHARE

Mimi nilikuwa Pugu kwa miaka miwili ya High School (Form 5 & 6). Huo mwaka nilioingia hapo ndio ulikuwa wa kwanza tangu shule kuchukuliwa na serikali na shule ikawa inaitwa "Pugu Secondary School" badala ya "St. Francis Pugu Secondary School". Hata majina ya mabweni yalibadilishwa kutoka ya kidini kuwa ya kisiasa. Mimi nilikuwa nakaa bweni la Azimio ambalo wale waliosoma hapo toka Form 1 walituambia bweni hilo lilikuwa likiitwa Charles Lwanga. Mwalimu Mkuu alikuwa Hokororo ambaye baada ya miezi michache tu alihamishwa na kupelekwa kwenye ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa. Nafasi yake ikachukuliwa na mwalimu Kategile ambaye hatukupenda sana uongozi wake.
 
Je kipindi hiko mlichokuwa mnasoma niambie sifa za bweni la Mapinduzi maana nasikia lile bweni hostoria yake haijabadilika kwa kukaa wanafunzi watoro na madoja.
 
PUGU PUGU PUGU.
Nimesoma pale chini ya uongozi wa mkuu wa shule anaitwa Mwero.Mwenyew anadai kirefu cha Pugu ni Pata Ujuzi Gawia Umma.
Huwezi taja chemistry bila kuwataja walimu kama Shilondinga (sijui jina lake halisi),mwl Kaundula,mwl Anjelo na Master plan Kibiriti.
Physics na wakali kama mzee Nzoe,Senzota n.k huku hesabu ikibebwa na wakali kama Madamu Muchunguzi na Shoki wa EGM..
Nakumbuka kuna mwalimu alikuwa ana watoto wake wa kike watu walikuwa wanoawatumia tu bila kujali haha,mi pia nilikuwa na mchepuko wangu wa kizaramo chini kidogo ya nyumba za walimu uliitwa Grace siku moja Mabagala alinikuta nao usiku tukakimbizana sana (alikuwa hachoki huyu mzee)

Kuna wakali kama Rwezahula (R.I.P) na wababe kama Nampanda na yule mwalimu mlemavu jina simkumbuki.
Kuna wanafunzi wasiosahaulika kama babu wa mapinduzi 7 bila kumsahau Pendeka haha Pugu acha iitwe Pugu.
Mama Mzula,Mama Amina na wengine ndo waliolainisha kidogo maisha ya pugu kwa kuuza vitu vidogo dogo.

Pugu na pondi....DH na kumiss chakula...... Kibiriti na Prac...... Lamboto na kudrop.......beto na harufu.......

Yote tisa,kumi ni yule Chatu wa Mapinduzi 7 kwenye mti mkubwa haha...huyu chatu watu wanadai bado yupo hadi leo.

Kwa sasa mimi ni injinia lakin ni zao la Pugu kabisa,proudly Pugu boy......Ita polisiiiiiiiii hahahaha
 
Dah.....
aisee nilisoma pale kipindi cha Magambo....
Tukaandamana hadi Wizara ya Elimu
Aka hamishwa....
 
Huyo Kaundula mimi ni Baba yangu Mlezi(Baba wa Kambo), kwenye masomo ya Chemistry na Physics alikuwa akinisaidia sana vitabu kama una namba zake niPM mkuu maana nilivurugana nae ndo nikatoka kwake kwa hasira nikaenda zangu Bush kujipanga, lakini namwombea kwa Mwenyezi Mungu apate Baraka tele, na Mr.Mabagala alikuwa ni best yake, dah! Umenikumbusha mbali mkuu
 
Pugu ni chuo kikuu tosha,Unajufunza kujisimamia
Maisha magumu sana lakini purukushani zake zinakufanya kuwa strong.
Kwanza pugu boys tunapendana sana, haijalishi mtu alisoma lini na kidato kipi,.
 
Pugu ni chuo kikuu tosha,Unajufunza kujisimamia
Maisha magumu sana lakini purukushani zake zinakufanya kuwa strong.
Kwanza pugu boys tunapendana sana, haijalishi mtu alisoma lini na kidato kipi,.
Sure ...Ile hali ya kukaa mchanganyiko ili tusaidia Sana

Viva PuGuuuuuuu
 
PUGU PUGU PUGU.
Nimesoma pale chini ya uongozi wa mkuu wa shule anaitwa Mwero.Mwenyew anadai kirefu cha Pugu ni Pata Ujuzi Gawia Umma.
Huwezi taja chemistry bila kuwataja walimu kama Shilondinga (sijui jina lake halisi),mwl Kaundula,mwl Anjelo na Master plan Kibiriti.
Physics na wakali kama mzee Nzoe,Senzota n.k huku hesabu ikibebwa na wakali kama Madamu Muchunguzi na Shoki wa EGM..
Nakumbuka kuna mwalimu alikuwa ana watoto wake wa kike watu walikuwa wanoawatumia tu bila kujali haha,mi pia nilikuwa na mchepuko wangu wa kizaramo chini kidogo ya nyumba za walimu uliitwa Grace siku moja Mabagala alinikuta nao usiku tukakimbizana sana (alikuwa hachoki huyu mzee)

Kuna wakali kama Rwezahula (R.I.P) na wababe kama Nampanda na yule mwalimu mlemavu jina simkumbuki.
Kuna wanafunzi wasiosahaulika kama babu wa mapinduzi 7 bila kumsahau Pendeka haha Pugu acha iitwe Pugu.
Mama Mzula,Mama Amina na wengine ndo waliolainisha kidogo maisha ya pugu kwa kuuza vitu vidogo dogo.

Pugu na pondi....DH na kumiss chakula...... Kibiriti na Prac...... Lamboto na kudrop.......beto na harufu.......

Yote tisa,kumi ni yule Chatu wa Mapinduzi 7 kwenye mti mkubwa haha...huyu chatu watu wanadai bado yupo hadi leo.

Kwa sasa mimi ni injinia lakin ni zao la Pugu kabisa,proudly Pugu boy......Ita polisiiiiiiiii hahahaha[/QUOTE

Ahahahahaha. Mkuu unakumbukumbu sana
 
Hahahaha pugy boy dah kuna mwalimu mmoja alikuwa mswahili sana sijui anaitw juma sikumbuki vizuri hivi shile bado yupo pale shoki magesa etc
 
Mama P alikuwa anauza viazi na mihogo. Kuna veteran mwingine Mama G kwenye maji, kumbuka Nzoih na physics alikuwa ananyuka bakora mpaka PCB tukaipenda physics kwa lazima.

Mr Ogesa, Madame S Mtuwa Biology. Mimi niliripoti tarehe 28 april siku ya alhamis nikapangiwa Mapinduzi 7 na tarehe 30 wakaniibia viatu kisha nikahamia Azimio 2 the same day.

Kulikuwa na madogo wa O level wezi kinoma kule. Darasa letu la Form six F nililipenda kwa sababu tulikuwa tunawaona waschana wakipita kwenda kanisani na hivyo kila mtu alitaka kukaa upande wa kushoto kwenye dirisha. Daaaa Pugu shule tamu sana.

Kuna kitu kilikuwa kinaitwa P.E (Pumb.u Erotion) ni hatari sana kila mda unajikuna na ukienda Mchikichini Mkandawile anakuumbua labda usijishike mfukoni.
 
Nawakumbuka sana teachers wa chemistry Shrondinga jina lake kimili nimelisahau alikuwa mzur sana kwenye organic chemistry
Kiberit..huyu alikuwa mzee daaa kwa practical za chemistry alikuwa njema sana na tulielewana sana maswali ya chemistry nilikuwa nayo niliyasolve yote kwa msaada wake kwahyo students ilikuwa lazma anione akitaka solution za practical aliwaelekeza waje kwangu
Anjelo..mtaalam wa physical chemistry nilifanya mitihan ming kwake
Mpaka natoka Pugu huyu Anjelo hakuwahi kumpenda mtu anaitwa Mkandawile kwa maana tulikuwa tunapiga tuition kwa Mkanda ila Anjelo akiita watu hatutokei
 
Wazee wa Five Z!!

Long live Nzoi...

Nilikua naelewa Sana mikwara yake...

siku Shile akiwa on duty asembo Ina jaa faster!!
 
Hivi haya maneno DOCEBIT VOS OMNIA yanamaanisha nini? Yameandikwa kwenye ule ukuta una-oface parade ground, halafu kwa juu yake kuna picha ya Njiwa/Hua
Hayo maneno yanamaanisha "atakaposhuka (hua/njiwa/roho mtakatifu) Atawafundisha yote.... (vos omnia - everything )
 
Back
Top Bottom