Tukumbushane ya Pugu Sekondari

Mr Kaundula! Mzee wa head on collitions of neutrons and electrons during chemical reactions! Bombardments, empty obitals na makolo kolo ya namna hiyo! Yule mwalimu kiboko sana! Tulikua tunamkubali sana! Hana time na mtu yeye ni kushusha nondo tu! Halafu kizungu mwanzo mwisho!
 
Mwalimu Sarawati kuna kipindi alihamishiwa Ifunda Technical miaka ya 2006,alikuwa Mwalimu wa Advance Physics pale,uwepo wa ulanzi pale ifunda ulimpendeza. ......huyu Proffesa na nguli wa Physics pombe iliharibu kipaji chake
 
kamwambie mama yako mimi ndio Nampanda ,kichaa kweli yule
 
Bwahahahahaha wa pondiiii

Sent from my SM-G950FD using JamiiForums mobile app
 

Cobra jina lake halisi alikuwa anaitwa Wajimila. Pia umesahau kitu kimoja kwamba saa 1 asubuhi kulikuwa na Chai. Possibly mlikuta imeshafutwa, kwa sababu inaonyesha wewe ulisoma kipindi ambacho Second Master Mr. Swai alikuja hatimaye akaaga dunia, sisi tulimwacha akiwa bado yuko hai, ila Mkuru alikuwa ameshapewa promotion kwenda Wizara ya Elimu. Pia kulikuwa na Mwalimu Mzava, amabaye alikuwa mwalimu pekee aliyekuwa anamiliki gari pale shuleni. Waliokuwa wanasoma PCB walikuwa wanamhara Charwe ukiingia kwenye Practical ya Biology huna chura. Kwa hiyo haikuwa ajabu kuwaona watu wa PCB usiku wa Mbalamwezi wanahangaika kukamata chura kwenye nyasi. Mimi nilikuwa PCM na walimu wangu walikuwa Cobra kwa Physics na Rwezaura kwa Advanced mathemativcs. Mwaka wetu tulipiga mahesabu kwenye mtihani wa NECTA tukawa wa kwanza kitaifa, kwa hiyo Rwezaura ilibidi apate zawadi!
 
People
Usually
Go
University
 
historia nzuri sana namkumbuka mwalimu Nzoy wa practicals za physics A level sijui kama bado yupo..mwalimu mzava alikuwa na vitoto vizuri balaa vilikuwa jangwani nadhani sisi tukawa tunatembea humo humo daaah..alikuwa peace sana yule mzee sijui kama nae yupo..palikuwa na mwalimu mchekeshaji kila siku parade lazima atuambie maana ya jina docebit vos omnia sikumbuki pia jina lake..nakumbuka pia fainali ya uefa champions league 1999 kati ya man u na Bayern (man u walichukua ndonga dakika za nyongeza wote tulijua amelala tayari) watu tukahamia kwenye TV ya pale kanisani kuangalia mpira wakati kesho yake ilikuwa pepa ya national six... enzi hizo lami kweli inaishia mwisho wa lami...Daaa those were the days.. nasikia siku hizi raha tu lami imepita kuna ukuta maji sio ya shida nk
 
Mimi niliondoka hapo mwaka 1992, wakati huo watoto wa mwalimu Mzava walikuwa wanasoma shule ya msingi, na wengine ndahani walikuwa bado wako chekechea. Ukiondoa Mzava ambaye sina taarifa zake, hao wengine uliowataja walishatwaliwa na Bwana. Mara ya mwisho nilifika Pugu ilikuwa mwaka 2013 na nilikuta walimu wawili tu walinifundisha, Mr Mabagala na Mrs Mugyabuso
 
daaaah heshima yako mkuu.wapumzike kwa amaani manguli wetu
 
Duu mzee una miaka mingapi mimi nimemaliza pale 2006
 
Huyo Mabagala kama ume doji parade, alikua anatutoa nduki kutoka Azimio hadi Pond hiyo ilikua 2008.

Nakumbuka wakati wa graduation yetu mgeni rasmi alikuja Pugu boy mwenzetu Mh. Mizengo Pinda akawa anatupa stori za enzi zao walivuokua wanapiga msuli bila kusahau huku watoto wa Jangwani na Azania wakienda Pugu kuburudika nao theque
 
Hahaha mwalimu nampanda alikuwa anapenda kusema '' Nitakupiga halafu ukaseme kwa mama yako akija mimi nampanda"

Namkbuka Nzoi wa physics alikuwa anapenda kusema nakupa vimaksi vya kupunguza pocket money kutoka kwa wazazi wako,

Kweli maksi za Nzoi ni maksi za viatu haswa.

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Kumbe mkal wa hesab SHOKI ni kitambo sana PUGU na msimazi wa miradi NAMPANDA mzee wa kilimo
 
Pugu na pond, P.E, kudrop kwenda lamboto, vidumu vya lita tano kutafta maji ya kunywa....

yote kwa yote Pugu inakuweka kuwa strong... Long live Pugu secondary and high school
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…