pmwasyoke
JF-Expert Member
- May 27, 2010
- 4,760
- 3,324
2011Kwani ilikuwa mwaka gani?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
2011Kwani ilikuwa mwaka gani?
Asante Mkuu. Watu wa mitaa ile tuliionja jehenama siku ile.Pole sana mkuu.
Umenikumbusha mbali sana mkuu. Kipindi hicho nilikuwa pale pembeni kabisa ya majengo ya chuo (nilikuwa nimeajiriwa kama producer kwenye studio moja hivi) mabom yalianza mida ya saa 11 kuelekea saa 12 jioni na watoto wakawa wanashangilia lin mida hiyo yalikuwa madogo, hayakuwa na kishindo wala mlipuko mkubwa. Kufika mida ya 12 kuelekea moja jioni mambo yakabadilika....nakumbuka niliacha studio wazi na nilikimbia nikajikuta nimetokea Ukonga gerezani. Pale ukonga tulitulizwa na askari tukalala chini wakati huo mizigo inapita juu kama vitani! Huo ndo ulikuwa mwanzo wa kurudi nyuma kwenye audio productioni japo baadae niliendelea.Nakumbuka siku hiyo wakati ukitokea mlipuko wa mabomu maeneo ya Gongo la mboto, nilikua sinza, ghafla nikaanza kuona miale ya moto juu ya anga, binafsi nilihisi labda tayari kimenuka.
Naanza kutafuta namna ya kuwatafuta watu wangu wa karibu naona simu hazitoki, nikasema ehee.
EBwana wee siku hiyo ilikua ya tofauti kidogo ila kesho yake tukaanza kupokea wakimbizi wa muda.
Wakati haya yanayotokea ulikua wapi na ulikua ukifanya nini?