Tukumbushane yaliyojiri mlipuko wa mabomu ya Gongo la Mboto

nilikua pugu boys pale asee tulikimbizana ovyo ovyo yani alafu ile shule ina wanafunzi wenyw ulemavu kilichotokea daah ...
 
Umenikumbusha mbali sana mkuu. Kipindi hicho nilikuwa pale pembeni kabisa ya majengo ya chuo (nilikuwa nimeajiriwa kama producer kwenye studio moja hivi) mabom yalianza mida ya saa 11 kuelekea saa 12 jioni na watoto wakawa wanashangilia lin mida hiyo yalikuwa madogo, hayakuwa na kishindo wala mlipuko mkubwa. Kufika mida ya 12 kuelekea moja jioni mambo yakabadilika....nakumbuka niliacha studio wazi na nilikimbia nikajikuta nimetokea Ukonga gerezani. Pale ukonga tulitulizwa na askari tukalala chini wakati huo mizigo inapita juu kama vitani! Huo ndo ulikuwa mwanzo wa kurudi nyuma kwenye audio productioni japo baadae niliendelea.
Kuna mambo mengi sana yalitokea lkn kwa bahati mbaya mimi si muandishi mzuri so nashindwa kuyaandika yote kwa mtiririko mzuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…