proton pump
JF-Expert Member
- Apr 30, 2017
- 6,814
- 10,104
- Thread starter
- #21
Hapo sasa wanataka koo zao zitawale milele.mi wananichosha hawa viongozi wetu...wanasema tukienzi kiswahili lkn watoto wao wote wanawapeleka English medium
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hapo sasa wanataka koo zao zitawale milele.mi wananichosha hawa viongozi wetu...wanasema tukienzi kiswahili lkn watoto wao wote wanawapeleka English medium
Kwani hicho Kiswahili chenyewe wanafaulu? Na kikifutwa Kiswahili unahisi ndio italazimisha wanafunzi kuwa mahiri kwa kiingereza? Mi nadhani tulitafakari kwa kina suala la lugha tz halihitaji majibu mepesiMimi naomba kiswahili kifutwe kuanzia shule za msingi, ndio maana hata wanafunzi bora shule za msingi hawawi bora sekondari .
Hapo sasa watuonyeshe mfano kwanza kwa watoto wao.mi wananichosha hawa viongozi wetu...wanasema tukienzi kiswahili lkn watoto wao wote wanawapeleka English medium
Itakua hata chenyewe isingekua mzungu kwani tungekiongea!Kwani hicho Kiswahili chenyewe wanafaulu? Na kikifutwa Kiswahili unahisi ndio italazimisha wanafunzi kuwa mahiri kwa kiingereza? Mi nadhani tulitafakari kwa kina suala la lugha tz halihitaji majibu mepesi
Nimekuelewa mkuuUfahamu wako no mdogo sn kuhusu dunia na kiswahili.china hawafindishi hicho kizungu chako.italia hawama hicho kizungu chako.ni mataifa mengi tuu yameendelea bira hicho kizungu chako.mtu yoyte aliesoma na akaelimika 《sio kasuka km mtoa post aliekalilishwa lkn hana elimu》anaenzi mira desturi na utamaduni wake.ni lazima tutambua thamani ya kilicho chetu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Ila mada imeletwa ijadiliwe tuUfahamu wako no mdogo sn kuhusu dunia na kiswahili.china hawafindishi hicho kizungu chako.italia hawama hicho kizungu chako.ni mataifa mengi tuu yameendelea bira hicho kizungu chako.mtu yoyte aliesoma na akaelimika 《sio kasuka km mtoa post aliekalilishwa lkn hana elimu》anaenzi mira desturi na utamaduni wake.ni lazima tutambua thamani ya kilicho chetu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Ila mada imeletwa ijadiliwe tuUfahamu wako no mdogo sn kuhusu dunia na kiswahili.china hawafindishi hicho kizungu chako.italia hawama hicho kizungu chako.ni mataifa mengi tuu yameendelea bira hicho kizungu chako.mtu yoyte aliesoma na akaelimika 《sio kasuka km mtoa post aliekalilishwa lkn hana elimu》anaenzi mira desturi na utamaduni wake.ni lazima tutambua thamani ya kilicho chetu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kila kunapokucha kiswahili kinasisitizwa sana kiwe lugha ya kufundishia kuanzia la kwanza hadi chuo kikuu,
Hiki kiswahili kitakupeleka wapi? Ili hali hata masomo ya art yameshapuuzwa? Wanafunzi wanasisitizwa kusoma sayansi la hasha hicho kiswahili wapi tena sasa.
Licha ya hivyo ni mtoto wa nan mwenye hela anasoma shule za kiswahili?
Tuna bidhaa gani tunazozalisha ili kutangaza kiswahili nchi za nje?
Bunge la afrika mashariki lenyewe lazima watu watoe sera kwa kiingereza
Ni masomo gani ya shule za sekondari yanatolewa kwa kiswahili isipokua kiswahili chenyewe?
Licha hivyo watafanya transilation lkn utakuta mtu kaandika labda chloroquine, sulfuric utabaidilishaje kwa kiswahili? Na hao unao waandaa watapata wapi soko?
Nchi nyingine wanakienzi kiingereza japokua kiingireza si njia kuu ya maendeleo
Tungekienzi mda huo tungekuta masomo yote yapo kwa kiswahili Lkn hadi sasa msingi kiswahili sekondari kiingereza.
Kiswahili kimeandaliwa ili maskini aendelee kuwa maskini kwa maana hapo ni fumbo,watoto wa matajiri wanasoma shule za kiingireza.
Unaonaje ukidadavua sentensi yako? Sijakuelewa ndo maana nimesita kukujibuItakua hata chenyewe isingekua mzungu kwani tungekiongea!
Unasema hivyo kwa vile hujui asili ya lugha hii pamoja na wenye asili ya lugha hii. Kwa asili lugha hii ni ya watu wa ukanda wa pwani ukianzia somalia hadi visiwa vya ngazija. Wenyeji wote wa sehemu hii hutumia lugha hii wakitofautiana lahaja tu.Kila kunapokucha kiswahili kinasisitizwa sana kiwe lugha ya kufundishia kuanzia la kwanza hadi chuo kikuu,
Hiki kiswahili kitakupeleka wapi? Ili hali hata masomo ya art yameshapuuzwa? Wanafunzi wanasisitizwa kusoma sayansi la hasha hicho kiswahili wapi tena sasa.
Licha ya hivyo ni mtoto wa nan mwenye hela anasoma shule za kiswahili?
Tuna bidhaa gani tunazozalisha ili kutangaza kiswahili nchi za nje?
Bunge la afrika mashariki lenyewe lazima watu watoe sera kwa kiingereza
Ni masomo gani ya shule za sekondari yanatolewa kwa kiswahili isipokua kiswahili chenyewe?
Licha hivyo watafanya transilation lkn utakuta mtu kaandika labda chloroquine, sulfuric utabaidilishaje kwa kiswahili? Na hao unao waandaa watapata wapi soko?
Nchi nyingine wanakienzi kiingereza japokua kiingireza si njia kuu ya maendeleo
Tungekienzi mda huo tungekuta masomo yote yapo kwa kiswahili Lkn hadi sasa msingi kiswahili sekondari kiingereza.
Kiswahili kimeandaliwa ili maskini aendelee kuwa maskini kwa maana hapo ni fumbo,watoto wa matajiri wanasoma shule za kiingireza.
Mbona inarleweka mkuuUnaonaje ukidadavua sentensi yako? Sijakuelewa ndo maana nimesita kukujibu
Mbona hakileti maendeleooooNikiwa kama mtu niliyewahi lugha zote mbili(Kiswahili na Kingereza) kisarufi na hata kifasihi, naomba nikujibu kama ifuatavyo;
Kiswahili kutumika lugha ya kufundishia kutoka ngazi ya juu hadi ya chini inawezakena ikiwa sote tutakuwa na nia ya kuruhusu jambo hili litokee. Kuanzia kila namna, hakuwezi kutokea jambo lolote baya ikiwa tutajiandaa vyema kulikabili hili. Hebu tuchukulie mfano lugha ya kichina, kijapana,kiarabu, kikorea, kifaransa, kihispaniola au kigiriki.
Hizo ni lugha ambazo hutumika kama sehemu ya kufundishia kwenye nchi husika, kutokana na kuwa mapenzi na kitu cha kwao basi wameweza kusonga mbele na wala hakuna kilichotokea ingawa wengine walitawaliwa kabisa na bado hawakupatwa na athari za wakoloni. Mfano China.
Tukumbukeni hata kingereza ni lugha ya waingereza, imesambaa tu duniani na kutambulika kutokana na waingereza wenyewe kuipenda na kuitumia kwa kila namna. Je sisi tunashindwa kufanya hili na ikashindikana?
Ilihali lugha yetu hivi sasa inatambulika ya kimataifa na vipo hadi baadhi ya vyuo barani Amerika, Ulaya na hata Asia wana hadi idara za kiswahili na kuna wasomi wanasoma wakitumia vitabu vya wafasihi wa nchi hii kujibia mitihani. Hii ni hatua nzuri hata waingereza walianza kwenye hali ya chini katika kuisambaza lugha yao, hadi wakafikia mahala hapo. Hebu tuipendeni lugha yetu kwanza, tuipe heshima na kutoona aibu kuongea popote. Huu ni uzalendo wa kweli.
Suala la kufundisha, mwanafunzi huelewa zaidi akifundishwa kwa kutumia lugha ya nyumbani kuliko ya kigeni. Hebu tujaribu kujiuliza ni mara ngapi walimu wamekuwa wakichanganya lugha ili waweze kueleweka, wakitumia ugha ya kingereza moja kwa moja ni ngumu mno kufahamika kile wanachokiongea. Hivi kiswahili kikitumika kutakuwa na tabu kama hizi?
Pamoja na hilo tukumbuke makadirio ya asilimia 78% ya wanafunzi wote nchini hawaelewi kile wanachofundishwa darasani kutokana na lugha, hii ni asilimia kubwa mno kutokana na wingi wa watu wenye kusoma shue za umma. Wanafunzi hukariri tu kuweza kujibia mtihani na si kuelewa, hivi hii ingekuwa ni kutumia lugha ya kiswahili ingetokea? Lugha mama ni muhimu mno kwa hivi sasa wanafunzi kufundishwa ili tupunguze idadi kubwa ya watu wanaofeli kwa kutoelewa hadi kufikia kununua kamusi waelewe.
Vilevile suala la maneno kama hiyo 'Sulphur' kuwepo na maneno mbadala kwenye kiswahili si sabababu haswa. Hivi iliwezekana vipi neno kama 'Mercury' kupatikana neno mbadala la kiswahili Zebaki. Jamani sarufi ya lugha ina kipengele cha uundaji wa maneno, zipo njia kama kukopa, kutohoa, uundaji kutokana na sauti, uundaji kutokana na umbo, ufupisho na njia nyingine nyingi. Hata kingereza chenyewe njia hizi imetumia kwenye baadhi ya maneno, hakijakamilika kama ilivyo kiswahili kuweza kujitegemea kwenye baadhi ya maneno. Kuna maneno ya kilatini mule mengi tu wanayatumia haswa huko kwenye nyanja ya sayansi, kwanini kwenye kiswahili isiwezekane.
Pia, kutokuwa na watoto wa wenye pesa wenye kusoma shule zetu za msingi zenye kutumia kiswahili siyo sababu. Hebu tupime idadi ya waafunzi wa shule za kawaida, na za wa hizo wanazoziita international schools. Wapi kuna wanafunzi wengi? Kina nani ambao wakiingia shule za sekondari huishia pabaya kwa kutoelewa lugha hiyo, ndipo utabaini hizi zinazojulikana shule za kiswahili ndiyo zenye watoto wengi ambao wakipewa mwongozo uleule wa kufundishwa watakuja kufikia kwenye namna nzuri hapo baadaye. Wingi wa hawa wakija kupewa kipaumbele hapo baadaye kwa kutumia lugha ya kiswahili kila mahali, ndipo kunaweza kukaleta mabadiliko chanya kwenye elimu kwa kutoa ufaulu mkubwa. Wingi huohuo pia ndiyo utakuwa chachu wa kuanza kufundishwa kiswahili hata kwa watoto wa matajiri. Hapo hakuna sababu kama ulivyosema kwenye mada yako.
KIPI KIFANYIKE?
Serikali inatakiwa ibadili mfamo wake wote wa kufanyika kwa kazi, uwe wa kutumia lugha hiyo pendwa ndiyoo kutaweza kufanya ajira hapa nchini iende namna ileile. Bidhaa kuandikwa kwa lugha hii pia ishinikizwe, naamini kwa kutumia nguvu yao tutaweza kufanikisha kutumiwa kwa lugha hii kwa kiasi kikubwa kwenye nyanja mbalimbali. Shule nazo ndani ya mfumo wa lugha yetu kuanzia kila ngazi, watakuja kuajiriwa vyema kwenye nyanja zake.
Pia ihimize kila sekta kubwa itumie lugha ya kiswahili kwenye kila shughuli zake, matumizi haya ndiyo yanaweza kuleta mabadiliko hata kwenye shughuli za sekta binafsi. Kwani nao wakiona kila wataalamu wazawa na hata wafanyakazi wenye kuwa na ujuzi fulani wanaelewa kiswahili tu, watabadili mfumo mzim wa utendaji na kuifanya kuwa ni lugha ya ufanyakazi. Hii hata wakoloni walifanya baada ya kuona kazi haziendi, wakaanza kuitumia kwenye shughuli zao. Kwanini tushindwe jamani?
Hayo mawazo ya kushindwa tukiyaweka mbele wala hatutofika popote pale, ugumu unaanzia hapo kwa kasumba zilizo vichwani mwa wengi mno juu ya kiswahili. Laiti kama tukiwa na maono chanya juu yake, tunaweza kufika mbali kabisa juu ya hili. Na kupelekea ipokewe vyema kimataifa, tukumbuke usambaaji wa kitu huanza kwa mzawa mwenyewe. Hata kingereza alianza Mwingereza kukisambaza ndiyo kukaja wengine kukipata.
Mabadiliko yanaanza na sisi, wala si kuangalia hali ilivyo juko nje ya nchi
Kiswahili ni alama ya kiafrika, tudumishe kuonesha alama yetu kwa kila mgeni.
Maendeleo yanaletwa na lugha au juhudi za watu? Mbona unachanganya habari?Mbona hakileti maendeleoooo