Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

Nakumbuka kuna siku niko peke yangu kwenye gari mchana kweupeee mitaa ya kkoo opposite na kituo cha polisi msimbazi.
Ishu ilikua hivi, kulikua na kifoleni cha kizushi tu gari zinasonga mdogo mdogo, na mie nipo kwenye foleni nimefunga zangu vioo nakula acc tu, nasogea kidogo nikasikia papapaaaa! Nikastuka, naangalia kwa umakini nje naona kila mtu anatafuta njia ya kukimbilia, wakati sijakaa vizuri naendelea kuzisikia tena papapaaa!
Kutazama pande zote kweupeeeeee yaani kama sio kkoo vile, mara namuona polisi anatokea kituoni ameshika mjegejo wake nae anapiga hewani huku anakimbilia pale ilipo gari yangu.(wakati huo mimi najiuliza, nifungue mlango nitoke nduki ama nifanyeje) mara kidogo zikalia tena upande wa pili(mtaa ule ilipo stand ya daladala za mbezi) zilipolia zile zilikua mfululizo mpaka yule askari akateleza(mie nikigeuza shingo huku nawaona wazee wa kazi hawa hapo hata presha hawana, nikigeuka huku namuona askari na mjegejo wake, hebu vuta picha upo mtu kati) basi bwana yule askari alivyoinuka tu akaifanya gari yangu guard/gadi.
Akawa anapiga juu jamaa nao wakajibu halafu haoooooo wakapanda kwenye bodaboda tatu wakasepa kuelekea yalipo makao ya klabu ya yanga, hapo ndo nikaona askari wengine wanajitokeza na raia wanaanza kurudi kwenye vyombo vyao.
Mie hapo kijasho kinanitoka pamoja na kuwa acc inawaka, sitaisahau hiyo siku, halafu kilichoniponza zaidi mpaka kujikuta uwanja wa vita ni kitendo changu cha kuwasha muziki wa sauti ya juu mpaka unashindwa kusikia mambo yanayoendelea nje, na hii tabia ilishawahi kunigharimu tena, ngoja niwape japo ni nje ya mada.
Kuna siku nayo ni mida ya mchana natoka zangu mitaa ya posta nakuja morocco, ujana mwingi nimefungulia mziki kwa sauti kuuuuubwa, nafika ile petrol station ya kabla ya mataa ya saint Peter’s nikaingia kujaza mafuta.
Nimemaliza fresh kabisa natoka ili niingie main road nakuta barabara nyeupeee hakuna hata gari, bwana bwana bwana! Hata sikujua nini kinaendelea mie nikaangalia kulia naona gari ipo mbali nikaingia, ile napandisha kile kilima kuelekea mataa naona mi V8 ya kutosha imeniweka mtu kati(kama mnavyojua magari ya msafara yanavyosambaaga barabarani, mara hili litoke kushoto kwenda kulia na lile nalo vile) msafara ukapunguza spidi kabisaaaa(na mie tayari nishachanganyikiwa nayumba tu na kagari kangu, kulia si kulia kushoto si kushoto naelea tu) kioo cha moja ya yale magari kikashushwa nikaonyeshwa tu alama za kidole ile ya weeeweeee!
Aaaah! Nilishtuka gari imezima japo ni auto(nilizima bila kujielewa yani)
Mara paaap msafara ukatembea nikabaki peke yangu nimetoa macho tu, kidogo askari yule aliekua kwenye mataa akaja mbiooo na kitambi chake
Kufika pale hakuna cha kuuliza nini wala nini nilikula makofi kama matatu ya kunirudisha kwenye hali yangu.
Nikawekwa siti ya nyuma, akaiwasha gari fasta akaipeleka kwenye kibanda chao kile cha kumalizana( hapo kumbuka hajanisemesha kitu) nafika pale nakuta clue nzima nikashushwa kama jambazi( mitama ya DAR to LAGOS nilichezea ya kutosha)
Baada ya hapo ndo naulizwa ulitaka kufanya nini mi nikawaambia sikujua kama kuna msafara
Wakaniambia umevamia msafara wa mke wa rais( kilikua kipindi cha babu cheka/mkwere)
Basi baada ya ile presha kutulia nikaanza kubembeleza yaishie pale, nikaambiwa ngoja mpaka msafara ufike salama ndo tutaongea
Ilinitoka 70 na nilikaa masaa matatu pale pale.
Nilipotoka hapo hata nikisikia honi ya bajaj napunguza mwendo kuhakikisha.
Yaani sitasahau. Poleni kwa kwenda nje ya mada


Sent from my iPhone using JamiiForums
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16], vipi hao wazee wa kazi kariakoo walikamatwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ilikuwa 2015 nikiwa mkoa mmoja wa kaskazini siku hiyo usiku wa saa 3 nimejiachia kichochoroni kuna msingi wa nyumba flani haijaisha nimekaa hapo na kabinti flani ka mtaa huo nilikuwaga nakatafuna!
Sasa tumekaa hapo huku demu ameweka laptop kwenye magoti anacheki movie mara ghafla tukazingirwa na vijana kama saba hivi umri kama miaka 17-20 hivi wana mapanga!
Wakaanza kutuchimba mkwara eti tuwaachie laptop, simu na pesa !
Demu alianza kulia kwa hofu lakini !
Lakini ghafla...nilipata ujasiri wa ajabu nikawarukia bila kutengemea nikakamata koromeo la mmoja wapo mpaka alikunya!
Waliishia mitini!

Sent using Jamii Forums mobile app
Alikunya wapi acha fix mzee[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku moja kabla ya mwaka mpya nilivamiwa na majambazi/Vibaka sugu home walikua kama watano hivi... Ilikua mida ya saa 8 usiku nipo pekeyangu home.... Walifanikiwa kuvunja grill la nje ile wanataka kuvunja mlango nikashtuka... Mkwara niliopiga walijua tupo 10 ndani.... Nikawaambia mbw* nyie mimi nipo ndani nyie nje mtu aingize shingo yake ndani.... Nimekamata panga huku natetemeka hahahaha asee usiombe ukutwe na hizi mishe...
All in all nilifanikiwa kuomba msaada kwa majirani jamaa wakasepa...
Mpaka sasa huwa nalala kimachale mno hofu bado ipo....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahaha
mie mwaka 2009 mwaka mpya walikuja njemba zaidi ya 10,nakumbuka mzee ndo siku alikuwa ameuza spacio yake kwa milioni 9 hata bank alikuwa hajaipeleka wakavunja mlango but kabla walipiga risasi moja juu mi nlivyoskia tu fasta nkapanda juu ya dari nlipanda vipi mpka leo sikumbuki basi wakafanya yao mzee alikuwa analia kama mtoto,asubuhi akaitwa mpemba akafanya dua yake bhana dah wapemba siyo watu wazuri maana baada ya dua tu jirani zetu zaidi ya wa 3 waliondoka siku ile ile mpka jioni vitu vyote vilirudi na faini juu
heahima kwenu wapemba


Sent from my iPhone using JamiiForums

Sent using Jamii Forums mobile app
 
HII YANGU ITAKUWA KALI NA HATARI ZAIDI......

Ilikuwa ni moshi mwaka 2009 mwezi wa sita mahindi yamekuwa marefu, miti mirefu, migomba mingi kiasi kwamba hata taa za umeme hazimwiliki vizuri na kuna wingu zito sana na GIZA NENE. Mida ya saa mbili usiku nimetoka town nimeshuka kwenye daladala, nikaingia njia ya kuelekea home. Njia hiyo mpaka kufika home ni parefu kidogo, halafu ina giza kuu. Katikati ya njia kuna geti la kuingia nyumba ya jirani, nilipofika pale nikakuta pikipiki mbili na washkaji waliponiona wakashtuka mmoja akaninyooshea bastola akaniambia lala chini. Sasa maana ilikuwa ghafla na tumekaribiana sana na nilikuwa najiamini sana nikamrukia nikashika ile bastola kuielekeza juu zikatoka risasi kama nne kwa haraka sana....... kumbe ndani kuna majambazi mengine manne yanaforce jamaa ayape hela na yameshatoa kipigo cha maana......

Yule jamaa baada ya risasi kuisha kwenye bunduki nikampiga ngumi akadondoka chini, mwenzake akawa anakuja na sime, ile anainyanyua anikate nikawahi kumdaka mkono nikampiga ngumi ya mbavu akaachia sime, nikampiga ngumi ya pili halafu nikawahi ile sime.
NIKAWAAMBIA MKINIFUATA NAWACHINJA, sasa mimi nilidhani walikuwa wananiwinda mimi kumbe jamaa walikuwa wanawasubiri wenzao. Mara nikaona majamaa wanne wameruka ukuta kwa speed ya hatari na wale wawili wakawasha pikipiki haraka sana wanaulizana imekuwaje jamaa akawaambia kuna mwanajeshi hapa tuondoke...... Wakati huo mimi nimeingia kwenye mahindi wakamulika na tochi huku na huku hawakuniona. Wakawasha pikipiki wakaondoka kwa kasi ya ajabu.

NIKABAKI PALE NA ILE SIME HUKU BADO SIELEWI NINI KINAENDELEA NDIYO SASA NDANI YA ILE NYUMBA WAKAANZA KUPIGA YOWE NA MAJIRANI WALIOSIKIA WAKAJA......

nakumbuka kilikuwa ni kitendo kama cha dakika mbili tu.

YULE MZEE ALINIPA LAKI MBILI AKANIAMBIA KAMA SIYO MIMI WANGEMUUA NA WANGEMUIBIA HELA NYINGI SANA.....
Hiyo siku sitaisahau aisee.
 
Eeeeeh bwana hili kundi unalifahamu mkuu??? Liliwahi kuvamia lodge ya home miaka ileeeee naishi home ila cha ajabu yanatembea na mapanga sijui majambia tu hayana bunduki...kumi yanajipanga nje kuangalia usalama na kumi mengine yanazama ndani... Siku hiyo mnyama nimejilaza usiku wa manane kumbe yalishamchorea ramani mshua mmoja alikuja kulala pale lodge na alikua na mpunga wa maana kwenye briefcase yake. Majamaa kuvunja mlango yule manager wa lodge akaanza kupiga kelele za msaada jamaa yakamuwahi alichezea kichapo huku kabanwa mdomo, muda huo nilishafika dirisha kubwa maana dirisha moja la hiyo lodge limeelekea home ila kutokana na kuwepo kwa liukuta lirefu na geti yasingeweza kuingia ndani... Sijui ule ujasiri niliutoa wapi nachokumbuka yaliingia kila chumba na jamaa limoja linaonekana ndio tembo lao lina booooonge la mwili ndio lilikua linajivuta linauvamia mlango unajiachia wenyewe. Wakaingia chumba kimoja wakakuta binti mkali amelala na kichupi tu nikasikia yanasema "Hatujaja kuangalia pichu wala chiu ya mtu hapa tunataka helaaaa tuuuu" basi mnyama si nikaropoka "Wewe hapo nimeona sura yako, na wewe hapo yaani inshort niliwataja kama wanne hivi wakawa wanatafuta sauti inatoka wapi maana mimi nje nawaona ndani maana nje giza ila ndani hawaoni nje sababu ya mwanga ndani. Jamaa kuona vile wakaongea "hoya mfanyieni kazi kuna dogo nje huku ametuchora, weeee kusikia vile acha nipige yowe la hatari nje "Jamani weziiiiiiiiiiiiiii" uzuri jirani yetu ni mwanajeshi mwenye nyota zake tatu akachomoka na bunduki yake usiku ikapigwa hewani "Paaaaaaah" majamaa yakaambiana "Kimenuka wana tusepe" yakakimbia mpaka kesho hata nikikutana nao siwakumbuki maana kwa ule uoga hata sikukariri sura zao kwa umakini ila wamewatesa saaaana wafanyabiashara wa maeneo ya kimara na mbezi miaka ile
Ulivyo jiita mnyama nikajua unaunyama Kweli Kama Savimbi ama Idiamiani kumbe paka tu[emoji1]
 
Wale vibaka wangu walikuwa wajinga sana..........2001 hiyo nimetoka zangu kupiga liquid narudi home kama saa 7 hivi ucku, nilipokuwa naishi kuna umbali kidogo kutoka barabarani, dereva taxi kanishusha nikaanza kukata vichochoro kuelekea nyumbani, ghafla nikamulikwa usoni na tochi yenye mwanga mkali sana halafu ikatoka amri kali eti:- simama hapo hapo na ujisachi mwenyewe utoe kila ulichonacho mfukoni........yani sikujiuliza mara mbili mbili, niligeuka kwa kasi na kufyatua mbio kali sana ambazo sijawahi kukimbia.

Kuona ivo na wao wakaniunganishia kuanza kunikimbiza halafu mbaya zaidi wakaanza kuniitia mwizi, mi kusikia ivo nikapunguza mwendo hatimae nikaanza kutembea kwa mwendo wa haraka, kuona natembea na wao wakaanza kutembea na hawapigi tena kelele za mwizi, nilipoona wananikaribia nikachomoka tena mbio kali......zoezi likarudia lile lile la kupigiwa kelele za mwizi, bahati nzuri natokeza barabarani na gari ya police hii hapa, nikawaelezea tukarudi hadi walipoanza kunikimbiza lakini hakuna mtu, basi wakanisindikiza hadi nyumbani.

1993 Tabora hiyo jamaa yangu mmoja kaja mjini kupokea pesa yake ya mauzo ya tumbaku, akawa na mipango mingi balaa ikiwemo kununua baiskeli mpya, kununua radio kaseti ya Lasonic na kuongeza mke wa tatu..........hakuna hata mpango mmoja uliotimia, usiku wa hyo aliibiwa pesa yote sh 100,000/= na baamedi aliyelala nae gesti (nadhani ndo alikuwa anamfanyia intavyuu kama anafaa kuongezwa kuwa mke wake wa tatu, tangu siku hyo jamaa yangu huyo alishikwa na uchizi akatoweka nyumbani hadi tulipokuja kupata taarifa za kifo chake cha kugongwa na gari.

Juzi juzi tu hapa kuelekea kipindi cha sikukuu za krisimasi na mwaka mpya kundi la vibaka wapatao kama 17 hivi walivamia kwa jirani yangu aliyekuwa kauza kagari kake kamechakaa chakaa kwa sh milioni 6, wale wapuuzi wakataka kuja kuchukua zile pesa kama vile walimuwekeza........kwa mara ya kwanza ndo nilikatumia vizuri ka manati kangu ka kizungu, nilimkongoroa goti mmoja wao na wengine wakakimbia, yule tulimmalizia pale pale kwa kushirikiana na wananchi wenye hasira kali.

2007 kuna majambazi yalivamia mtaa flani wenye maduka mengi, sasa ile tabia ya mlinzi mmoja analinda karibu maduka 40, wakamkamata mzee wa watu wakaenda nae hadi kwenye mojawapo ya maduka anayolinda wakamkazimisha aanze kuvunja, zoezi lilipokamilika wakamlazimisha aanze kusomba vitu anapakia kwenye gari la majambazi.......ile wanamalizia mara paaaaap na mwenye duka akatokeza akamuona yule mzee mlinzi wa duka lake yupo kwenye harakati kupakia vitu kwenye gari ya wale wezi, jamaa akafyatua risasi hewani, wale wezi wakawahi kwenye gari yao ili wakimbie, na yule mzee mlinzi na akaona hapo sio pa kukaa tena, akadandia kwenye gari ya wale wezi akaondoka nao...........!!!!!!!!!!!!!!!!


komando kinjekitile ngwale
Hahahahah hapo kwa uyo mzee mlinzi hapo nimecheka kinyama
 
Hiii kitu ni very interesting, huwa nina matukio mengi, nimepitia. Mengine mission zili fail, nikaumia sipendi kumbuka hizo kumbukumbu. Ila some ambazo was man of the match nazikumbukaga [emoji3]

Nilikuwa Tanga kwa kazi flan hivi, kwa kipindi huko. Nikiwa na wenzangu, tukazoea zle chimbo pasi na kuwa wenyeji kiihiivyo, wenzangu alikuwa mtu wa [emoji482][emoji481], so ilibidi akitaka kujitwika huwa nampa escort yasije mkuta, . Huwa sipigi maji, bt nikienda huko bado naenjoy kama kawaida.

Sasa usiku huo, ndipo uhusiano wa njemba flani na girl wake ulingia dosali

Tulipo ingia katik baa flan, huwa sikai katik kona ambayo mtu atapita mgongon, yaan huwa naweka watu wote mbele yangu kama ikiwezekana. Ingawa sinywi bia lakin huwa naagiza chupa moja au mbili kwa jili kuamshia dude, kama mamb yakiwa meeng na watu weeng
(nadhan unaelewa bia ikipigw chini baada ya kuzungushwa inatoa mlio gani. Hii ni kwa ajili ya kuchanganya adui zako)

Sasa pale, tulipata kampany la binti flan la mboga saba na man wake, walikuwa wagen, kwa stry story, waliemda kule kutafuta ishu za jadi.

Kumbe kuna watu walikuw wanawalia timing kitambo, wao walikuwa na gari ndogo yao, wamepaki nje tu hapo, basi kwa kuwa tunaleleka njia moja, wakasem watupe lift, bana bana, ile tumetoka mchiz akatangulia katik gari akawa anaweka vitu sawa siti ya nyuma ili tupande, sijui kulikuw kuna vitu gan hakutana tuvione soo aliwah kwanza, ili tuna karibu gari, hatuja ingia njema kadhaa hizi hapa, wametuzingila, wemgine wanaifata ndinga, ipo kama mita kumi tokea tulipo.

Wako na silaha za jadi tu, walijua yule demu, ni mtu wa madini, maan alivyo na kule kuna sehem wanachimbaga, so watu wa town huwa wanaend kuyanunua huko kwa wachmbaj wa dogo. Mchiz wake, si akaondoa gari mkuku kuepuka msala, mm partner wangu, yupo bwax, nikikimbia tutaangalianaj, kumbe jembe pombe zilikata, nikasikia yeye ndo anasema, baba tuwa gawanye then kila mtu adili na mbinu, zake nikamjib WORD.

yule binti, akasema usiniache plz, nikiend left nimvuta mkono, nikamwambia usiwe mzito, mwana akaend kulia basi, ikawa mshike mshike.
Jamaa wanasilaha, lakini nilicho wasoma hawana ujuzi nazo, mbwembwe tu, then hawana format ya kushambulia, ishu ni speed and violence, mambo yalikuwa mengi, kuna bwege aliniotea kisu cha mkono, bahat nzuri lile jamaa lilikuja na back up ya wanakijiji. Masela wakasepa, sasa ile mchizi anafika, anaanza kumuuliza demu wake, vip, mama, hujaumia
Demu akamjib, WHEN MEN WERE MEN, WHERE WERE YOU[emoji3][emoji3] NIACHE MWANAUME GANI..



Kuna matukio, mengine ni shida, unakutana na jitu, unalipa vitasa, hata hashtuki, damn.


Sent using Jamii Forums mobile app
Hapo kwa mdada haujamalizia vzr bob

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usiku una mengi, kuna wanadamu wao wamejitolea usiku kama ndio muda wao wa kutafuta chochote kitu,,, binafsi nimewai kukutana na matukio machache ya kukutana na wezi usiku.

Tukio la kwanza, nakumbuka tulikua form six miaka ya nyuma tunatoka kwenye kumbi za starehe tukiwa watatu tunarudi tuliko kua tumepanga uswahilini, njiani tulikutana na wezi wametoka kuiba samani meza, vitanda, na viti walikua wengi kiasi, jamaa walitusimamisha mmoja wao akatupiga mkwara mzito sanaa, nakumbuka walitubebesha meza, rafiki angu mmoja mwenye mwili mkubwa yeye alibebeshwa kabati, tulitembea kama kilomita mbili hivi wakatuachia, yule mwenzetu aliebeba kabati aliumwa mgongo wiki nzima.

Tukio la pili, nikiwa nakatiza mitaa ya sinza, nikakutana na kundi la vibaka wako kama sita hivi, saa sita usiku, ilikua ni ile position unakata kona unakutana na watu hawa hapa, siku sita nikapita kati kati yao maana hakukua na namna nyingine ya kukimbia, nilipigwa kabali ya hatari, huyu kashika mguu huu, mwingine kashika mguu mwingine, walinichukulia simu, waleti na viatu, tukaachana kwa mengi matusi tunatukanana.

Tatu, hii ilinikuta maeneo mapya niliyokua nimehamia, mida ya saa tano usiku nimetoka kunywa mitungi mtaa wa pili, walikuja vijana wawili kwenye boda boda na mapanga yao, mmoja nilimvamia kwa speed ya hatari nilimrukia teke moja akaanguka analia ana kufa, siku laza damu nilikimbia speed ya kufa mtu.

unaweza kushare mawili matatu kama umewai kukumbwa na mswaibu haya, then watu wakajifunza chochote na kuchukua precautions siku za mbeleni.
...Mkuu, una Pepo la kupendwa na Vibaka ![emoji16][emoji16][emoji16]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom