Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16], vipi hao wazee wa kazi kariakoo walikamatwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alikunya wapi acha fix mzee[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku moja kabla ya mwaka mpya nilivamiwa na majambazi/Vibaka sugu home walikua kama watano hivi... Ilikua mida ya saa 8 usiku nipo pekeyangu home.... Walifanikiwa kuvunja grill la nje ile wanataka kuvunja mlango nikashtuka... Mkwara niliopiga walijua tupo 10 ndani.... Nikawaambia mbw* nyie mimi nipo ndani nyie nje mtu aingize shingo yake ndani.... Nimekamata panga huku natetemeka hahahaha asee usiombe ukutwe na hizi mishe...
All in all nilifanikiwa kuomba msaada kwa majirani jamaa wakasepa...
Mpaka sasa huwa nalala kimachale mno hofu bado ipo....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahaha
Sent using Jamii Forums mobile app
 
HII YANGU ITAKUWA KALI NA HATARI ZAIDI......

Ilikuwa ni moshi mwaka 2009 mwezi wa sita mahindi yamekuwa marefu, miti mirefu, migomba mingi kiasi kwamba hata taa za umeme hazimwiliki vizuri na kuna wingu zito sana na GIZA NENE. Mida ya saa mbili usiku nimetoka town nimeshuka kwenye daladala, nikaingia njia ya kuelekea home. Njia hiyo mpaka kufika home ni parefu kidogo, halafu ina giza kuu. Katikati ya njia kuna geti la kuingia nyumba ya jirani, nilipofika pale nikakuta pikipiki mbili na washkaji waliponiona wakashtuka mmoja akaninyooshea bastola akaniambia lala chini. Sasa maana ilikuwa ghafla na tumekaribiana sana na nilikuwa najiamini sana nikamrukia nikashika ile bastola kuielekeza juu zikatoka risasi kama nne kwa haraka sana....... kumbe ndani kuna majambazi mengine manne yanaforce jamaa ayape hela na yameshatoa kipigo cha maana......

Yule jamaa baada ya risasi kuisha kwenye bunduki nikampiga ngumi akadondoka chini, mwenzake akawa anakuja na sime, ile anainyanyua anikate nikawahi kumdaka mkono nikampiga ngumi ya mbavu akaachia sime, nikampiga ngumi ya pili halafu nikawahi ile sime.
NIKAWAAMBIA MKINIFUATA NAWACHINJA, sasa mimi nilidhani walikuwa wananiwinda mimi kumbe jamaa walikuwa wanawasubiri wenzao. Mara nikaona majamaa wanne wameruka ukuta kwa speed ya hatari na wale wawili wakawasha pikipiki haraka sana wanaulizana imekuwaje jamaa akawaambia kuna mwanajeshi hapa tuondoke...... Wakati huo mimi nimeingia kwenye mahindi wakamulika na tochi huku na huku hawakuniona. Wakawasha pikipiki wakaondoka kwa kasi ya ajabu.

NIKABAKI PALE NA ILE SIME HUKU BADO SIELEWI NINI KINAENDELEA NDIYO SASA NDANI YA ILE NYUMBA WAKAANZA KUPIGA YOWE NA MAJIRANI WALIOSIKIA WAKAJA......

nakumbuka kilikuwa ni kitendo kama cha dakika mbili tu.

YULE MZEE ALINIPA LAKI MBILI AKANIAMBIA KAMA SIYO MIMI WANGEMUUA NA WANGEMUIBIA HELA NYINGI SANA.....
Hiyo siku sitaisahau aisee.
 
Ulivyo jiita mnyama nikajua unaunyama Kweli Kama Savimbi ama Idiamiani kumbe paka tu[emoji1]
 
Hahahahah hapo kwa uyo mzee mlinzi hapo nimecheka kinyama
 
Hapo kwa mdada haujamalizia vzr bob

Sent using Jamii Forums mobile app
 
...Mkuu, una Pepo la kupendwa na Vibaka ![emoji16][emoji16][emoji16]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…