NetMaster
JF-Expert Member
- Sep 12, 2022
- 1,454
- 4,925
Asante kwa JF humu tunaongea bila kujuana hata katika vitu ambavyo huwa hatupendi kuviweka wazi kama kuchapiwa maana ni aibu, humu hatujuani inakuwa rahisi kuweka mambo wazi...
Kisa changu
Nilimuaga ex girlfriend wangu kwamba nimepata safari ya kikazi nitakuawa nje ya mji kwa muda flani kuna tajiri anataka nimwekee makabati nyumba anayofanyia finishing anayokaribia kuhamia.
Nilifika huko lakini nilikuta kuna wenzangu wengine kwa hiyo kazi iliisha mapema , niliwahi kurudi nikiwa nimeshalipwa na tajiri kama laki 3 hivi, nilifika kwangu kuweka begi na kisha nikaanza safari ya kwenda kwa ex wangu, nilifika kwake nilimkuta hayupo, nikaanza safari ya kurudi nikaona wacha nipate chakula lodge flani ya karibu.
Wakati nakula wali kuku kwa jeuri ya pesa nilizopata huko kibaruani nikaona kuna gari Rav 4 imekuja pale lodge ikapaki sehemu ambayo naweza kuiona.
Kuna jamaa alishuka akaingia ndani kwenye lodge nadhani alienda kuulizia chumba na kufanya malipo, muda huo nipo kwenye angle ya ku-observe mengi, nikaona jamaa katoka nje karibu na mlango wa kuingia lodge katoa simu mfukoni anaitumia, itakuwa alikuwa anatuma meseji, baada ya sekunde chache kuna binti akashuka kwenye Rav 4 kisha akaanza kumfata jamaa alipo, LA HAULA! Sikuamini macho yangu, aliyeshuka alikuwa ni dem wangu jamani.
Nilipatwa na mshangao kumuona dem wangu japo yeye hakuweza kuniona, kiukweli alikuwa amependeza hiyo siku alienda salon, nikawa siamini amini nachokiona, yaani dem wangu kaingia lodge na hiyo njemba, aaaaahhh!! Maumivu makali mno!
Hata msosi ukageuka mchungu, nililipa na kuondoka hapo hapo, siwezi kuanzisha varanga kwa demu ambaye kwa maamuzi yake kakubali kuliwa.
Nilifika gheto nampigia lakini simu inaita tu, hapa nikawa navuta picha game imeiva, huo moto anaopelekewa huko si wa kitoto, niliumia sana kwakweli.
Nilienda pharmacy ya karibu kununua sleeping pills (vidonge vya usingizi) maana mawazo yalinisonga sana, nilirudi gheto nikagonga vidonge viwili nikajilaza kitandani huku naendelea kuwaza lakini usingizi ukanichukua.
Kesho yake naamka kama kawaida ila daah!! Nikikumbuka kilichotokea jana yaani maumivu tu, nikacheki simu nikaona ex alinipigia kama mara tatu hivi na kuacha meseji kwamba alikuwa kanipigia sipokei, ila muda alionipigia hapo nilicheki ilikuwa ni baada ya masaa mawili na nusu hivi.
Nilimwambia aje gheto, ile kafika akaanza kujifanya kamaindi sikupokea simu alizopiga akaanza ku-act kujifanya alikuwa kapatwa wasiwasi kudhani labda nilipatwa na tatizo, hapohapo akaanza kujifanya anajichekesha kufurahi nimewahi kurudi na kanimisi sana, mimi namchora tu.
Nikaanza kumpiga maswali pale moja kwa moja kwamba jana aliyeshuka nae kwenye Rav 4 ni nani, akaanza kama kujistukia hivi akawa anakazia kwamba alikuwa kwake labda nimemfananisha, nilimnasa kibao taaa!!! Cha nguvu ili ajue nipo serious, akaanza kulia, nilimkazia ajibu swali hayo machozi yake hata ajaze ndoo nahitaji majibu, akawa anaendelea ubishi kusingizia namuonea na kwamba sio yeye, nilimnasa tena vibao vingine viwili vya nguvu zaidi na vilisikika aisee...
Akaanza kukiri kweli ni yeye na kuniomba msamaha kwamba hatarudia, haikuwa nia yake, bla bla bla,,,,, nilifungua mlango nikamwambia its over!, hatuwezi kuendelea ....
Ilikuwa shughuli nyingine kuanza kumtoa, alipiga sana magoti kuniomba msamaha, namuinua asimame yeye anapiga magoti na kunukamata miguu, ilibidi nguvu ya ziada itumike sambamba na vibao vitatu vya zaida, alijifuta futa machozi, nikamtoa mpaka getini nikafunga geti nikarudi chumbani kwangu, uzuri siku hio nilikuwa mpangaji peke yangu niliebaki.
Nilikuwa na maumivu mengi moyoni lakini kwenda kazini na mazoezi kulisaidia kimtindo, sikutaka kujifungia ndani, maumivu yalikuwepo pindi muda wa kulala ukifika nikianza kuwaza nilivyochapiwa, daaah!! yaani nikaanza kuwaza jinsi ex alivyokuwa anapelekewa moto kuna siku nilitoa chozi kama mtoto mdogo.
Hali hiyo ilidumu kwa wiki hivi ila baada ya hapo niliweza kupata nguvu ya ku-move on mdogo mdogo.
Baada ya miezi miwili niliweza kujitosa upya kuanza mahusiano mapya, mahusiano mapya yalinisaidia kwa kiasi kikubwa kupooza maumivu na hatimae nikasahau kabisa.
KISASI:
Kwa sasa huyo jamaa alienichapia ndie aliemuoa ex wangu lakini cha ajabu mpaka leo ex wangu ni kama analazimisha mawasiliano, huwa hapitwi kunitumia meseji za Pasaka njema, Iddi njema, n.k. ila namjua kabisa anachotaka ni ukaribu tu.
Kuna siku nilikutana nae nikampanga twende kwangu alikubali kabisa na nilipanga nimtafune nilipize kisasi kwa huyo jamaa alienichapia na hata nipige picha au video nimtumie ili naye aumie lakini nafsi ilisita, niliahirisha na kumwambia ex lakini ajabu yeye alijaribu kunibembeleza twende akijua kabisa kinachoweza kutokea lakini nilisimamia msimamo wangu nikazuga tutapanga siku nyingine.
Ni kwamba huyu ex muda wowote nikimtaka anaweza kunipa mzigo lakini sioni ambacho nitafaidika nacho, nimekubali yaishe tu maisha yaendelee.