Tukutane hapa wapenda ujasiriamali

Dah hii tam Sana,vp kuusu sendo za kike kwa bei ya jumla na n mitaa ip maarufu San kwa uuzaji wa jumla

Vya kkoo ipo mitaa mingi kuna kwa mchina

Na kuna kituo cha msimbazi polisi mbele si kuna sheli sasa mtaa unaofata, utaona tu wamemwaga viatu nje
Ingia yale maduka ya chini

Kuna yeboyebo nazo zinalipa kweli jumla unakuta 1,300 kwa 1,700 wewe unauza 3,000 kwa 3,500
Hizi zinapatikana upande wa china plaza si kuna kanisa, sasa mitaa miwili inayofatia (kituo cha pili cha mwendokasi) kama unatokea muhimbili

Sendo zingine

Manzese ni zile kama za kimasai jumla inategemea na piece unazochukua kuna za 3000 kwa 4,500 (manzese darajani upande wa kulia kama unatokea ubungo) kuna mafundi kabisa hapo hapo
 
Shu Shukrani sana. Barikiwa
 
Pia jengo la Machinga Complex nyuma wanatengeneza hizo sendo za kimasai. Sijui bei yake kama ni reasonable
 
Wazo zuri..
 
Wapi nawezapata magauni mazuri ya harusi kwa bei ya jumla?
 
Nice
 
Pia jengo la Machinga Complex nyuma wanatengeneza hizo sendo za kimasai. Sijui bei yake kama ni reasonable

Bei zake ukienda straight mwenyewe ndio hizo 3,000/4,000 ikizidi 4,500 ukienda kichwa kichwa unapigwa hadi 5,000
 
Wa mikoani wenyewe baadhi wanafata vitu vya dar
Dada kati ya kule Ilala sokoni na Karume, wapi kuna nguo nzuri za mtumba kwa bei rahisi? na ni nguo gani za kike zinauzika sana kati ya magauni au skin jeans? Asante
 
Dada kati ya kule Ilala sokoni na Karume, wapi kuna nguo nzuri za mtumba kwa bei rahisi? na ni nguo gani za kike zinauzika sana kati ya magauni au skin jeans? Asante

Ilala sokoni saa 10 hadi saa12 alfajiri kila siku wanafungua mabalo ya nguo (jeans magauni nguo mchanganyiko) nguo hadi 1,000/500 nzuri tu


Nguo zinazouzika sana it depends na wateja wako kama watu wa makazini basi magauni sana, jeans pia zinauzika ziwe tu nzuri na bei inayoendana na hali ya nchi[emoji1][emoji1] affordable

Blouse pia, shifon nzuri nzuri ukiwahi asubuhi sana unakuta nguo nzuriii blouse unanunua hata jero na nzuri hatari wewe usiuzie tamaa, uza 5,000 au 3,000 tu
2,500 ni faida kubwa sana hapo ukiuza blouse kumi unafaida ya 25,000 per day (sio kila siku)

Mapochi pia
 
asante sasa dada, ngoja nifanye hii nione na mtaji kama laki 3 hivi wa kutest hali siunafaa?
 
Ilala sokoni

Ukiwahi saa10 alfajir unakuta wanafungua mabalo unachagua unafua fresh tu unapiga pasi vizuriii tena hadi mapya unaweza kupata
Kumbe yanapatikana ya mtumba pia?
Mimi niko mkoani naweza pata mawasiliano ya muhusika yeyote unayemfahamu hapo tafadhali?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…