Sawa lakini sasahivi lugha yetu ya kiswahili imekuwa tajiri hivyo hakukuwa na haja ya wewe kutumia neno "Allergies", badala yake ungetumia neno "Mzio".
Ni neno limekaa safi na kiumaridadi!.
Mimi sidhani kama nina mzio ila kuna siku sikumbuki hata nilikula nini!, Tumbo likaanza mashetani yake!, ghafla tu nikatapika!.. ulikuwa ni mtapiko mmoja tu ila ni ule ambao unakuja haraka yani ni hauwezi kuuzuia hata uwe umekaa sijui na nani ile ni moja kwa moja!, bahati nzuri nilikuwa sehemu nzuri kwa hilo jambo laiti ningekuwa kwenye jumuhiya ya watu walahi sikuhiyo ningeaibika!.
baada ya hapo mwili ukaanza kuwasha miguuni na mikononi!, nusu saa tena vidole vikaanza kuvimba nikajua haya sasa shughuli imeanza!.
ila haikukaa sana ile hali ikaisha sijui ndo ulikuwa ni mzio ama nini!.