Tukutane QuizUp

King Shaat

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2013
Posts
863
Reaction score
835
Habari wakuu! Poleni na majukumu ya kila siku.
Katika games za Android/OS ninazozikubali ni QuizUp. Ni game inayohusisha topics nyingi sana na za aina mbalimbali. Topic yeyote ile inayokuvutia utaikuta QuizUp.

Namna ya kucheza ni rahisi. Chagua topic, halafu chagua mpinzani wako. Round ziko 6 na moja ya Bonus yenye maksi 40. Kila round na swali moja na majibu yake hapo chini, ukipatia jibu kwa haraka zaidi unapata maksi 20 kamili, jinsi unavyozidi kuchelewa kujibu maksi nazo zinapungua (unapewa sekunde 10 kujibu swali).
Kwa round ya kwanza mpaka ya sita ni maksi 20 na bonus round ni maksi 40.

Ni game zuri linalokupatia fursa (pale utakapopata nafasi) ya kuchangamsha akili huku unajifunza kidogo kidogo.

Karibu kule ukipata nafasi, utanikuta kwa jina hili hili la hapa JF.
 
game ni ya bure au ya kulipia.....?........tusichoshane saa hizi.......
 
Nikitaka kucheza na Mtu humu JF nafanyaje? Nataka nikupige KO moja matata.
 
Nikitaka kucheza na Mtu humu JF nafanyaje? Nataka nikupige KO moja matata.
Hahaha, kwanza i'download halafu chagua topic ambayo unahisi/fahamu kuwa unayetaka cheza naye anaifahamu. Mfano, kama mimi naweza cheza topics za Logos, Greek Mythology, General Knowledge, Barcelona (sema kidogo), Name the Job, etc. uta'search tu jina langu halafu utani'challenge kwa hiyo topic. Tukikutana wote online ndo itakuwa mzuka zaidi ili hata ukitaka rematch tunapiga.
 
mbona wananiambia ninunue........natumia Appstore.........
wananitaka nini mimi........?.....
Duh, kwa AppStore nilikuwa sifahamu kama wanaiuza. Developers wanabanaga kiaina inapokuja kwenye iOS app community. Mfano game kama Alto, Playstore ni bure sina uhakika kama AppStore itakuwa Free. Mi ni mtumiaji wa Android. Dah ingekuwa fresh sana ungekuja leta some challenge kule.
 
inatafuna bandle kama instagram
 
inatafuna bandle kama instagram
Hahaha mkuu bundle kuisha litaisha tu hata ukisema uweke kwa ajili ya kusomea emails tu. Na ndio maana nkasema ukipata nafasi.
Umecheza mechi ka ngapi ukaambiwa bundle lako limeisha? Maana juzi kati tu nlikuwa na 100MB na nikacheza mechi zaidi ya 10 bila kuambiwa "kifurushi kimekwisha". Ila ukipata nafasi, karibu mkuu.
 
mi nikicheza sichezi mechi kumi kama wewe
wakati naifuta nilikua naongoza prison break tanzania
 
Hizo ni baadhi ya topics ambazo huwa nacheza mara nyingi. Kuna topic kama hiyo ya Logos, unajaribu kutambua nembo ni ya kampuni gani au taasisi gani. Political Geography. Kwa wapenzi wa Man U naona mtakutana na wenzenu washakamia msimamo hata huku. Vampire Diaries na famous TV series utazikuta.
 
mi nikicheza sichezi mechi kumi kama wewe
wakati naifuta nilikua naongoza prison break tanzania
Mkuu hizo "mechi 10" ni katika kuelezea hoja yako ya bundle kuisha. Asee kumbe ulikuwa mkali (japo sidhani ka ukirudi utakuta bado unaongoza PB) rudisha ushindani mkuu. Mimi ni game ambayo nimekuwa nayo since 2015 na ndo the best All-Time in Greek Mythology (GM) TZ. Nakumbuka niliachaga hivyo hivyo kama ulivyoachaga wewe, nliondoka nkiwa naongoza GM TZ nkiwa na level 28, nlivorudi miezi ka 3 baadae nkakuta kuna jamaa ndo anashikilia na level 35. Baada ya mechi kadhaa nkarudisha namba.
It's fun asee.
 
mi nikicheza sichezi mechi kumi kama wewe
wakati naifuta nilikua naongoza prison break tanzania
Hahaha mkuu nliotoka kukuambia naona ndo reality. Sa ivi PB uko wa 4, and it'll take you some time urudishe namba.
 
Hahaha mkuu nliotoka kukuambia naona ndo reality. Sa ivi PB uko wa 4, and it'll take you some time urudishe namba.
umejuaje mi wanne ??
nina miaka miwili sijaicheza hii game ngoja nijiangalie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…