Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Tukio la mashabiki wa Simba la kuingia na jeneza uwanjani limewakera wanaoitwa Maaskofu na viongozi wa dini na tumeshuhudia matamko kadhaa kutoka kwa Askofu wa Kikatoliki Kilaini na mzee wa mkono wa baunsa Gwajima. Sijaelewa kilichowatoa mafichoni, kama ni ushabiki wao kwa Yanga au ni kwa sababu ya jeneza au labda nifahamishwe kama watu hawa wameingia nchini Tanzania Wiki iliyopita, vinginevyo nitawashangaa.
Tulia Ackson katika harakati zake za kuusaka ubunge wa Mbeya Mjini, baada ya kutumwa na Magufuli alibeba majeneza na misalaba ya kila rangi kama Ishara ya kuizika CHADEMA. Alitembea Mbeya yote bila kificho chochote, mbona Kilaini na Gwajima walinyamaza?
Wakati huyu Tulia akifanya yote haya alikuwa Naibu wa Spika wa Bunge la Tanzania (sasa hivi ni spika kamili). Ni mtu aliyekuwa anajitambua, mbona hawa wacha Mungu hawakuwahi kukemea? Iweje leo mtu msela kama Tundaman akifanya aliyoyafanya Tulia wao wanapambana naye, kulikoni?