Tulia Ackson ana uroho wa Madaraka

Tulia Ackson ana uroho wa Madaraka

Huyu mdada wa hovyo sana,Lkn na yeye huwa anafikiri anajua kiongozi.
Nimegundua Tulia anaogopwa kweli kweli, kama kachmeka si aachwe atashindwa kwa kura kwanini anaogopwa hivi? kila mtu Tulia Tulia aachwe atashindwa kama kachemka
 
Tuna wabunge wasio na sifa za kuwepo Bungeni ndio maana hawawezi kusimama Sheria za Bunge
Waliingizwa kiujanja ujanja
So wanaishi kwa fadhila tu
Hawawezi kumkosoa Tulia Ackson anachofanya
 
Tuna wabunge wasio na sifa za kuwepo Bungeni ndio maana hawawezi kusimama Sheria za Bunge
Waliingizwa kiujanja ujanja
So wanaishi kwa fadhila tu
Hawawezi kumkosoa Tulia Ackson anachofanya
Umeandika ukweli mtupu, we just wasting our time, hata aingie nani hana cha kufanya
 
Nimegundua Tulia anaogopwa kweli kweli, kama kachmeka si aachwe atashindwa kwa kura kwanini anaogopwa hivi? kila mtu Tulia Tulia aachwe atashindwa kama kachemka
Hakuna anayemuogopa
 
Wanaona Ila Hawana Kauli, Hata Kama Sheria Haisemi Lolote Alitakiwa Aachie Kwanza


Wanaogopa kupiga kelele wanadhani ni maagizo kutoka juu lakini hawafurahishwi na Tulia kutojiuzulu
 
Amechukua fomu ya kugombea kiti cha Spika pasipo kujiuzulu U Naibu Spika kwa lengo la kuwa akishindwa aendelee kuwa Naibu Spika, Huu ndio unaoitwa uroho wa madaraka wenyewe.

Anasema, “kwa mujibu wa katiba waliotajwa kutogombea uspika ni Mwaziri na watu wenye madaraka ya umma”, kwani cheo cha Naibu Spika sio madaraka ya umma? vile vile anasema, “hata kama nimechukua fomu si kwamba kiti cha Naibu Spika kiko wazi, hapana”. Ina maana anazuia wengine kugombea U Naibu Spika hadi ajihakikishie ameupata U Spika.

Sawa pamoja na kuwa ni haki yake na sheria haimzuii kufanya hivyo, angeonekana ni mtu mwenye busara na hekima kama angesema, kama ni kuwatumikia wananchi kwa hadhi niliyonayo inatosha sana, lkn kwa kitendo alichofanya machoni pa watu anaonekana ni mtu dhaifu na mwenye tamaa.
ni wachache mno wataokua na busara kuwacha kiti
 
Hapa mnajichanganya.

Tulia amechukua fomu kuomba kupendekezwa na chama chake kugombea uspika. Wabunge ndio wanaochagua spika sio chama. Hata wanachama wa vyama vingine wana nafasi ya kugombea uspika kwa mujibu wa taratibu za vyama vyao.

Kwa hiyo atajiuzulu unaibu baada ya kupitishwa na chama chake kama ikiwa hivyo.

62299F0B-E277-4878-B38B-B7A6E588D681.jpeg
 
Hakuna ubaya kwa mtu yoyote to aim higher, kitu cha muhimu ni kufuata katiba, sheria, taratibu na kanuni.

Huyu ni mwalimu wangu wa sheria pale UDSM, kiukweli kwenye hili, mwalimu wangu amechemsha!. Alipaswa ajiuzulu kwanza u naibu spika ndipo agombee u spika!. Mimi huu nimeuita ubatili

This is not right

Sio haki yake na sheria inazuia, ila wanaopaswa kumzuia Tulia, wamenyamazia!.

Ili mtu atumie busara, kitu cha kwanza ni hiyo busara yanyewe kwanza iwepo kisha ndipo itumike!. Kama hiyo busara yenyewe haipo, kwa mtu kama huyo unategemea nini?.
P

Mayalla, have you really decided to jump on this bandwagon? Deputy speaker doesn’t fit the definition of a civil servant at all. This is very astonishing because you at least know a thing or two about law!
 
Tulia hafai kabisa kuwa Speaker, lakini sio sahihi kusema kwamba ana tamaa ya madaraka kwasababu tu hajajiuzulu unaibu speaker.

Kutaka ajiuzulu kwanza unaibu speaker ndipo agombee kiti cha speaker sio reasonable. Hiyo ni sawa na kutaka kila anayefanya application ya kazi nyingine aiache kwanza kazi aliyonayo. In real life, no one does that!
Hiyo kazi unayoomba kwa Mwajiri mpya huwa unamjulisha Mwajiri wako wa Zamani?
 
Hiyo kazi unayoomba kwa Mwajiri mpya huwa unamjulisha Mwajiri wako wa Zamani?

Kwanini unadhani swali lako ni relevant?

Wapo employers wanaotangaza kazi ambazo zipo open to internal and external candidates. Kwa muktadha huu, Bunge ni classic example. Kiti cha speaker (when vacant) kiko open to internal and external candidates!
 
Back
Top Bottom