Tulia Ackson jimbo lako linapoteza timu mbili Ligi Kuu, unazisaidiaje?

Tulia Ackson jimbo lako linapoteza timu mbili Ligi Kuu, unazisaidiaje?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Tulia Ackson Mbunge wa Mbeya Mjini, Mbeya City FC na Prison ziko kwenye hatari kubwa ya kuporomoka daraja.

Una mikakati gani ya kuzisaidia hizi timu? Tunajua umekuwa unajinasibu kuwa wewe ni shabiki kindakindaki wa Simba. Hatujawahi kuona unatoa amsha amsha kwa timu za jimboni kwako.

Hizi timu zikiteremka sio tu kwamba wana Mbeya tutahuzunika, ila hata wewe itakuathiri kwa namna moja ama nyingine.

Kumbuka ulipita Mbeya kimazabe, wananchi hawakukubali wala hawakuelewi, huu ndio ungekuwa muda wako wa kuwafanyia mambo wapenzi wa kandanda.

Kwanza kwa nafasi yako umeshindwa kuwa approach hata watengeneza pombe wazifadhili timu za jimbo lako?
 
Ndio maana sisi kama IHEFU hatutaki unafiki wa viongozi kwenye team yetu....
Mwaka juzi mbeya city iliponea chupuchupu kushuka Mpaka kuishia kwenye playoff,yeye(TULIA) ndiye aliyekua anawapa mil 5 kwa kila game....baada ya muda siri ikabumbuluka kuwa zile hela alikuwa anawakopesha na walishindwa kulipa na ndio maana kajitoa...

juzi SUGU alikua na kikao na mbeya city,prisons waliposikia wakaanza majungu...
 
Tulia Ackson mbunge wa Mbeya Mjini, Mbeya City FC na Prison ziko kwenye hatari kubwa ya kuporomoka daraja.

Una mikakati gani ya kuzisaidia hizi timu? Tunajua umekuwa unajinasibu kuwa wewe ni shabiki kindakindaki wa Simba. Hatujawahi kuona unatoa amsha amsha kwa timu za jimboni kwako.

Hizi timu zikiteremka sio tu kwamba wana Mbeya tutahuzunika, ila hata wewe itakuathiri kwa namna moja ama nyingine.

Kumbuka ulipita Mbeya kimazabe, wananchi hawakukubali wala hawakuelewi, huu ndio ungekuwa muda wako wa kuwafanyia mambo wapenzi wa kandanda.

Kwanza kwa nafasi yako umeshindwa kuwa approach hata watengeneza pombe wazifadhili timu za jimbo lako?

Bado na Yeye kupoteza Jimbo hapo 2025.
 
Mada nzuri nilikuwa nawaza kuileta kitambo.

Inabidi wana Mbeya wote tujiunge kunusuru timu zetu. Sugu ameonyesha njia ila Tulia na wafanyabiashara wote waunge mkono hizo juhudi, siasa tuweke pembeni. Ni muhimu kushinda mechi zilizobaki hasa zile za nyumbani.

Wasaliti hawatakiwi kuishi.
 
Back
Top Bottom