Uchaguzi 2020 Tulia Trust imefanya mambo makubwa Mbeya kuliko mbunge yeyote yule katika historia ya jiji hilo

Uchaguzi 2020 Tulia Trust imefanya mambo makubwa Mbeya kuliko mbunge yeyote yule katika historia ya jiji hilo

Naunga mkono hoja, na kwa vile hadi jeneza lilishazikwa, aliyepo ni msukule tuu, Tulia atulie tuli, jeneza lifanye mambo, then yeye atapita bila kupingwa.
P
Mwalimu wako huyo wa The Law of Contract muheshimu.....
 
Nami kama mmoja wa watu ambao nimekuwa nikifika jijini Mbeya na Tukuyu kwa vipindi kadhaa, nikiri ni kweli Tulia Trust imekuwa ikifanya kazi nzuri hususani katika miaka hii ya karibuni. Tatizo langu Napata shida sana na andiko lako mtoa hoja; Je, kazi hii nzuri ina uhusiano gani na Mh. Kuhitaji ubunge wa jimbo la Mbeya mjini? Kutokana na andiko lako, Je, ina maana Mh. akikosa Ubunge (Ambao kwa andiko lako ndio kichocheo cha yeye kutoa misaada/mikopo kwa jamii) atasitisha shughuli zake za kuisaidia jamii?

Kwa upande mwingine, kutokana na andiko lako na maelezo ya watu kadhaa humu jukwaani inaelekea bado tulio wengi hatufahamu au tunapotosha kuhusu majukumu ya Mbunge kama Muwakilishi wa eneo lake/watu wake. Kwa uelewa wangu jukumu la mbunge si kuleta maendeleo bali ni kuchochea maendeleo ktk eneo lake. Kwa hiyo inawezekana ata uwepo wa Taasisi kama Tulia Trust, ikawa ni kutokana na kazi nzuri inayofanywa na mbunge katika kufanya mahitaji ya waliompa dhamana yafahamike na wadau wa maendeleo ikiwemo serikali ili waweze kusaidiana na wanajamii husika katika kujiletea maendeleo aidha, kwa kuweka miundombinu Rafiki au katika kuweka mifumo itakayosukuma mbele mchakato wa maendeleo.

Ukimpima Sugu, kama muwakilishi wa wananchi wake wa Mbeya mjini kwa mtazamo wangu jamaa amejitahidi sana. Lakini pia kwa kutumia mfuko wa jimbo bado pia jamaa amejitahidi kwa kushirikiana na wadau wengine kufanya matumizi mazuri ambayo yana tija kwa wana-Mbeya hususani kwenye maendeleo ya elimu. Ubunge pamoja na uwakilishi mimi nauchukulia ni sawa na kazi kama ilivyo kazi nyingine yeyote, hivyo kumjudge mbunge kwa kujenga hotel kwa kutumia pesa zake binafsi (Kipato cha kazi yake ya ubunge) au mkopo sidhani kama tunamtendea haki kwani jukumu la mbunge si kugawana mshahara wake na wananchi wake.
 
Sugu ana street creds lakini huwa kuna muda vijana inabidi walipe kodi za nyumba,wanunue vocha, wakina mama wawe na vikundi vyenye hela na mitaji,watoto waende shule nk nk hapo ndipo anapokuja Tulia kama mbunge sahihi kwa wana Mbeya.

Nimekaa Mbeya kwa muda kidogo nakuona mambo yanavyokwenda kwenye ground kwa kweli suala la Sugu kurudi sio mjadala tena kama Dada Tulia atakuwa mgombea ubunge Mbeya.

Siasa za sasa hivi zinahitaji wanasiasa wanaowainuia wananchi kiuchumi na sio kuwainua kwenye maandamano pekee.

Tulia trust imewatoa vijana mitaani imewapa pikipiki,bajaji,wakina mama wamewezeshwa mitaji na mikopo,madarasa yamejengwa nk
Nyie vibaraka wa uyo kimbau mbau mnamdanganya ili muendeleee kuchota pesa kwenye hiyo organization ya kisiasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sugu ana street creds lakini huwa kuna muda vijana inabidi walipe kodi za nyumba,wanunue vocha, wakina mama wawe na vikundi vyenye hela na mitaji,watoto waende shule nk nk hapo ndipo anapokuja Tulia kama mbunge sahihi kwa wana Mbeya.

Nimekaa Mbeya kwa muda kidogo nakuona mambo yanavyokwenda kwenye ground kwa kweli suala la Sugu kurudi sio mjadala tena kama Dada Tulia atakuwa mgombea ubunge Mbeya.

Siasa za sasa hivi zinahitaji wanasiasa wanaowainuia wananchi kiuchumi na sio kuwainua kwenye maandamano pekee.

Tulia trust imewatoa vijana mitaani imewapa pikipiki,bajaji,wakina mama wamewezeshwa mitaji na mikopo,madarasa yamejengwa nk
huwajui wana Mbeya wewe. wamekula vya Tulia lakini usijeshangaa kuona wanampa ubunge mtu mwingine.

na kutokana na CCM kugawanyika jimboni humo (team Mwanjelwa, team Mwandosya, team Tulia, nk), si ajabu kuona msela Sugu akiendelea kukalia kiti kwa kipindi kingine.
 
Back
Top Bottom