Unaweza ukawa unadunda nao, na unaudundisha kwa wenzako. Haupimwi kwa macho. Na huo utamaduni wa kutokupima mpaka usikie kuumwa ndio hatari kwa huu ugonjwa.
Tuwe serious tuache mzaha!!!
Sent using Jamii Forums mobile app
Sio mzaha ni kueleweshana hapa na kutoana hofu ndugu. Tangu corona kuripotiwa kwa mara ya kwanza nchini, je ni muda gani umepita? Hiyo probation window ya 14days kwa mtu aliyeambukizwa na kama hali ni mbaya kihivyo tunavyoaminishwa, mbona ni zaidi ya hizo siku 14!!
Ni vema tukawa tunaeleweshana haya mambo pasipo kuwekeana hofu kwa sababu hofu nayo ni shida nyingine kubwa sana pengine hata zaidi ya hiyo corona yenyewe. Watu waambiwe tu kuwa ugonjwa upo na unaua na watu wachukue tahadhari nyingi na sio kutoa taarifa za watu kuugua kila siku na kuanza jazana hofu.
Angalia sasa matatizo yaliyosababishwa na hii hofu, watu wengi wataingia kupata shida ya akili tu kwa kufungiwa ndani, uchumi wa mtu mmoja mmoja kuanguka kutokana na kupoteza vipato na taifa zima kukosa mapato kwa kuwa watu hawafanyi kazi za uzalishaji. Ulaya na Marekani huko watu wanaandamana kwa kuwa wameona huu ni ujinga sasa kuwafungia watu ndani wanakosa chakula na fedha halafu corona yenyewe haiishi.
Approach ya kukabiliana na hili tatizo ilikuwa mbaya na watu hawakuelekezwa kiusahihi hatua za kuchukua ili wakabiliane nalo na matokeo yake sasa ugonjwa haujaisha na tumezalisha matatizo mengine lukuki. Nchi zinazotegemea utalii kwa mfano, zimeingia kwenye mdororo mkubwa sana wa kiuchumi kwa sababu ya watu wachache waliojiona wao ni wataalam wakatushauri vibaya kwa interests zao na matokeo yake tumeingia kwenye shida zingine lukuki.
Akili ya binadamu imeumbwa kufanya kazi sana na kwa ufanisi ili kupata suluhu wakati wa changamoto na sio hii ya kutishana na kutiana hofu na kuzifanya akili kudumaa na kulala kabisa.
Amini nakwambia matokeo yote mabaya yatakayokuja baada ya hii corona hayatakuwa yametokana na ugonjwa wenyewe bali ni maamuzi yasiyo sahihi ya kukabiliana na huu ugonjwa.