Kwa LUGHA YA KWENU KOJANI ,,,hivi FALA inamaanisha nini? NYERERE ANA UHUSIANO GANI NA HALI YA INCHI ilivyo SASA?kama ni SUALA LA VIONGOZI KUFUNGWA,,,huyo SHAMTE NDY WAKWANZA? hilo suala LA kufungwa SHAMTE LINAHUSIKA VIPI NA HALI YA UCHUMI WA TANZANIA KWA SASA? Mambo ya MASHEHE WA UAMSHO NYERERE ANAHUSIKA VIPI? NYERERE alikuwa Nov 1999..UAMSHO WAMEKAMATWA MIAKA KUMI BAADAE,,yeye anahusika na nn? VIONGOZI WOTE WANGEKUWA WAZALENDO KAMA NYERERE Leo tusingekuwa hapa TULIPO....WEWE utakuwa UMEAMINISHWA UPUUZI..NYERERE KAACHIA INCHI HII ILIKUWA na VIWANDA VINGI SANA,,,HATA SEKTA YA MADINI alikataa KUINGIA mikataba ya KIPUUZI.,,mpaka sekta ya UVUVI PIA KULIKUWA NA MELI ZA MUUNGANO WA CHINA NA TANZANIA,,,MABAHARIA TUNAPANDA NDONGA...WAKATI NYERERE ANAACHIA INCHI DOLA MOJA ILIKUWA SHULING NGAPI?ANZIA HAPO KWANZA...Leo hakuna hata kimoja kilichopo KWENYE USO WA RAMANI YA TANZANIA.... HIVI MZAZI KAACHA MALI,,watoto WAMEUZA KILA KITU,,,na KURUDI KWENYE ULOFA,,wa kumlaumu ni MZAZI ALIYEKUACHIA MALI? au watoto waliotumia kwa FUJO?USITUKANE WAZEE WEWE KIJANA....Mimi nimesoma enzi ya NYERERE TUKIKUNYWA UJI WA BLUGA SHULENI..NA KUPEWA MADAFTARI...leo HUO UJI UNAULIPIA ,tena sio uji wa maziwa,,ni chumvi na dona,, UNAMTUKANIA NN MZEE WA WATU? mwache apumziike kama UKIVYOWAACHA WAZEE WAKO CHOKOCHO...kama neno FALA SIO TUSI,,BASI NA WEWE PIA FALA...
Sent using
Jamii Forums mobile app
Kweli wewe hata huyo nyerere humjui , utakuwa ni mtoto uliyezaliwa kwa mbio za mwenge.
Yaani Shamte yuko nchi nyengine unaivamia na kuwafunga viongozi wake kwenye nchi yako wewe unasema sio wa kwanza , hapo tukuelewe vipi ???
Biblia inasema kwa matunda yao utawatambua
Nyerere ndiye aliyepanda huu mti wa CCM na sasa ndio tunavuna haya matunda yake , unalalamika kitu gani ??
Ukinywa uji upi na wakati wake hata chumvi tukibadilisha na dhahabu , Mbeya. Viatu tukivaa mapira ya gari , Sigara watu wakiuza pafu moja mtu mmoja.
Chakula kwa kadi tena unapewa dona la njano tukiita , YANGA tena unga wenyewe ulitoka Marekani , mahindi wanayolishia farasi huko kwao.
Fala wako ni balaa alikuwa akilitumikia kanisa kinoma.
Hiii ni article ya mwaka 1993 kabla huyo Laanatullahi hajafa
MJADALA unaendelea nchini kote juu ya kuundwa kwa serikali ya Tanganyika na muundo wa Muungano wa Zanzibar na Tanganyika. Inavyoelekea yapo matatizo, dosari na sababu za msingi zilizopelekea wananchi kuhoji muundo wa sasa wa Muungano na kuleta hoja ya kuundwa kwa serikali ya Tanganyika ni yenye kuundwa kama si leo kesho.
Lakini wapo pia wanaopinga kabisa kuundwa kwa serikali ya Tanganyika.
Aliyejitokeza kwa nguvu na kwa ukali hadharani kupinga hoja hiyo ni Mwalimu Julius Nyerere, katika kupinga hoja hiyo Mwalimu anatoa hoja zifuatazo:
Hoja ya kuundwa kwa serikali ya Tanganyika imeletwa kwa kuwachoka Wazanzibari na Waislamu. Ufupi wa maneno Mwalimu Nyerere anadai hoja ya kuundwa Serikali ya Tanganyika imetokana na chuki za kidini - Wakristo kuwachukia Waislamu.
Hoja haipo katika sera za CCM na taratibu zimekosewa.
Kuundwa kwa serikali ya Tanganyika kutavunja Muungano na kutavunja Tanganyika pia.
Ukizingatia sifa nyingi ambazo Nyerere alijilimbikizia wakati wa utawala wake na sasa si vigumu kuelewa kwa nini anapinga kuundwa kwa serikali ya Tanganyika. Mambo yake yote aliyoyaanzisha kwa vishindo huku akisifiwa kuwa zidumu fikra zake, yamekuwa yakiporomoka moja baada ya jingine huku mwenyewe akiona. Lililosalia ni Muungano; nao ukiporomoka haitaleta picha nzuri katika historia yake katika siasa.
Lakini lililo gumu kueleweka ni hatua ya Mwalimu Nyerere kutumia Turufu ya udini kuwagawa Wabunge; wana-CCM na Wa-Tanzania kwa ujumla katika suala hili. Kauli hiyo ingesemwa na Muislamu ingepewa mtizamo tofauti na labda isingeeleweka hasa miongoni mwa Waislamu. Lakini kusemwa na Mwalimu Nyerere kunaleta mkanganyiko zaidi. Kwanini; (udini ulikuwa umejengeka). Hali hiyo ilipelekea Masheikh kumlalamikia lakini akawanyamazisha kwa kuwashutumu kuwa wanachanganya dini na siasa. Miongoni mwa Masheikh hao wapo waliofukuzwa nchini; waliowekwa kizuizini, waliofukuzwa katika chama na kadhalika.
Sheikh Hassan bin Amir katika waraka wake kwa Waislamu mwaka 1963 aliutaja udini uliokuwa unajengwa Tanzania kwa kutoa mifano ifuatayo:
Kuingizwa nchini Tanganyika mara tu baada ya uhuru vimedali vidogo vidogo vyenye picha ya bendera ya Tanganyika usoni na katikati ya bendera hiyo amesimama Mama Maria na mtoto mchanga na nyuma yake maandiko '
MARIA MTAKATIFU ULINDE UHURU WA TANGANYIKA'.
Gazeti la
KIONGOZI la tarehe 1/8/1963 lilimuonyesha Bwana George Kahama akipewa cheo cha dini na Pope kwa
kuwakilisha serikali ya Tanganyika katika mkutano wa Makanisa ya Roma.
Mwaka huo huo wa 1963, mnamo tarehe 24 mwezi wa nane, Baraza Kuu la Makanisa ya Kilutheri Tanganyika lilitoa matangazo kuwa Uhuru wa Tanganyika ulikuwa '
Chini ya Msalaba'.
Tarehe 17/5/1963 Makanisa yalifanyia mkutano wao ndani ya Bunge.
Alipokufa Pope Yohana wa 23 bendera ya taifa ilipepea nusu mlingoti nchi nzima!
Kabla ya kifo chake Pope Yohana wa 23 alimletea Mheshimiwa Nyerere barua ya pongezi kwa kuupanua Ukristo- barua ambayo ilitiwa saini na Pope mwenyewe. Barua hiyo imetangazwa kwenye gazeti la
Tanganyika Standard.
Gazeti la
Reporter la Kenya la tarehe 20/6/1963 lilitangaza katika ukurasa wake wa mbele: "
KUIBADILI AFRIKA YA MASHARIKI KUWA KATIKA DINI YA ROMANI CATHOLIC". Ndani ya gazeti hilo ukurasa wa 18 liliwataja waliopewa dhamana ya kufanikisha jambo hilo kuwa ni: Uganda - Kiwanuka, Kenya - Mboya na Tanganyika Mheshimiwa Nyerere.