Gai da seboga
JF-Expert Member
- Apr 19, 2019
- 515
- 1,015
Katika Mei Mosi ya mwaka huu 2024, Makamu wa Raisi wakati akihutubia akimwakilisha Raisi alisema suala la nyongeza ya mshahara tusubirie Jambo kutoka kwa Raisi mwenyewe.
Tunavyofahamu nyongeza ya mshahara hubadilika katika mshahara wa Mwezi July, sasa mpka tarehe ya leo 14 July hakuna tamko lolote la Mheshimiwa Raisi juu ya Nyongeza ya mshahara, hii inamaansha nini kuwa watumishi ndio tumechinjiwa Baharini?? Au ndio anataka aongeze kimya kimya?
Kiuhalisia hali za kimaisha kwa watumishi wa umma ni mbaya sana, yani maisha yamepanda gharama mara dufu lakini kimshahara ni kile kile hakijabadilika, kwakweli watumishi wamekataa tamaa sana hata morali ya kazi haipo watu wanaenda makazini tu lakini hawana shauku ya kuchapa kazi kweli kweli.
Mheshimiwa Raisi kundi la watumishi wa umma ni kundi muhimu sana kukufanya ukarudi kwenye Ramani zako za Kisiasa 2025, nadhan unajua namna mnavowatumia walimu na askari katika kutimiza ndoto zenu za kuwa madarakani, hivo kuwatelekeza watumishi wa umma kwa kutowaongezea ata mia ni ukatili mkubwa sana, na mjue mnaweka vinyongo kwenye nyoyo za watumishi wa umma siku yakijakuibuka ya kwa majirani Kenya msije mkamtafuta mchawi.