Tuliambiwa tuseme "Dawa ya mboga " tulipo tumwa chumvi usiku

BARDIZBAH

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2017
Posts
5,259
Reaction score
10,078
Habari wana jukwaa la Histori.

Niende moja kwa moja kwenye mada tajwa hapo juu. Hapo juzi juzi miaka ya nyuma kidogo wazazi , walezi na wakubwa wetu walikuwa wakitusisitizia sana pindi walipo kuwa wakitutuma chumvi dukani usiku ya kwamba tusiseme chumvi ila tusema "DAWA YA MBOGA" .

Kulikuwa na ulazima gani katika hili?
 
Dah mimi nlikuwa nikitumwa chumvi kwa neighbor naambiwa niseme naomba dawa ya mboga... Dah long time sana yaani
Vip hukujua kwanini mkuu?? maana me nilimuuliza sana Mama lakini hakuniambia kitu
 
Ni dawa ya jiko, najua mtoa mada amesahau kidogo maana ni long time sana.
Sababu niliambiwa ni kumchanganya mwanga ili asije akaiharibu na hatimae akaharibu mboga. Kumbuka hilo neno lilitumika usiku ambapo ndo mida ya wanga kupiga misele.
Mwanga akiharibu mboga lazima ichache . So hiyo ilikuwa ni kuwapiga chenga wanga.

Swali: Je wanga wenyewe walikuwa hawalifahamu hilo jina la dawa ya jiko?
 
hahahaha..walisema usiku hutakiwi kusema chumvi...ila sema dawa ya jiko....kuna siku nikasema nitest mitambo..nikatia chumvi jikoni.....duh nikasikia tu milio ya risasi,mabomu ,makombora n.k...then moto ukazima kama mshumaa

Ilikuwa DAWA YA JIKO ya mawe?
 
Habari wana jukwaa la Histori.

Niende moja kwa moja kwenye mada tajwa hapo juu. Hapo juzi juzi miaka ya nyuma kidogo wazazi , walezi na wakubwa wetu walikuwa wakitusisitizia sana pindi walipo kuwa wakitutuma chumvi dukani usiku ya kwamba tusiseme chumvi ila tusema "DAWA YA MBOGA" .

Kulikuwa na ulazima gani katika hili?
Ni imani tuu na chumvi Ina nguvu sana kiimani kwaiyo iliitwa dawa ya mboga usiku ili kuelezea kuwa ni kwa matumizi ya mboga na sio yakiimani maana chumvi ingewezatumika kujilinda dhidi ya wachawi sasa mwenye duka na waliodukani huwezijua mchawi nani sisi tukiwa wadogo bundi akilia tulirusha jikoni na kuinenea shindwa shindwa na bundi aliondoka
 
Logical answer.

Kwa namna hii ndo maana mamaza walikaza kutuambia sababu.
 
Ndivyo ilivyokua niliwahi kudadisi nikaambiwa wachawi wanapenda kujaribu watu ili wajue nguvu zao sasa kwa matumizi ya chumvi ni wazi kuna namma watu wanaelewa namma yakujilinda/kujizindika
 
Ni dawa ya jiko, najua mtoa mada amesahau kidogo maana ni long time sana.
Sababu niliambiwa ni kumchanganya mwanga ili asije akaiharibu na hatimae akaharibu mboga. Kumbuka hilo neno lilitumika usiku ambapo ndo mida ya wanga kupiga misele.
Mwanga akiharibu mboga lazima ichache . So hiyo ilikuwa ni kuwapiga chenga wanga.

Swali: Je wanga wenyewe walikuwa hawalifahamu hilo jina la dawa ya jiko?
Anhaa!! Dah wazee wetu walikuwa na mambo mengi aise.
 
Back
Top Bottom