Tulichomfanya yule mchawi hatakuja kusahau kamwe

Tulichomfanya yule mchawi hatakuja kusahau kamwe

Tulichomfanya Yule Mchawi hatokuja kusahau kamwe! - 25.

Baada ya Headmaster kutoka kuwasindikiza wageni,tuliamua kukaa kikao cha kifamilia na kuzungumza mambo kadhaa yaliyotuweka sawa.Sasa kila mtu alielekea chumbani kulala,baba mdogo na mkewe waliingia chumbani kwao,mimi na Ema pia tuliingia chumbani kwetu kulala.

Siku hiyo mle chumbani hakuna aliyepata usingizi kabisa,kabla ya kulala nakumbuka tulipakaa usoni dawa aliyokuwa ametupatia mama yake Monica,pia tukashikiria na zile hirizi mkononi kama alivyokuwa ameagiza tufanye!.Kadri muda ulivyokuwa ukisonga tuliona kimya,mimi nilianza kupitiwa na usingizi maana nilikuwa nimechoka sana!,kumbe wakati mimi napitiwa na usingizi,Ema yeye alikuwa macho kabisa na jamaa alikuwa na shauku ya kuona ni kitu gani kingetokea!.

Sasa ilipofika mida ya saa 8 usiku,nilishitushwa na Ema akiniamsha!.

Ema "Umesikia hicho kishindo?".

Mimi "Hapana,kishindo cha kitu gani?"

Ema "Kutakuwa na kitu nadhani!"

Ema alikuwa akiniambia kwa sauti ndogo kabisa na yenye uoga ndani yake!.

Mimi "Nyamaza"

Niliamka kitandani nikaenda kuwasha taa,nilifahamu kabisa kile kishindo Ema alichosikia hakikuwa cha kawaida na uenda wale jamaa wakawa wamekuja kama kawaida yao,kiukweli mimi kwa upande wangu sikuwa kabisa na hofu kwasababu kwa siku chache nilikuwa nimeshazoea yale mazingira ya kuwaona wachwawi laivu!.Nilimwambia na kumbusha Ema ya kwamba chochote atakachokiona asipige kelele wala kushituka!.

Haukupita muda,mara ghafla wakaonekana watu watatu wakiwa wamesimama mle chumbani huki wakiwa uchi kama walivyozaliwa,watu wale safari hii walikuja wawili wanaume na mmoja akiwa mwanamke!.Niliwaangalia kwa kuibia kama vile sielewi chochote!,Ema alikuwa akitetemeka sana na nilimpatia ishara ya kwamba atulie kabisa!.Basi nadhani yule mwanamke alihisi jambo maana niliona anamsogelea Ema akawa kama anamtisha aone kama amemuona,sasa alipoendelea kumtisha Ema nikaona anaweza kupiga kelele,nikaanza kumpigisha Ema stori ili kupotezea ile hali!.

Mimi "Mwanangu wewe piga kimya kabisa wala usimfanye chochote yule demu"

Ema "Yule demu mwanangu anazingua kinoma"

Mimi "Halafu Headmaster alisema ukamuamshe aandae yale masomo"

Ema "Halafu kweli umenikumbusha,ngoja nikamuamshe!"

Sasa wakati tunaongea yule mwanamke alirudi kwa wenzie na wakaendelea kushangaa shangaa,tulichokifanya na Ema pale kwa ule muda mfupi ni hakika walidhani hatuwaoni kumbe lengo lilikuwa ni kumuondolea Ema uoga na kuwapoteza maboya!.
Ema aliamka akatoka kwenda kumgongea Headmaster chumbani kwake ili aje ajionee!,sasa wakati Ema ameondoka,nilianza kujipigisha mruzi wa uongo na kweli ili kuikabili ile hali kwasababu ilikuwa inatisha si kitoto!..

Headmaster "Umughaka tacho omahe"

Baba alipotoka nje aliniita kwa kilugha nikawa nimetoka nje,sasa alianza kutueleza ya kwamba tusishituke na tuendelee kuwa watulivu,alitwambia Ema achukue madaftari tuelekee wote sebuleni ili iwe rahisi kuwakabili,mimi nilimwambia wao wakae sebuleni na mimi nirudi chumbani kukaa karibu na kibuyu kwa kazi maalumu!.
Basi wale watu wakawa wamepotea ghafla mle chumbani!,nilitoka nje kwenda kumwambia Headmaster.

Headmaster "Ngoja tusubiri,yawezekana wakawa wameshituka"

Mimi "Lazima warudi"

Headmaster "Halafu mbona yule mzee hayupo?"

Mimi "Uenda leo kawaagiza hawa"

Wakati tukiwa tunaendelea kuongea pale,Maza mdogo akamwambia Headmaster kwa kikurya kwamba,wale watu wako kule chumbani kwake na anawaona,Headmaster akamwambia atulie na asipige kelele!.Sasa tukiwa tunaendelea kuongea pale sebuleni huku Headmaster akijifanya kumpigisha Ema pindi,tukasikia kishindo kikubwa tena pale uani!.

Haukupita muda akawa ametokea yule mzee makono akiwa na usinga mkononi huku akiwa uchi kama wenzie!,akaja mpaka pale sebuleni huku tukiendelea kumpimia tu!,aliendelea kuangaza huku na huko na hatimaye akawa ameingia mle chumbani kwa Headmaster.Basi baada ya kuingia chumba cha Headmaster,Headmaster aliinuka kwa ghadhabu huku akisema "Lero n'uramanye uwe tombanyoko" (Leo utanitambua).

Sasa Headmaster alipoingia chumbani alijifanya kuongea na mkewe huku wakiwatazama,sasa nadhani mzee makono aliwaambia wale watu waende wakawalete watu wa kwenda kulima ili wakifika watuunganishe na sisi tuondoke!,wale watu watatu walitoweka wakamuacha mzee makono mle chumbani akitaka kufanya mambo yake ili amchukue Headmaster kama kawaida aje atuunganishe na sisi tuelekee kwenye kilimo cha usiku kisichokuwa na tija!.

Wale watu walipotoweka tu na mzee makono kubaki mwenyewe,Headmaster alichukua kile kibuyu alichopewa na mama yake Monica akakifungua,alipokifungua tu!,yule mzee akaanza kucheza kwa kuzunguka mle chumbani kama mwendawazimu!.Headmaster alituita tukaingia kumtazama,yaani kuna muda nilianza kumuonea huruma maana alikuwa kama amepagawa kwa kushikwa ugoni.

Kadiri muda ulivyokuwa ukienda,wale watu waliotumwa na mzee makono hawakurudi kabisa na nadhani watakuwa walishituka mapema!.Ile hali ilifanya maza mdogo kutoka kule chumbani akabaki mzee makono akizunguka chumba kizima kama mwendawazimu.Usiku huko hakuna mtu aliyepata usingizi kabisa,tumekuja kushangaa imefika saa 11 alfajiri bila kujua!.
Sasa ilipofika saa 12 asubuhi,Mama yake Monica alikuja akiwa na wale kina mama,alihuzunika sana kwanini tuliamua kuwaachia wale watu watatu wakaondoka!.

Mama Monica "Mwalimu nilikwambia,nadhani sasa unaniamini"

Headmaster "Sikuzote Msukuma nakuamini,si leo tu!".

Mama Monica "Kwanini mmewaachia wale washenzi?"

Headmaster "Wameondoka wenyewe"

Mama Monica "Nilikwambia wakifika tu,ungefungua kibuyu"

Headmaster "Nilipoingia chumbani kufungua kibuyu wakawa wameondoka akabaki mzee lameki"

Mama Monica "watasimuliana,hakuna kilichoharibika"

Aliendelea "Haya sema,unataka tumfanye nini huyu mzee"

Headmaster "Nadhani kama kuna uwezo muondolee uwezo wake asije akaponyoka halafu mengine utaniachia mimi"

Mama Monica "Huyu ameshakwisha,hapa hawezi kukuponyoka kamwe"

Aliendelea "Mimi namshughurikia halafu nakuachia wewe utajua cha kumfanya".

Basi mama yake Monica alimsogelea yule mzee akachukua ule usinga kisha akamvua shanga alizokuwa amejivika kuanzia begani kuteremkia kiunoni!,baada ya hapo kuna dawa alimpatia Headmaster akamwambia kukishapambazuka vizuri atampaka ile dawa na kisha atamuondoa mle ndani!.Mama yake Monica na wale kina mama waliondoka wakawa wamemuacha mzee makono humo ndani akizinguka kama mwehu!.

Kulipopambazuka,Headmaster alielekea kwa mwenyekiti wa kijiji na kutaka yowe ipigwe karibia kijiji kizima ili wananzengo wahalifiwe ya kwamba kulikuwa kuna tukio kubwa la kushangaza!,Basi yowe ilipigwa na watu wakawa wanakuja pale nyumbani huku wengine mikoni wakiwa wameshika mapanga na mafimbo!.Haukupita muda mrefu watu wakawa wamejazana pale nyumbani huku wengine wakichungulia dirishani wakishangaa lile tukio!.

Ilipofika mida ya saa 3 Asubuhi baada ya watu kujazana pale nyumbani,Headmaster alifanya kama alivyoambiwa afanye na mama yake Monica,baada ya kupakwa dawa yule mzee alikurupuka akawa anashangaa sana!,alikuwa akizunguka kitafuta usinga wake lakini hakuuona,ndipo Headmaster aliamrishwa na wananzengo ya kwamba amtoe yule mzee nje ya nyumba ili akapambane na viboko vilivyokosa huruma!.

Yule mwenyekiti aliamuru yule mzee avishwe nguo hadi kwenye ofisi ya serikali ya kijiji lakini wananzengo wakagoma,walisema inapaswa atembezwe kijiji kizima huku akila mboko na inapaswa siku hiyo hiyo ahame kijiji!.

Basi nakumbuka Headmaster alimuagiza Ema akalete viboko ili aanze nae mle ndani kwasababu alikuwa akimtafuta sana,viboko vilipoletwa kiukweli yule mzee alichezea kiasi kwamba sikutaka hata kuangalia,viboko vilipozidi aliamua kutoka ndani spidi akikimbilia nje,kufika nje wananzengo wakamdaka nako wakaanza kumsulubisha!.
Alitembezwa kijiji kizima huku akiwa uchi kama alivyozaliwa,kiukweli lilikuwa ni tukio la aibu mno!,sasa walipomfikisha kwake wananzengo hawakutaka mjadala,walimwambia avae nguo kisha atoke,alipotoka waliwasha moto nyumba yake na kila kitu kiliteketea kwa moto!.

Baada ya pale alirudishwa serikali ya kijiji na kutakiwa apotee kwenye kile kijiji ndani ya masaa 2!,hakutakiwa kubaki pale na wananzengo walimwambia watamuua endapo angebaki kwa siku hiyo!.

Lile tukio lilivuta hisia kubwa sana pale kijijini na kiukweli lilimpatia Headmaster ujiko na heshima sana ingawaje mimi ndiye niliyepambana sana mpaka kufikia ile hali.Headmaster aliogopeka sana tangu siku ile lile tukio litokee na hakukuwahi tena kuwa na mambo ya ajabu pale nyumbani.

Headmaster kwa baadae alihama ile shule na kuhamia huko Biharamulo ambako amejenga na anaishi hadi leo,mimi niliondoka na kurudi nyumbani kisha kuelekea shuleni Advance!.

Ema yupo hapo Shinyanga anauza duka la vipuri vya magari,amejenga na anaishi hapo hapo shinyanga.

Monica kuna wakati niliambiwa yupo Mwanza ila sijajua ni Mwanza sehemu gani!,kuna mtu nilikutana nae wa pale kijijini akawa ameniambia hivyo,kwasababu baada ya mimi kuondoka pale kijijini sikurudi tena hivyo tukawa tumepotezana na mpenzi wangu huyo!.

Mimi kwasasa nipo Dar es salaam napambana na maisha ya kukimbizana!,nina kiboda boda changu japo kimekwisha lakini tunapambana na maisha!.Kijiwe changu huwa ni hapo Bunju ndugu zangu!.

MWISHO.
Dah bro heshima kwako mkuu
 
Mkuu Armani William kuhusu kuondoka na dawa HAPANA,baada ya kumkamatisha yule mzee makono,nilikaa pale kijijini kwa muda kidogo kisha nikaondoka zangu,ingawaje kuna dawa baadhi nazifahamu,na kuhusu kuwaoma wachawi siwezi tena kuwaona kwasababu sina hizo dawa!.

Monica sijajua kwasasa anafanya ishu gani Mwanza,nimepanga siku moja niibuke kule kijijini nina amini nikienda mpaka pale kwao kama kutakuwa na watu watanipatia namba yake ya simu.
Monica hakufa?
 
Endeleea.....

Basi bhana baada ya kuchukua ile miwa kwa Mzee Masumbuko kama kawaida yangu nikawa naelekea senta,kufika pale nikaiweka ile miwa na kuanza kukata kata zile pingili za miwa..aisee hakika siku hiyo ndo niliamini kua Mungu sio Mwigulu Nvchemba niliuza sana ile miwa watu wakawa wanaulizia hadi bei ya lile panga nililoazima kwa yule mama nikawa nawaambia haliuzwi[emoji3064]

Basi bhana nakumbuka siku hiyo miwa yote iliisha ndani ya lisaa limoja na nikarudisha panga kwa yule mama ili nirudi nyumbani,nakumbuka ilikua mida ya saa tatu asubuhi[emoji1]..nikapita njia ile ile ninayokutanaga na Mzee Makono basi bhana kama kawaida yangu kua nikitembea naangalia chini kama ngiri huku nikiwa na mawazo ya kumkosa mwise,nikakumbuka pia kua sikuiona timu ya yangu ya Arsenal kwa kipindi kirefu ukijumlisha na mauza uza niliyokua nakutana nayo nikabaki nasonya tu..

lakini ghafla nikiwa karibu na lile eneo lenye miembe miwili karibu na njia ya kuelekea nyumbani nikakuta watu watano wakiwa wamelala chini wakiwa kama walivyozaliwa,basi bwana kutokana na uzoefu,ukomavu na ubobevu wa masuala yale ya kutisha sikuogopa hata kidogo,nikawasogelea wale watu na hapo nikawa nimewatambua alikua ni Mzee Makono,Mama Mkwe,Monica na wale Mama zake wadogo wawili.

Nikiwa katika bumbuwazi ghafla nikashtushwa na sauti ya mwanamke akicheka ambayo niliitambua kua ni ya maza mdogo,kupepesa macho huku na huko nikamuona juu ya muembe akiwa katika ungo unaoelea angani,kipindi cha nyuma nilikua siamini hizi stori za watu kupaa na ungo angani kama nilivyokua namuona mama mdogo[emoji2297]

Basi bhana nikamuona mama mdogo akirusha kitu mithili ya moto na kile kitu kilivyonikaribia tu kikadunda kwa kasi ya ajabu kumrudia maza mdogo ndipo nikakumbuka ile kauli monica kua nina mizimu mikali sana[emoji1],kilikua ni kitendo cha sekunde moja tu wale watu wote wakapotea nikabaki nikishangaa pale kwenye ile miembe....fasta nikaanza safari ya kurudi nyumbani na kushangazwa na umati wa watu uliojaa pale nyumbani..Aisee nilivyofika sikuamini nilimkuta maza mdogo akiwa pale amedondoka na ule ungo akiwa kama alivyozaliwa.Kumbe bhana mama mdogo ndo kiongozi wa wale wachawi wote pale kijijini na baada ya Headmaster kusema atawakomesha wale wachawi mama mdogo alienda kuwaelekeza wale wachawi waache michezo yao lakini walimkatalia kwa kua walitaka mashamba yao yamalizwe ndipo ugomvi mkubwa ukazuka mpaka kuwaua wale wachawi wenzake pamoja na mpenzi wangu Monica na washirika wake pale miembeni[emoji24].

Aisee nilikua nina hasira sana ila sikutaka kuionesha mbele ya watu wale waliojaa pale,nikaingia ndani moja kwa moja nikamkuta emma kitandani akiwa amekauka (kumbe na alikua mshirikina ndiyo maana hata mambo mengi yaliyokua yakimtokea au kututokea pamoja alikua anayaficha) basi bhana nikatoka na shuka na kumfunika Maza mdogo na kuingia nae ndani huku watu wakiendelea kupungua kadri muda ulivyozidi kwenda.

Mida ya saa 11 jioni Headmaster alirudi akiwa na mganga mwingine lakini akiwa amesikia stori nyingi huko vijiji vya jirani kwa kile kilichotokea pale shuleni na kijijini kwa ujumla hakika yalikua ni maafa walikufa wachawi wengi sana karibia watu 100 katika kile kijiji walikua ni wachawi

alivyofika nilimuelezea yote yaliyotokea mchana akiwa na yule mganga akasikitika sana na kuniomba msamaha kwa yote aliyonifanyia,nakumbuka yule mganga akautoa ule mwili wa Emma na katika mazingira ya kushangaza akapotea ghafla tukabaki mimi,Headmester na yule mganga....Bamdogo akaniuliza tumfanyie nini huyu maza mdogo?? hakika nilikua nina uchungu sana kwanza wa kudharauliwa na watu wengi,kumkosa mtoto Mwise ambaye aliuteka sana moyo wangu,lakini pia kuondokewa na mpenzi wangu Monica ambaye alikua ananipa ndipo nilipomwambia bamdogo tumpige collabo (mtungo) mama mdogo

Basi bhana shughuli ilianza mida ya saa moja hakika nilimchakata sana maza mdogo kwa hasira sana nikawa nabenua kiuno chake na kupiga lile ta-call alilonisingia kua nilimshika basi bhana nilienda goli kama tano bila kupumzika na nakumbuka mbili nilipiga kwenye mbunye na tatu nikapiga kule alipokua anajichezea lulu diva na kuzimwagiemo[emoji23] then nikampisha na mganga nae afanye yake..

ilikua ni aibu n uchafu mwingi sana kwa maza mdogo na wiki ile ile alikunywa ile lotion yote aliyonituma kipindi kile alimeza na mchanganyiko wa dawa flan za vidonge ambao sikuutambua ila vilikua na rangi tofauti tofauti na huo ndo ulikua mwisho wa maza mdogo gwiji la wachawi aliyeuficha ushirikina wake kwa mgongo wa ufundi cherehani[emoji1]

Basi maisha yakaendelea kama zamani pale kwa headmaster nikiwa mimi na bamdogo tu nikawa nakula ile mikuku n mimaziwa mpaka nikairudisha ile nuru yangu kama zamani,na furaha yangu ilizidi zaidi baada ya kumpata mtoto mwise tena nilimkuta akiwa sild kabisa[emoji23][emoji119]...

MWISHO[emoji120]
Watu ni Vichaa kweli[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwa mara ya kwanza Hadithi inasimuliwa hadi kufikia Tamati, wengi huja na Visa vyao lakini huishia kutoikamlisha.

Hongera sana Mkuu UMUGHAKA Kuna visa hapo umesimulia umefanya nikumbuke mbali sana. Kweli tunaishi Kwa Imani [emoji120][emoji120]
Kasome kisa Cha Jack Daniel jamaa alitema story yake nzuri bila shida story hiyo Ni Moja ya story nilioipenda Sana hapa jf pmj na jamaa aliyetoa mkasa wa bomu za mbagala hzo story Ni Kali haswa
 
Tulichomfanya Yule Mchawi hatokuja kusahau kamwe! - 24.

Baada ya Maza mdogo kurudi,ulikuwa ukiwaangalia yeye na Headmaster ilionekana kuhuzunika sana na sikuelewa sababu ilikuwa ni nini!,nimewazoea mara zote tukiwa pale sebuleni eidha tukila chakula au tukiwa tumekaa,mara zote mazungumzo yenye utani na ucheshi mwingi huwa yakishika kasi,safari hii imekuwa tofauti kabisa!.

Headmaster "Ulisema ulikuwa na jambo la kutuambia,ni jambo gani hilo bhana"

Mimi " Ni jambo la kawaida tu Baba"

Mimi "Baba mimi nina rafiki yangu wa kike anaitwa Monica,na niseme tu ukweli baba ile siku uliyoniadhibu ni kweli nili lala kwao".

Mimi "Sasa nimeamua Kuwaita ili niwashirikishe jambo"

Mimi " Yule binti kiukweli kwao ni wataalamu wakusaidia watu na wameshawasaidia watu wengi,sasa huwa nikienda kwao kumsalimia ananielezaga mambo mengi kuhusu hii nyumba tunayoishi".

Sasa niliamua mambo mengine kukoleza chumvi ili mradi tu waniamini na wakubali hatua za haraka zifanyike!.

Mimi " Jana nilipotoka senta nilikutana nae njiani akawa amesema nimsindikize hadi kwao,sasa nilipofika kwao mama yake akaanza kuniambia kuna mtu amewahi kuja hapa nyumbani kufanya zindiko,sasa lile zindiko lilifeli kwasababu yule mtu aliuawa kichawi"

Sasa baada ya kusema hiyo sentensi,nikaona Headmaster na mkewe wanaangaliana kwa mshangao!.

Mimi "Yule mama aliniambia adui wa hii nyumba ni mzee makono!".

Headmaster "Hivi huyo mzee makono ndiye nani?"

Mimi "Kama unakumbuka baba nimewahi kukwambia nilikutana nae akaniambia anakusalimia na akajitambulisha kwamba anaitwa makono"

Headmaster "Sawa nakumbuka lakini najaribu kuvuta picha ni mzee gani huyo"

Mimi "Unakumbuka ile siku Ema amening'inizwa darasani?"

Headmaster "Mmh!"

Mimi "Sasa siulikuja na wazee wawili kama unakumbuka,yeye ni yule mwemamba mrefu"

Headmaster "aaaaaaah!,hivi kumbe ndiyo anajiita makono!"

Maza mdogo "Ni nani?"

Headmaster "Si yule mzee lameki"

Headmaster "Sawa,sasa hapa ndipo naanza kupata picha!"

Aliendelea "Basi hilo jina litakuwa la kisukuma au la kwao huko,kama ni yule mzee jina lake ni Lameki"

Aliendelea "Na alikuwa rafiki yangu sana lakini siku za karibuni naona ananikwepa sana".

Headmaster "Sisi bhana tumekuelewa na labda kwa niaba ya mama yako mdogo nikuombe radhi kwasababu kuna mahali tulienda na tukaambiwa mambo mengi sana,hata suala wewe kumchungulia mama yako akiwa anaoga haikuwa kweli,tumeambiwa ni mtu mmoja ambaye anazo nguvu za kutosha tu,na kwa maelezo yako sasa angalau nduyo napata mwanga".

Aliendelea "Kumbe matukio yote yanayofanyika hapa ndani kuna watu ndiyo wanatufanyia hiyo michezo na tumeambiwa anayeongoza genge ni mwanaume mwenye nguvu haswa,sasa namna ya kukabiliana nae ndiyo changamoto,ingawaje kuna dawa tumepewa ndo tunataka kuzijaribu tuone!"

Alisema "Je mama yake huyo binti anapatikana wapi?"

Mimi "Wao wanaishi kule masairo"

Headmaster "Aisee mnazurura,hadi Masairo ushafika!"

Aliendelea "Huyo mama yukoje?"

Basi baada ya kumuelezea namna mama yake Monica alivyo,mzee alishangaa sana!.

Headmaster "Siyo mke wa mzee Kulola kweli?,maana kwa unavyoniambia ni kama yeye"

Aliendelea "Yaani yule mchawi ndiyo unasema anasaidia watu?,wale inasemekana walifukuzwa huko vijijini kwasababu ya uchawi!"

Baada ya kuniambia hivyo nikaona kabisa bila kujitetea nitaharibu mambo!.

Mimi "Hata mimi mara ya kwanza baba nilikuwa nasikia watu wanasema hivyo,lakini nilivyombananisha yule binti alikataa na hata pia nikaongea na mama yake akaniambia walikuwa wanasingiziwa tu,hakukuwa na ushahidi dhidi yao"

Headmaster "Mimi na yule mama hatupatani na yeye analijua hilo,kuna kipindi nilimtukana sana"

Mimi "Lakini baba asingekuwa mtu mwema asingeniambia haya yote"

Maza mdogo "Ila kweli,kama ni mchawi unadhani angesema hivyo?"

Mimi "Kuna dawa alinipatia jana akawa amesema tuitumie na kama ukikubali mimi nitamuita aje atusaidie ili kumnasa mtu anayetusumbua"

Headmaster "Hiyo dawa iko wapi?"

Basi niliondoka kwenda ndani kuchukua ile dawa na kuileta!.

Headmaster "Ndiyo hii?"

Mimi "Ndiyo baba"

Maza mdogo "Matumizi yake yakoje?"

Mimi "Hii tunaogea watu wote mama"

Maza mdogo "Baada ya hapo"

Mimi "Nitaenda kumuita mama yake Monica aje atuelekeze cha kufanya"

Headmaster "Shida tukitumia dawa zote hatutajua ni nani ametusaidia"

Aliendelea "Sawa,ngoja tumuone huyo mama,kama amekwambia yote hayo inawezekana akawa mkweli "

Kwakuwa nilifahamu ikifika usiku mama yake Monica angekuja kama alivyokuwa ameniahidi,sikuwa na presha na niliwaambia ningemfata kumbe mimi nilikuwa ninaujua ukweli.

Headmaster "Hivi huyo mjinga bado hajarudi tu"

Mimi "Bado sijamuona"

Headmaster "Ngoja licheze na dunia,sikuhizi badala ya kusoma limeanza kuhangaika na wanawake!"

Aliendelea "Mabinti wa hii shule niwa kuhangaika nao?,ngoja acheze na hiki kijiji kama hatujamuacha hapa".

Baada ya maelekezo ya namna ya kutumia ile dawa,namshukuru Mungu walikubali na walioga!,sasa kitu kilichokuwa kinasubiriwa ni mama yake Monica kuja,niliwaambia ikifika jioni nitaenda kumuita,lengo langu lilikuwa ni kusubiri mpaka atakapokuja mwenyewe maana nilichoka kutembea mpaka Masairo ambako kulikuwa mbali!.
Headmaster alihuzunika sana kusikia ya kwamba aliyekuwa akitufanyia uhuni pale nyumbani alikuwa huyo mzee aliyejiita makono ilihali jina lake ni Lameki.Nakumbuka Headmaster alisema akipatikana huyo basi angejuta kuzaliwa!.

Ilipofika mida ya saa 11 jioni,niliwaaga nikasema naelekea kwao Monica kumchukua mama yake!,sasa kwa muda ule niliona nitembee kwa kukimbia ili niwahi kufika maana palikuwa mbali!.Baada ya safari ya muda mrefu kidogo nilifanikiwa kufika kwao Monica.

Nilimkuta bibi yake Monica akiwa amelala kwenye jamvi kwa nje!,nilipiga hodi yule bibi akaitikia kisukuma,sasa kasheshe ilikuwa ni kuongea nae kumuuliza Monica na mama yake wako wapi kwasababu sikuwakuta!,nilipojaribu kumuuliza kwa kiswahili,yeye alinijibu kwa kisukuma,niliamua kusimama kando ya nyumba ili kuvuta muda angalau nikiamini wangekuja maana walikuwa wamemuacha bibi peke yake.
Baada ya muda kwenda ikiwa inakaribia saa 1 usiku,nilimuona Monica akiwa anakuja akiwa amebeba gunia kichwani na jembe mkononi!,alipofika nilienda kumtua ule mzigo ndipo nikakuta alikuwa amebeba mihogo mibichi.

Mimi "Mlienda shambani?"

Monica "Eeeh!,umekuja muda mrefu?"

Mimi "Nimekuja muda ndiyo"

Mimi "Mama yuko wapi?"

Monica "Anakuja,nimuacha hapo nyuma"

Mimi "Sasa hii mihogo mtamenya saa ngapi?"

Monica "Hii itamenywa kesho,nani wakumenya sasa hivi nimechoka"

Mimi "Sawa,kesho nikipata nafasi nitakuja kuwasaidia kumenya".

Ile mihogo ilikuwa ni ile michungu(rumala) iliyokuwa inavundikwa ikishamenywa kwa ajili ya kutengenezea unga wa muhogo(Udaga).

Basi haukupita muda mama yake Monica naye akawa amekuja na yeye akiwa na mzigo wa mihogo kichwani.

Mimi "Mama shikamoo"

Mama Monica "Marhaba mwanangu"

Aliendelea "Umefika zamani?"

Mimi "Ndiyo mama,nimefika muda tu"

Mama Monica "Tusamehe mwanangu,tulienda kuchimba mihogo tumtengenezee bibi yako unga wa kuondoka nao"

Mimi "Sawa mama haina shida"

Mimi "Sidhani kama nitakaa sana,maana nimetumwa ba Ba'mdogo "

Mama Monica "Mwalimu anasemaje?"

Mimi "Mama niliwaeleza jambo uliloniambia na wamekubali"

Mama Monica "Kweli?"

Mimi "Kweli mama"

Mama Monica "Basi wewe nenda ukawaambie nakuja,ngoja nijiandae nikawachukue wenzangu tunakuja"

Sikutaka kupoteza muda nilitoka nduki kurudi nyumbani kwasababu ilikuwa tayari ni usiku!.Nilifika nyumbani mida ya saa 2 usiku nikamueleza headmaster na mkewe na wao wakawa wanawasubiri!.
Kila mtu hapo nyumbani alikuwa amekwisha kuoga ile dawa na hata Ema ambaye nae pia wakati naondoka sikkumuacha ila alipo rudi alipewa maelekezo namna ya kuoga ile dawa!.

Sasa wakati usiku tukiwa tunakula,nilisikia mlango wa nje unagongwa,Ema alienda kufungua ule mlango na alikuja kuniita akisema naitwa!.Basi nilinyanyuka kuelekea nye ndipo nikamuona mama yake Monica akiwa na wale wanawake wawili,safari hii walikuja wakiwa wamevaa nguo za kawaida na wametanda Khanga!.

Mimi "Karibu mama"

Mama Monica "Haya tushafika,hao wapo?"

Mimi "Wapo mama,ingieni ndani?"

Basi waliingia mpaka uani wakawa wamesimama,mimi niliingia ndani kumwambia headmaster.

Mimi "Amekuja baba"

Headmaster "wewe msukuma njoo tule bhana"

Mama Monica "Nyie endeleeni sisi tumekula"

Headmaster "Toa viti hapo nje"

Basi nikatoa viti vya idadi ya wale kina mama nikapeleka!.

Tulivyomaliza kula,headmaster alitoka nje na mkewe ili kumsikiliza mama yake Monica!.

Headmaster "Mmh!,we msukuma lete maneno"

Mama Monica "Mimi nipo mkurya"

Mazungumzo ya kutaniana kati ya headmaster na mama yake Monica yalipokwisha maliza,sasa usiriasi ulichukua nafasi!.

Headmaster "Huyu kijana wangu amenifikishia yote uliyomwambia,na sisi tumeyapokea kwa mikono miwili"

Aliendelea "Hebu nisaidie maana nimeshahangaika sana na sijui nitakulipa nini nikifanikiwa"

Aliendelea "Hayo yaliyopita tuachane nayo,mimi na wewe tuanzie hapa sasa!"

Mama Monica "Tusipoteze muda,nileteeni karai na maji"

Nilichua karai nikasogezea mama yake Monica.

Alisimama akafungua mfuko uliyokuwa na makorokoro mengi yasiyoeleweka,alichukua unga akawa amemwaga ndani ya yale maji kwenye karai,baada ya hapo alizungumza kisukuma na mmoja ya wale kina mama ndipo mmoja wapo akawa amebeba lile karai na kutoka nje,haukupita muda akawa amerudi yale maji ndani ya karai yakiwa yameisha!.

Mama Monica "Leo wabaya wako wapo kwenye kikao mwalimu,hivyo wakiishatoka tu lazima waje hapa,wakifika hapa ndipo wataipata freshi"

Aliendelea "Sasa nawapatia hii kitu kila mmoja ahakikishe analala nayo kwa kuishikiria na usije ukaiachia"

Alitukabidhi watu wote kitu kikiwa kimeshonwa na kitamba kigumu mno,mimi sikupata shaka kuelewa kwamba ile ilikuwa ni irizi!.

Mama Monica "Hizi hapa mtapakaa kila mtu usoni kabla ya kulala"

Aliendelea "Mwalimu shika hii"

Headmaster alipewa kibuyu kidogo kama kile ambacho nilipewa mimi siku ile.

Mama Monica "Hiki kibuyu hakikisha unakiweka nyuma ya kona ya mlango"

Headmaster "Sawa"

Mama Monica "Mwanangu shika hii"

Na mimi pia alinikabidhi kile kibuyu kidogo na akanitaka nikiweke nyuma ya mlango kwenye kona.

Mimi na ndugu zangu hawa tutakuwa mazingira ya karibu,hivyo msiwaze!.

Headmaster "Kwahiyo hapa ushamaliza?"

Mama Monica "Kila kitu tayari"

Aliendelea "Msije mkapiga kelele kwa mtakachokiona,mkipiga kelele tu ,mtakuwa mmeharibu kila kitu!"

Mama Monica "Kama kuna mtu anajua hatokuwa mvumilivu aseme kabisa"

Baada ya hilo swali na wote kumuhakikishia tutakuwa wavumilivu ndipo aliendelea akasema.

Mama Monica "Mwalimu utakachokishuhudia wewe simama na chukua kibuyu nilichokupatia na ukifungue kikae wazi"

Aliendelea "Ukishakifungua tu,huyo mbaya wako atajuta kuitembelea hii nyumba"

Baada ya muda mama yake Monica na wale kina mama waliaga kuondoka,Headmaster na mkewe walitoka kuwasindikiza.
Wabeja sana.

#MaendeleoHayanaChama
 
Tulichomfanya Yule Mchawi hatokuja kusahau kamwe! - 25.

Baada ya Headmaster kutoka kuwasindikiza wageni,tuliamua kukaa kikao cha kifamilia na kuzungumza mambo kadhaa yaliyotuweka sawa.Sasa kila mtu alielekea chumbani kulala,baba mdogo na mkewe waliingia chumbani kwao,mimi na Ema pia tuliingia chumbani kwetu kulala.

Siku hiyo mle chumbani hakuna aliyepata usingizi kabisa,kabla ya kulala nakumbuka tulipakaa usoni dawa aliyokuwa ametupatia mama yake Monica,pia tukashikiria na zile hirizi mkononi kama alivyokuwa ameagiza tufanye!.Kadri muda ulivyokuwa ukisonga tuliona kimya,mimi nilianza kupitiwa na usingizi maana nilikuwa nimechoka sana!,kumbe wakati mimi napitiwa na usingizi,Ema yeye alikuwa macho kabisa na jamaa alikuwa na shauku ya kuona ni kitu gani kingetokea!.

Sasa ilipofika mida ya saa 8 usiku,nilishitushwa na Ema akiniamsha!.

Ema "Umesikia hicho kishindo?".

Mimi "Hapana,kishindo cha kitu gani?"

Ema "Kutakuwa na kitu nadhani!"

Ema alikuwa akiniambia kwa sauti ndogo kabisa na yenye uoga ndani yake!.

Mimi "Nyamaza"

Niliamka kitandani nikaenda kuwasha taa,nilifahamu kabisa kile kishindo Ema alichosikia hakikuwa cha kawaida na uenda wale jamaa wakawa wamekuja kama kawaida yao,kiukweli mimi kwa upande wangu sikuwa kabisa na hofu kwasababu kwa siku chache nilikuwa nimeshazoea yale mazingira ya kuwaona wachwawi laivu!.Nilimwambia na kumbusha Ema ya kwamba chochote atakachokiona asipige kelele wala kushituka!.

Haukupita muda,mara ghafla wakaonekana watu watatu wakiwa wamesimama mle chumbani huki wakiwa uchi kama walivyozaliwa,watu wale safari hii walikuja wawili wanaume na mmoja akiwa mwanamke!.Niliwaangalia kwa kuibia kama vile sielewi chochote!,Ema alikuwa akitetemeka sana na nilimpatia ishara ya kwamba atulie kabisa!.Basi nadhani yule mwanamke alihisi jambo maana niliona anamsogelea Ema akawa kama anamtisha aone kama amemuona,sasa alipoendelea kumtisha Ema nikaona anaweza kupiga kelele,nikaanza kumpigisha Ema stori ili kupotezea ile hali!.

Mimi "Mwanangu wewe piga kimya kabisa wala usimfanye chochote yule demu"

Ema "Yule demu mwanangu anazingua kinoma"

Mimi "Halafu Headmaster alisema ukamuamshe aandae yale masomo"

Ema "Halafu kweli umenikumbusha,ngoja nikamuamshe!"

Sasa wakati tunaongea yule mwanamke alirudi kwa wenzie na wakaendelea kushangaa shangaa,tulichokifanya na Ema pale kwa ule muda mfupi ni hakika walidhani hatuwaoni kumbe lengo lilikuwa ni kumuondolea Ema uoga na kuwapoteza maboya!.
Ema aliamka akatoka kwenda kumgongea Headmaster chumbani kwake ili aje ajionee!,sasa wakati Ema ameondoka,nilianza kujipigisha mruzi wa uongo na kweli ili kuikabili ile hali kwasababu ilikuwa inatisha si kitoto!..

Headmaster "Umughaka tacho omahe"

Baba alipotoka nje aliniita kwa kilugha nikawa nimetoka nje,sasa alianza kutueleza ya kwamba tusishituke na tuendelee kuwa watulivu,alitwambia Ema achukue madaftari tuelekee wote sebuleni ili iwe rahisi kuwakabili,mimi nilimwambia wao wakae sebuleni na mimi nirudi chumbani kukaa karibu na kibuyu kwa kazi maalumu!.
Basi wale watu wakawa wamepotea ghafla mle chumbani!,nilitoka nje kwenda kumwambia Headmaster.

Headmaster "Ngoja tusubiri,yawezekana wakawa wameshituka"

Mimi "Lazima warudi"

Headmaster "Halafu mbona yule mzee hayupo?"

Mimi "Uenda leo kawaagiza hawa"

Wakati tukiwa tunaendelea kuongea pale,Maza mdogo akamwambia Headmaster kwa kikurya kwamba,wale watu wako kule chumbani kwake na anawaona,Headmaster akamwambia atulie na asipige kelele!.Sasa tukiwa tunaendelea kuongea pale sebuleni huku Headmaster akijifanya kumpigisha Ema pindi,tukasikia kishindo kikubwa tena pale uani!.

Haukupita muda akawa ametokea yule mzee makono akiwa na usinga mkononi huku akiwa uchi kama wenzie!,akaja mpaka pale sebuleni huku tukiendelea kumpimia tu!,aliendelea kuangaza huku na huko na hatimaye akawa ameingia mle chumbani kwa Headmaster.Basi baada ya kuingia chumba cha Headmaster,Headmaster aliinuka kwa ghadhabu huku akisema "Lero n'uramanye uwe tombanyoko" (Leo utanitambua).

Sasa Headmaster alipoingia chumbani alijifanya kuongea na mkewe huku wakiwatazama,sasa nadhani mzee makono aliwaambia wale watu waende wakawalete watu wa kwenda kulima ili wakifika watuunganishe na sisi tuondoke!,wale watu watatu walitoweka wakamuacha mzee makono mle chumbani akitaka kufanya mambo yake ili amchukue Headmaster kama kawaida aje atuunganishe na sisi tuelekee kwenye kilimo cha usiku kisichokuwa na tija!.

Wale watu walipotoweka tu na mzee makono kubaki mwenyewe,Headmaster alichukua kile kibuyu alichopewa na mama yake Monica akakifungua,alipokifungua tu!,yule mzee akaanza kucheza kwa kuzunguka mle chumbani kama mwendawazimu!.Headmaster alituita tukaingia kumtazama,yaani kuna muda nilianza kumuonea huruma maana alikuwa kama amepagawa kwa kushikwa ugoni.

Kadiri muda ulivyokuwa ukienda,wale watu waliotumwa na mzee makono hawakurudi kabisa na nadhani watakuwa walishituka mapema!.Ile hali ilifanya maza mdogo kutoka kule chumbani akabaki mzee makono akizunguka chumba kizima kama mwendawazimu.Usiku huko hakuna mtu aliyepata usingizi kabisa,tumekuja kushangaa imefika saa 11 alfajiri bila kujua!.
Sasa ilipofika saa 12 asubuhi,Mama yake Monica alikuja akiwa na wale kina mama,alihuzunika sana kwanini tuliamua kuwaachia wale watu watatu wakaondoka!.

Mama Monica "Mwalimu nilikwambia,nadhani sasa unaniamini"

Headmaster "Sikuzote Msukuma nakuamini,si leo tu!".

Mama Monica "Kwanini mmewaachia wale washenzi?"

Headmaster "Wameondoka wenyewe"

Mama Monica "Nilikwambia wakifika tu,ungefungua kibuyu"

Headmaster "Nilipoingia chumbani kufungua kibuyu wakawa wameondoka akabaki mzee lameki"

Mama Monica "watasimuliana,hakuna kilichoharibika"

Aliendelea "Haya sema,unataka tumfanye nini huyu mzee"

Headmaster "Nadhani kama kuna uwezo muondolee uwezo wake asije akaponyoka halafu mengine utaniachia mimi"

Mama Monica "Huyu ameshakwisha,hapa hawezi kukuponyoka kamwe"

Aliendelea "Mimi namshughurikia halafu nakuachia wewe utajua cha kumfanya".

Basi mama yake Monica alimsogelea yule mzee akachukua ule usinga kisha akamvua shanga alizokuwa amejivika kuanzia begani kuteremkia kiunoni!,baada ya hapo kuna dawa alimpatia Headmaster akamwambia kukishapambazuka vizuri atampaka ile dawa na kisha atamuondoa mle ndani!.Mama yake Monica na wale kina mama waliondoka wakawa wamemuacha mzee makono humo ndani akizinguka kama mwehu!.

Kulipopambazuka,Headmaster alielekea kwa mwenyekiti wa kijiji na kutaka yowe ipigwe karibia kijiji kizima ili wananzengo wahalifiwe ya kwamba kulikuwa kuna tukio kubwa la kushangaza!,Basi yowe ilipigwa na watu wakawa wanakuja pale nyumbani huku wengine mikoni wakiwa wameshika mapanga na mafimbo!.Haukupita muda mrefu watu wakawa wamejazana pale nyumbani huku wengine wakichungulia dirishani wakishangaa lile tukio!.

Ilipofika mida ya saa 3 Asubuhi baada ya watu kujazana pale nyumbani,Headmaster alifanya kama alivyoambiwa afanye na mama yake Monica,baada ya kupakwa dawa yule mzee alikurupuka akawa anashangaa sana!,alikuwa akizunguka kitafuta usinga wake lakini hakuuona,ndipo Headmaster aliamrishwa na wananzengo ya kwamba amtoe yule mzee nje ya nyumba ili akapambane na viboko vilivyokosa huruma!.

Yule mwenyekiti aliamuru yule mzee avishwe nguo hadi kwenye ofisi ya serikali ya kijiji lakini wananzengo wakagoma,walisema inapaswa atembezwe kijiji kizima huku akila mboko na inapaswa siku hiyo hiyo ahame kijiji!.

Basi nakumbuka Headmaster alimuagiza Ema akalete viboko ili aanze nae mle ndani kwasababu alikuwa akimtafuta sana,viboko vilipoletwa kiukweli yule mzee alichezea kiasi kwamba sikutaka hata kuangalia,viboko vilipozidi aliamua kutoka ndani spidi akikimbilia nje,kufika nje wananzengo wakamdaka nako wakaanza kumsulubisha!.
Alitembezwa kijiji kizima huku akiwa uchi kama alivyozaliwa,kiukweli lilikuwa ni tukio la aibu mno!,sasa walipomfikisha kwake wananzengo hawakutaka mjadala,walimwambia avae nguo kisha atoke,alipotoka waliwasha moto nyumba yake na kila kitu kiliteketea kwa moto!.

Baada ya pale alirudishwa serikali ya kijiji na kutakiwa apotee kwenye kile kijiji ndani ya masaa 2!,hakutakiwa kubaki pale na wananzengo walimwambia watamuua endapo angebaki kwa siku hiyo!.

Lile tukio lilivuta hisia kubwa sana pale kijijini na kiukweli lilimpatia Headmaster ujiko na heshima sana ingawaje mimi ndiye niliyepambana sana mpaka kufikia ile hali.Headmaster aliogopeka sana tangu siku ile lile tukio litokee na hakukuwahi tena kuwa na mambo ya ajabu pale nyumbani.

Headmaster kwa baadae alihama ile shule na kuhamia huko Biharamulo ambako amejenga na anaishi hadi leo,mimi niliondoka na kurudi nyumbani kisha kuelekea shuleni Advance!.

Ema yupo hapo Shinyanga anauza duka la vipuri vya magari,amejenga na anaishi hapo hapo shinyanga.

Monica kuna wakati niliambiwa yupo Mwanza ila sijajua ni Mwanza sehemu gani!,kuna mtu nilikutana nae wa pale kijijini akawa ameniambia hivyo,kwasababu baada ya mimi kuondoka pale kijijini sikurudi tena hivyo tukawa tumepotezana na mpenzi wangu huyo!.

Mimi kwasasa nipo Dar es salaam napambana na maisha ya kukimbizana!,nina kiboda boda changu japo kimekwisha lakini tunapambana na maisha!.Kijiwe changu huwa ni hapo Bunju ndugu zangu!.

MWISHO.
Mkuu UMUGHAKA asante sana kwa story nzuri

Vipi Mwise anaendeleaje kwa sasa?
 
Back
Top Bottom